Anayeshtakiwa kumuua Mkewe adai haogopi Kunyongwa

JAMANI MAPENZI NI KIUMBE KAMA VIUMBE VINGINE...HUZALIWA, HUKUA, HUSTAWI NA HUFA...

MAPENZI YANAPOKUFA YASILAZISHWE...WATENGANISHWE...KILA MTU ACHA ACHAGUE NJIA YAKE...HII KULAZIMISHA SIJUI HAKUNA WA KUTENGANISHA ZAIDI YA MUNGU...MARA OOOH VUMILIA UTAMPENDA MBELE KWA MBELE...HII SIO SAWA...POLISI WANGELIINGILIA HILI WANGEEPUSHA MENGI...WAZAZI NA NDUGU KUJIFANYA HAYAWAHUSU NDIO YANAPELEKEA MAMBO KAMA HAYA...
 
wajina hapo umepuyanga.sababu ya kumsukuma mkeo ndo imesababisha kumuua.ni uongo 100%.sawa tuseme ni bahati mbaya.na kumchoma moto ni bahati mbaya?umeua bila kukusudia ila umemchoma moto MAKUSUDI
 
haya mambo yanatukuta sisi lakini hata wazazi wetu sometimes tunawaambia wavumiliane but bora kukubali watenganeee ndoa ni hatari sana msipofanana
Na wengine hata wakitengana anabaki kumfuatilia hasa wanaume hupenda asiwe na mwingine[emoji3][emoji3][emoji3], Mungu atusaidie jamani kuna mtu unakuta anavumilia mpaka unabakia shingo tu unachungulia kama mtu anayezama kwenye tope.
 
mimi toka mwanzo nilishasema huwezi kumuua mwanamke uliyempenda mwenyewe ukaenda kwao ukamtolea mahari.

ukiona imefikia hapo kuna jambo kubwa nyuma yake.

Mwamba hata wakunyonge sisi bado tunakuelewa sana …
 
Ndiyo hili nilikuwa nalizungumza kwenye post iliyopita. Kwenye ndoa, ligi ya kushindana na kulipizana visasi, eti huyu alikuwa anani-treat hivi basi na mimi nalipiza ni sumu mbaya sana. Mauaji kama hayo kwenye hii kesi hutokana na mambo kama haya.
Na ubaya ni kwamba siku zote asiyetakiwa kulipa visasi ni mwanamke yeye avumilie tu lakini mwanaume yeye ni haki yake kulipa visasi atakavyo
 
Ningekuwa judge kabla ya yote jamaa angekula fimbo tatu safi za kujiingiza ndoani ndipo mengine yafuate.
 
Na ubaya ni kwamba siku zote asiyetakiwa kulipa visasi ni mwanamke yeye avumilie tu lakini mwanaume yeye ni haki yake kulipa visasi atakavyo
Hili unalisema wewe. Ndoa inahitaji pande zote kuvumiliana, ila general rule ni kuwa mwanaume ndiye anatakiwa kuwa kiongozi wa nyumba. Nimeishi nchi zilizoendelea ambazo wanawake wana haki sawa na wanaume lakini hii principle bado ina apply. Tunaposema awe kichwa cha nyumba hatumaanishi awe na kura ya tufuru ya kuamua kila kitu.
 
Yotee ya nn ukiona mambo hayasomeki ni kutimua mbio sio lazima wote tuoe au tuolewe
 
Namuelewa sana jamaa…. Tunaweza kumuona Katiti sana, lakini hatujui alichopitia hadi kufika hapo

Kwa ujumla, jamii yetu ina jukumu kubwa sana la kusaidia wenye ndoa

Mapito ni magumu sana wajameni
 
Cha ajabu hakimu anakomaa kuwa kesi ya jamaa haikutikisa nchi, kuwa ni kesi ya kawaida.
 
Kitendo cha kua tayari kwa hukumu yeyote hata kunyongwa hadi kufa,kinaashiria kua mtuhumiwa amekubali kosa lake,na anaona kabisa kua ni haki kuhukumiwa kwa alichokifanya,

Sometimes majuto huja baada ya kitendo but hua ni too little too late.
Amekubali kosa lake kuwa aliua ila anaongea kisheria kuwa, kama ataamriwa kunyongwa anataka iwe ni kwa haki maana anajua kweli aliua lakini bila kukusudia hivyo hastahili kunyongwa. Hajutii kwa kilichomtokea.
 
Kuna uwoga kuingia kwenye ndoa
Ni bora nitafute mwanamke anizalie
Kuliko kuua mtu
Si mpaka uwe na akili hiyo, jamaa akili yake haiko sawa, atakuwa anavuta bangi hataivyo wanawake ni wavumilivu sana kwa vyvyote vile yapo matukio kadhaa atakuwa alishafanya huko nyuma yakiashilia tukio kubwa kama hilo sema mwanamke hakung'amua mapema au alidharau hiyo hali.Hata kama alinyonga Kuku badala ya kumchinja ni kiashilia tosha kuwa kuna jambo baya linakuja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…