Anayoyafanya Mwamposa kama ni kweli, Watanzania tusipuuze kila kitu

Mkishapigwa msilete vilio.
 
Huyu muhubiri watu wanampuuza lkn huyu ni mtumishi wa kweli kabisa wa Mungu,mama yangu sukari imemsumbua sana lkn baada ya kuombewa tu na Mwamposa hakika amepona kabisa sukari hakuna tena
 
Ilo ni kubwa la matapeli, wakristo mnaibiwa shtukeni!!!mmebakia Kobaz,kobaz
 
Aombe itokee computer ya ajabu, .Miujiza ni ile ile copy paste ya yesu. Muujiza ni kitu ambacho hakijawahi fanyika.
Mfano aombe andunje awe super tall na super tall awe andunje.
Augeuze huo umati wanawake wawe wanaume na wanaume wawe wanawake.
Mnashindwa miujiza na wanasayansi. Wameunda simu namskja bibi akiwa mbali. Acheni hizo.
 
Unaelewa hiki unaongea?

Kinachokuponya sio Mwamposa ni imani yako, yeye anakuwa ni chanzo tu cha kuamsha imani yako.

Akienda Hospital wagonjwa hawana imani, wanapona na nini?

Ndio maana ukimsikiliza vizuri huwa anasema au kuuliza, ni nani mtenda miujiza? Yesu.

Hata Yesu alivyoponya aliwaambia IMANI YAKO imekuponya.

Hata wewe hapo kinachokupa uwezo wa kufanya kazi ni Imani kuwa unaweza.
SIKU WAKIENDA HOSPITAL KUPONYA WAGONJWA NA KUKUSANYA VILEMA NA KUWAPONYA NTAAMINI WANATENDA MIUJIZA KWELI
 
Vipi kuhusu yule aliamini, nikigusa tu vazi la Yesu nimepona, alikuwa hamwamini Mungu? Na ni kweli aligusa na akapona ugonjwa wa kutoka damu miaka 12.


Siku hizi watu hawamwamini Mungu bali wanaamini mafuta,maji na keki ya Mwamposa.Yaani unakuta mtu badala aombe anakunywa mafuta ya Mwamposa akiamini shida itakwisha.
 
Kwanini mlimfitini kiboko ya wachawi wakati wote wanafanya kinachofanana?
 
Hivi ni nini maana ya miujiza? Maana naona vitu vyengine ni vya kawaida tu ila vinaitwa miujiza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…