Ndugu nikuhakikishie hakuna maigizo.
Ni nguvu halisi inafanya kazi.Pengine suala hapa la kujiuliza je ni nguvu za Mungu wa kweli?Shetani ana uwezo kama huo au hata zaidi.Shetani naye huwafanikisha watu wake na wanafiki wanaokataa neno na kumfuata mtu.
Jibu lipo katika maandiko.Mti mwema huzaa matunda mema.Mtawatambua kwa matunda yao.
Binafsi simjui Mwamposa kwa karibu lakini walio karibu yake watashuhudia matunda yake.
Hata hivyo ninaweka wazi tu msimamo wangu kuwa siamini matumizi ya mafuta ,chumvi au hata maji wanayaita living water.Tunaishi kipindi ambacho shetani anavaa ngozi ya kondoo ili kondoo wengi wamfuate.Ukifika wakati awachinje vizuri wakiwa kwenye himaya yake.Huwezi jua huenda hayo mafuta na vitu kama hivyo ndio muhuri wake unapigwa.
Kristo anapungua umaarufu badala yake watu na majina yao na mafuta yao ndio wanaotrend.
Haya mambo si ya kushangaza kuona kiboko ya wachawi na diamond ni washirika.
Sent from my Infinix X626 using
JamiiForums mobile app