Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,899
- 10,415
- Thread starter
- #41
Ndio maana nimeleta hii mada mezani kuna watu wanaujua ujamaa na ubepari kama neno tu. Tunahitaji mawazo yenu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio maana nimeleta hii mada mezani kuna watu wanaujua ujamaa na ubepari kama neno tu. Tunahitaji mawazo yenu
1. Ujamaa ni mfumo wa kiutawala ambao sekta kuu ya kiuchumi inaongozwa na serikali
2. Ubepari ni mfumo wa kiutawala ambao sekta kuu ya kiuchumi inaongozwa na watu binafsi ila serikali inabaki kusimamia na kuongoza sheria na taratibu
3. Mfumo mzuri unapaswa kufuatwa ni ule chotara yaani unachukua mazuri ya ubepari na ujamaa unapata mfumo chotara.
Sema hapa watu mnakosea kwa kushindwa kuelewa kuna ujamaa wa kiserikali na ubepari wa kiserikali pia kuna ujamaa wa kiraia (umma) na kuna ubepari wa kiraia (umma)Maswali yako yanaonyesha na wewe ni kati ya asilimia 95 ya watz wenye akili ndogo.....Siku za nyuma niliwahi fafanuzi kutoka katika akili yangu kuhusu mifumo 4
Nayo ni
1)Serikali ya kijamaa na umma wa kibepari
2)Serikali ya kijamaa na umma wa kijamaa
3)Serikali ya kibepari na umma wa kibepari
4)Serikali ya kibepari na umma wa kijamaa
Tumieni akili hapo juu ni lazima mnapo chambua serikali mchambue hivi nilivyo panga ndiyo mnaweza kugundua nini tatizo..
Mfano hapo nitakuambieni kuwa UJAMAA AU UBEPARI SIYO TATIZO TATIZO NI FORMATION KATI YA HIYO MIFUMO 4 HAPO JUU ....UBEPARI NA UJAMAA VYOTE NI MUHIMU SANA KWENYE TAIFA VYOTE VINATAKIWA KUWEPO KWA PAMOJA ILA KATIKA FORMATION ILIYO SAHIHI ZAIDI KATI YA HIZO FORMATION 4 KUNA MOJA NDIYO SAHIHI ZAIDI YA ZOTE NA KUNA NYINGINE HAPO KATI YA HIZO 4 NI MBAYA SANA ....Sasa kwa kifupi acha ni chambue kuhusu Rais Nyerere ukiniuliza kati ya hizo formations 4 Nyerere kakosea kwa kutumia hipi hapo nitskuambia kuwa Nyerere alijipiga pini na kujikwamisha na kukwamisha taifa kwa kutumia formation NO 2 hapo juu sasa tumieni akili kama Nyerere alitumia formation no 2 taifa likakwama je baada ya Nyerere kuondoka madarakani tulikosea wapi tena kwenye hizo formation 3 zilizo baki .....baada ya Nyerere kuondoka tulifuata formation iliyo mbaya zaidi kuliko ya Nyerere na ndiyo tunayo kwenda nayo hadi sasa japo kipindi cha JPM alichukua formation iliyo sahihi kuliko zote.... RAIS MWINYI alituingiza kwenye formation NO 3 AMBAYO NI MBAYA SANA NA NDIYO TUPONAYO HADI SASA KWA SAMIA FORMATION YENYEWE NI (SERIKALI YA KIBEPARI NA UMMA WA KIBEPARI ) hii formation inafanya serikali kuwa miliki ya kikundi kidogo cha watu kama mali yao binafsi ...na kufanya serikali kuwa kama kampuni la kibepari la watu fulani peke yao wanao jinufaisha wao binafsi na familia zao mfumo huu unaweza kuingiza taifa lolote kwenye machafuko ya wao kwa wao ni mfumo mbaya na muovu sana.
Kati ya hiyo mifumo 4 mfumo ulio sahihi ni mfumo no 1 ambao ni [emoji116]
[emoji95][emoji95][emoji95] (SERIKALI YA KIJAMAA NA UMMA WA KIBEPARI)[emoji95][emoji95][emoji95]
By GENIUS LWIVA THE GREAT [emoji106]
Ndio maana tumeitisha mjadala hapa tujaribu kupima uelewa wawatu juu ya hili.Hapo UDSM nadhani, Mtaala wa Shahada ya kwanza ya BA in Political Science and Public Administration haina somo rasmi la Socialism and Communism lakini Ina somo mahususi la Capitalism and Imperialism.
Najiuliza mbona tumehama kimya kimya kutoka Siasa za Kijamaa kupitia mitaala ya Vyuo vikuu!?
Kwa hiyo, mleta mada sina hakika kama utapata majibu unayotaka maana madesa hakuna ya socialism na communism.
Watu wengi huzungumzia ujamaa na ubepari lakini bado hawaelewi kwa kina.
Katika taifa letu la Tanzania tuna mchanganyiko wa ujamaa na ubepari.
Mfano mdogo uwepo wa sekta binafsi hiyo ni ishara ya kuwepo kwa ubepari. Na nikwambie tu kuna baadhi ya taasisi katika taifa letu zinatumia mfumo wa ujamaa.
Nakuomba sasa andika mawazo yako hapa kwa jinsi wewe.
1. Ujamaa ni nini?
2 . Na ubepari ni nini?
3. Na ni mfumo upi mzuri unapaswa kufuatwa na nchi ili iwe na maendeleo??
Wengine leteni michango"... Hawaelewi kwa Kina"...
Mara nyingi, maswali mengi ya kawaida ya wanajamii, husimamishwa katika wanda zisizothabiti kwa uelewa, tafsiri na mapelekeo.
Hili, pia liko hata kwenye visomo vyetu vya darasani hususani juu ya jamii, ustawi na maendeleo.
Haijalishi usomi wa kiwango cha uzamili ama uzamivu, kuna 'uelewa fulani' ni kama vile 'unazechezeshwa shere' ama 'jamii ya wasomi' wenyewe imeridhia upoyoyo kwa madanganyo ya 'majina' na 'uhitimu'.
Hili linafanya 'jamvi la utaalam' kuweza 'kufanya biashara', na huku vilevile umma wa wengi kuogelea katika mashauri ya juu juu kuhusiana na mambo na utashi -- vinavyosibu utamaduni, ustawi na maendeleo.
Utaalam hujengwa na fremukazi ya uelewa juu ya mambo, jambo linafanya shughuli hii ya maarifa kuwa ni 'ki-autocrat' hasa...
Utaalam na Maarifa huleta 'vichuguu' vya uweza na upeo wa kudadavua mambo...
Utaalam na Maarifa katika muktadha mmoja ni chaguo la mtu katika kutafuta uwezo na umahiri kumudu ufasaha, koherensia na vina vya tafsiri kwa mashauri ya kisomo.
Utaalam na Maarifa ni hasimu kwa 'maoni yasiyotaarifika' miongoni mwa wanajamii -- wanajamii ambao hawajakatashauri la 'kujua ilivyobora'.
Kimsingi, hili ndilo husababisha wale wenye kujua ilivyobora ama 'walio katika kujua' kuwaona wengine waliotafauti na hivi kama 'watawaliwa'--watu wanaofaa 'kuongozwa' na si 'kujiongoza'.
'Wenye kujua ilivyobora' ndiyo watu pekee katika jamii wenye >utashi wa kweli<.
Siku zote na daima--iwe duniani, ama kokote ulimwenguni kwenye sayari nyingine zenye viumbe watu, sura na tawala za kufanana na dunia, 'wenye kujua ilivyobora' ndiyo 'waamuzi' wa hatima ya utamaduni, ustawi na maendeleo--siku zote hawa huwa ni wachache, kulinganisha na umma unaofanywa na wengi.
Kinachosimama kati ya 'waamuzi' hawa na umma wa wengi ni 'ushawishi'; kwamba 'ontolojia ya taasisi' ni fanusi ya mifumo ambavyo wale wenye kujua ilivyobora hutenda ilivyobora. Basi, uweza na upeo wa wale wenye kujua ilivyobora ndiyo 'Mwangaza/Nuru' na 'Chumvi' ya wanajamii wengine. Kiufundi cha jamii yoyote habadilishiki kwa kutokea nje, wanajamii hubadilika maarifa na utashi utokanao na 'hisia za ndani' na tena za kudumu za 'mapenzi mema'.
Kwa minajili ya hili, mabadiliko ya jamii ni 'matokeo ya tafsiri' ijayo na taasisi na mifumo ya jamii yoyote kisomoni--ambavyo kiwakati ndiyo huzaa 'matendo' na 'kawaida' za jamii.
Hili ndilo linaloleta fasaha ya ukweli wa mambo--'matendo ya mtu ama jamii' ni zao la 'tunda la utaasisi' kupitia 'mifumo'.
Usifa-akili / Intelijensia, ujuzi wa kuona sura nyingi za mambo kwa wakati mmoja, huja na misingi ya kubaini utatusho wa 'Uono' na 'Ontolojia ya Taasisi' na 'Sura na Mienendo ya Jamii'.
Hivi ndiyo maana, ili kujua 'jana-leo-na kesho' ya jamii yoyote huhitaji ujuzi na ufundi wa Uono na Ufikirifu Mifumo.
'Uono na ufikirifu mifumo' ni starehe ya mtu yeyote 'mwenye kujua ilivyobora' na hali huo huo ni 'ukuta wa upeo wa mawazo na tafsiri ya mambo' kwa yeyote asiyejua ilivyobora.
SASA, mwenyekujua ilivyobora anao uweza wa kutenda ilivyobora.
Kuna mawili yanayowezekana kwa 'mwenyekujua ilivyobora'--kuwa na 'Nia rafiki' ama 'Nia isiyorafiki' mbele ya wengi wanaomzunguka. Nia rafiki ni kushiriki upeo wa mawazo, fikra na visomo/matendo na wengine kadri ifaavyo--wakati sahihi na kwa umma sahihi. Nia isiyorafiki ni 'kushikilia/hodhi mawazo bora, fikra na visomo' kwa manufaa binafsi--ya kadiri mtu mwenyewe ama taasisi, na tena kwa 'maslahi binafsi fulani ya kijamii'.
SASA, kuuliza 'Tanzania kama taifa inafuata mfumo gani wa maisha na kujiendesha(?)'; hili ni swali la kiufundi na linahitaji 'mafundi' wa uono na ufikirifu mifumo--si suala la mijadala ya fikra, mawazo na maoni. Hili ni suala la namna ya Elimu isiyofanania na Elimu tuliyoizoea--ya mashuleni ama vyuoni. Tena zaidi, hili hutaka upeo wa kuona na kubaina 'nje-ndani' ya mambo isivyokawaida.
Hili ndilo, 2023/2024 na kusonga, tunazungumza kwa minajili ya >Elimu 1.0, Elimu 2.0 na Elimu 3.0<...
Tanzania ni nchi-dola, na nchi-dola ni taasisi. Taasisi yeyote hujulikana bayana yake kwa vitendo vyake na maamuzi yake ili kukadirisha 'Sura na Mienendo ya Jamii'--jamii yake sovereini. Kwa Tanzania, kama ilivyo mataifa mengine yalivyo ni 'muktadha wa nchi dola'-->huwa na 'mwongozo wa kimaamuzi jamii' na 'kujichagulia' kama taifa moja<, misingi ya katiba na uhalali wa Taasisi Demokrasi miongoni mwa wanajamii wake.
Duniani kote, undani na uhalisia wa 'Dola' ni 'Fumbo la Imani'...
Kwa hivyo, fumbo la imani, ni jambo linaloweza 'kuondolewa pazia' kwa Elimu 2.0 na Elimu 3.0--si kwa Elimu 1.0 pekee. Elimu 1.0 ni shughuli ya 'kuwatengeneza wanajamii' kwa misingi ya 'watawala' na 'watawaliwa'--katika sura na nyanja yoyote ya maisha, utamaduni na ustawi.
Elimu 2.0 ndiyo uwanja wa Uono na Ufikirifu Mifumo ambavyo, 2023/2024 na kusonga, tunatumia 'fremukazi ya Uono na Ufikirifu Mifumo' kama nyenzo ya mtu yeyote na popote pale-- mwenye kujinasibu na 'Nia Rafiki' kutaka, kupenda na kujali kuelewa mapana na uhalisia wa jamii na 'miundo yake dhibitifu'--miundo dhibitifu juu ya maisha, utamaduni na ustawi.
Elimu 3.0 ni ugani mtu/jamii wa 'Wateule wa Kweli'; watu wenye kutafuta 'Mwangaza/Nuru' sahihi ya kutangamanisha 'Nia' za wanajamii... Elimu 3.0 ni ugani wa funguo za ufahamu, taamuli na makarama ya akili katika kuongozea njia za wanadamu kupitiliza 'mifumo ya utumwa' wa kinafsi na madanganyo ya fahamu za mwili na akili.
Kwa fremukazi ya Uono na Ufikirifu Mifumo, nchi yoyote kama taifa la watu, kwa kadiri ya hii kuwa ni 'Taasisi' ina mbegu tatu za 'UTU' wake, (1) Dini (2) Dola na (3) Elimu...
'Asiyejua ilivyobora' hufanywa kuamini 'nchi haina dini'--haya ni madanganyano ya vina na upeo wa kubaini ukweli wa mambo. Dini ni kitu cha msingi hasa katika kufafanua na kupambunua utu wa mtu/jamii; Asili ya ufahamu, Upeo na Makarama ya akili ni 'mawanda ya dini', >ontolojia na metafizikia<, ilivyo ni maisha ya ndani na nje mtu yeyote--ajue hivi ama asijue hivi.
'Asiyejua ilivyobora' hufanywa kuamini 'dola' huja na mamlaka ya kidunia yasiyojaribiwa/pingika na umma; haya ni madanganyano ya vina na upeo katika kubaini ukweli wa mambo kwa kuwa Dola ni 'Taasisi'--inaweza kumezwa na nia na matakwa ya watu wenyewe moja kwa moja na basi kupangua mpangiko wote wa Dunia, Tawala na Maisha.
'Asiyejua ilivyobora' hufanywa kuamini 'Elimu ni Ufunguo wa Maisha'--haya ni madanganyano ya vina na upeo wa kubaini ukweli wa mambo kwa kuwa Elimu iliyotamalaki duniani ni shughuli ya 'kumnunua mtu', kimifumo, na tena kwa hiyari yake mwenyewe ili kufaa 'hali ilivyo'--hali ilivyo kwa minajili ya Dunia, Tawala na Maisha.
Basi haya matatu ndiyo yatulete kwenye kumaizi ufunguo wa kweli wa maisha ya mtu ni 'NIA'-->Nia ya utu< wake inayomsukuma yeye kukizidi kiza chake cha mawazo, fikra na upeo wa vina vya tafsiri juu ya maisha yake duniani na kupita... Nia hii ndiyo inayofungamanisha Elimu 1.0, 2.0 na Elimu 3.0 katika 'Kiu ya Kujitambua' na 'Uono Sahihi wa Mambo yote'--yaliyo wazi wazi na hata yale yaliyositirika.
Kiufundi, 'Dunia, Tawala na Maisha' ilivyo kwa sasa ni sanaa, utundu na Hadaa ilikudumisha 'hali ilivyo' miongoni mwa jamii/jumuiya ya kimataifa. Dunia ya Mbabe/Mjanja/Mwenyekujibaruguza, katika kujua, atawale wazi wazi ama kimya kimya na tena pasipo kubughudhi 'ujinga/ushamba/kujisahau' vya wanajamii wengi waoifanya jumuiya ya kimataifa.
Ubepari kwa mfano, ni mfumo wa kinyonyaji, lakini kwa propaganda na uhuni mwingi--wa wazi na kificho--mataifa mengi yafyata mkia kuukata ama tuseme: hayana 'kujiongeza' ili 'kumalizana nao' -- labda kwa ajili ya yenyewe pia kujitafutia 'maendeleo ya kujipodoa' nao kama 'mpango mzima'..
Hili si hivyo kwa Tanzania kama nchi-dola...
Hili linahitaji ujuzi na ufundi wa kuzingatia 'Ontolojia ya Taasisi' ili kubaini 'mwanzo wa taifa' na 'hatima yake'...
Hata mbuyu ulianza kama mchicha, Taifa nalo huuanza na mwanzo teketeke na huishi kukomaa kulingana na uthabiti wa Taasisi zake -- Kiuongozi na Kujijengea uwezo.
Taifa la Tanzania, lini msingi na miongozo ya kinchi na tawala kama ilivyoasisiwa na wadau wa awali wa maendeleo ya watu na nchi -- >Mwalimu Kambarage Nyerere na Washirika, wadau wa utu na maendeleo duniani<.
'Dhana ya Uhuru' ndiyo azma na nia kuu ya Taifa, Dola na Serikali--na kiufundi, serikali ni chombo cha dola, na 'si dola hasa'; inaweza kuwa uso wa mbele wa dola lakini dola ni 'roho ya nchi'. Kama vile roho haionekani lakini mwili ni utukufu wa roho inayosukuma silika, muonekano na matendo ya mwili--ndivyo vivyo hivyo kwa dola na 'mihimili yake'.
Dola ni muktadha wa upatanisho wa 'Nia za Wanajamii' na 'Nia ya Kiumbe' cha 'kufikirika: 'Nchi-dola'; kwa namna hii Dola ni muktadha wa 'Nia' yenye kuratibu 'Ushawishi' wa Taifa kuwa kama kitu kimoja; miongoni mwa wanaojua ilivyobora na hata wale wasiojua ilivyobora. Na basi Dola, hufanyakazi kupitia watu wenyewe--wenye ushawishi/madaraka ya wazi wazi na hata wale wasio ushawishi ama madaraka ya wazi wazi.
Dola ni 'Mwili wa Ufahamu' juu ya 'miundo ya udhibiti' na pia mapana yote ya mifumo ya maisha/tawala/ustawi/utamaduni na maendeleo ya jamii inayofungamana nayo. Serikali inaweza kuwa ni 'kitu kinachokuja na kwenda', na hivyo basi dola ni kitu kinachodumu kupilitiza 'Serikali na Madaraka ya kisiasa'.
Ni uhalisia wa 'mwili wa ufahamu' unaofanya viongozi waandamizi, wastaafu, watumishi wa muda mrefu wa chama, serikali na jeshi kuwa hasa ndiyo sehemu ya 'Taasisi na Mifumo' ilivyo ni dola. Na vile vile kutengeneza mawezekano ya 'Dola ndani ya Dola'... Namna hii ya mambo ni suala linalojirudia kwa mataifa yote ulimwenguni, lina siasa zake za ndani kwa ndani na 'Ushawishi' kwa hatma za jumuiya za kimataifa...
Kwa hivyo kiuono na ufikirifu mifumo, dola ni sehemu na muktadha wa 'Kumbukumbu kiTaasisi'; ambavyo hata miili yote ya utendaji wa nchi na tawala unahitaji 'kukumbuka, kujikumbusha na kukumbushwa'. Yale yote yanayotajwa ni 'siri za serikali' ama taarifa za siri ni 'sehemu ya muktadha wa shughuli ya dola'. Kwa muktadha huu, siri si ishara ya 'nia ovu' bali sehemu ya utendaji inayozingatia 'usalama' wa maamuzi, kujichagulia na kujipanga--haya yote kama nchi-dola. Japo 'usiri' unaweza kutumika kama kichochoro cha 'Nia ovu'--muktadha wa maslahi binafsi ya mtu, chombo, na serikali; ni muktadha wa ukengeufu wa 'maadili' na 'miiko' ndiyo unayokadirisha 'elementi za kihuni' katika 'sehemu-mfumo' wowote inayotumia vibaya ule upendeleo wa 'mazingira ya kuwa katika kujua'.
Hili linatukumbusha umuhimu wa 'kujielewa' na 'Kuzingatia' maadili katika utendaji wa kiserikali, shirika ama hata chombo chochote cha kijamii--cha umma ama hata binafsi; kwa kuwa 'maamuzi, kujichagulia na kujipanga' ni kiini tete cha msimamo na mstakabali wa chombo kwa kuwa hufungamana na habari za uhatarishi wa kimazingira ya ndani na nje ya ustawi wa chombo husika.
Dhana ya chombo, matendo, ustawi na mazingira ndiyo hubidi ufundi kulandana na 'Nadharia ya Mchezo' ili kumudu sura, tawala na ustawi wa jamii ya watu. Kwenye ulimwengu wa leo, masuala ya nadharia ya mchezo ndiyo hufungamana na 'Uchumi' na maendeleo ya watu/vitu. Hili ndilo msingi wa kuelewa, Je, Tanzania inafuata mlengo upi hasa--Ujamaa ama Ubepari(?); Jibu la moja kwa moja, japo ni la juu juu, vyote viwili vinahusika kwa sasa... Ujamaa upo kwa kadiri ya tunu za taifa ilivyo ni Uhuru, Udugu, Haki na Amani--ni suala la 'Utabia wa Kishirika' unaotokana na 'Maono ya Waasisi wa Taifa'. Na tena haya yametaasishwa kikatiba sambamba na kulitangaza taifa la kijamaa na demokrasi. Kiufundi, haya ni mazingatio ya dola hadi hapo 'Maono Yabadilike' na basi katiba nyingine kutaasishwa...
Kwa hivyo kiufundi, Chama cha Mapinduzi ni 'chama-dola' na tena hiki hakina budi kuifuatisha misingi na miongozo yake kwa 'Maslahi ya Taifa'. 'Siyo dhambi' chama cha mapinduzi kutangaza kuachana na 'Imani za Kiujamaa' lakini jambo hili halipaswi kuja na 'utashi wa kisiasa' na tena kwa 'maslahi ya kisiasa'--hili linahitaji 'upeo' na 'ufahamu kumbaizi' wa wanajamii katika kung'amua mahitaji mapya, kama yapo, na kuyatetea wazi wazi; kinyume na haya Chama hiki matendo yake kiwakati ni 'kuchutama kwa muda' ili kutimiliza malengo yale yale yaliyoazmiwa na nchi dola--kuleta maendeleo ya watu na vitu.
Kwa 'Nia za Wenyekujua ilivyobora' zipo na Chama cha Mapinduzi; chama kilichoasisiwa kuwa ni >'Chama cha Wananchi wenyewe', 1977<. Na kama 'alama ya Ushindi' kwa kesho ya watu waliofaulu kupambana na mifumo ya kinyonyaji na tawala za kidhalimu; kwa Elimu, Uadilifu katia makusudi mema ya wanachi na serikali yao na zaidi kujituma na kujitolea katika huduma iliyo na 'Nia Rafiki/Njema' ya maendeleo ya watu--Tanzania, Afrika na Dunia yote.
Ujamaa ni Imani, kadiri vile Uhuru ni Kazi--watendaji wa chama na serikali kwa wakati wanaweza kuonekana kukengeuka na kujaribiwa na vishawishi vya 'kutafuta maslahi binafsi' kupitia ujasiria-mifumo, utendaji, upendeleo wa kimadaraka--hili ni jambo lililo ndani ya hesabu ya 'Waona Mbali' juu ya hatma ya Taifa; Japo kuwa hivi hakuhalalishi 'nia ovu'. Ubepari ni harakati za mpito za mifumo ya kibinadamu katika 'gombania goli' ya 'ukwasi wa kirasilmali fedha' na 'hijimoni' za jumuiya ya kimataifa. Ubepari ni shughuli isiyoishia na maendeleo ya kweli ya watu bali 'Vitu'. Tanzania kama nchi kwa sasa, kimkakati na tena kama taifa, tunatangamanisha maendeleo ya 'vitu' na 'watu' japo si kiuadilifu mkuu kielimu na rasilimali--rasilimali watu.
Wakati mmoja, siku si nyingi, ajenda kuu ya kitaifa itakuwa ni Elimu--elimu yenye tija kwa wanajamii wenyewe kwa kutafuta kuwajengea wananchi upeo na uweza wa kutekeleza 'siasa za ujamaa na kujitegemea'; japo kiufundi penye upeo halisi wa mtu na maendeleo hakuna 'siasa'. Siasa zipo kwenye 'Nia zisizo Rafiki' za makundi ya watu; watu wenye kujua ilivyobora wana muktadha wa matendo ulio ni 'meritokrasi na tekinokrasi'; siasa ni tunda bovu la misingi ya ubepari na demokrasia liberali; ambavyo maslahi ya kisiasa hujipambanua kwa utafutaji wa nguvu za kimadaraka na hatamu -- hata kama michezo ya 'vikundi vya maslahi binafsi' -- kunajisi 'utakatifu' wa dola yeyote kwa kisingizio cha 'demokrasia' na 'uwakilishi wa nia njema' za 'walio wengi'.
Maono na Busara ya Mwalimu Nyerere, ambavyo inaweza kufanyika na mtu mwingine yeyote mwenye Elimu 1.0, Elimu 2.0 na Elimu 3.0 ni kwamba >'elimu pekee yake ndiyo inaweza kuleta msingi wa kweli wa Maendeleo ya Watu'< na kisha watu hawa kuyatawala mazingira yao. Kuyatawala mazingira kwa maendelo ya vitu, ufanyaji maamuzi na kujichagulia. Tanzania kwa sasa hatuna utimilifu wa 'ELIMU' hii; lakini, In Shaa Allah--yaja!
Kwa hivyo, 'ubepari huleta maendeleo ya vitu' kwa utumikivu wa huduma-biashara ya vyombo vya fedha--kitaifa na mataifa; lakini miji mikubwa na maghorofa, si 'maendeleo' hasa, Lau miundombinu kama mabarabara na reli, usambazaji maji n.k huchochea yote mawili--maendeleo ya watu, pia vile vile biashara na ujasiriamali.
Maendeleo ni kuhama kutoka sura hafifu/duni ya ustawi wa jamii kuelekea kwenye sura bora; ama kusema pia kutoka katika muktadha usioridhisha wa maisha ya watu kwenda kwenye ule wenye kuridhisha. Kwa hivyo kiufundi, maendeleo si suala la tafsiri za kiuanazuoni na mapendeleo ya kutumia kigezo hichi ama kile 'kutafsiri maendeleo'--iwe kiukwasi wa fedha za mitaji ya uwekezaji, urefu wa maisha ama/na viwango vya usomi vya wanajamii...
Siku za mbele, msimamo wa jamii na ustawi wake utatahminiwa kwa 'Trizania'... Ikiwa inatupasa kidogo kumulika kuhusu 'Trizania'--hii ni instrumenti ya kujengea intelijensia -- kwa jamii yoyote kisomoni, iwe duniani ama hata kwenye stawi nyingine nje ya dunia. Hii ni pembe tatu ya kuakisi yale yote yafanyayo 'Uono na Ufirikirifu Mifumo'. Na ndiyo hujumuisha mawezekano ya kubaini 'mambo dhahiri' na yasiyo yale dhahiri ya 'sura, hadhi na mienendo ya jamii'.
Trizania inatoa mnyambulisho mwepesi wa miktadha ya 'Kujitambua', 'Uwezo wa Kiakili wa mtu/jamii/chombo/dola/jeshi kama taasisi', na 'Utukufu wake kwa minajili ya Sura na Mienendo yake'. Ubepari kwa mfano, kwa uono na ufikirifu mifumo na kupitia trizania ni 'mfumo mfu wa kiuchumi'. Unakosa mizania kwenye mapana ya 'Kujitambua' na vile vile unapelekea taasisi za utekelezaji wa haki kuwa utendaji wa kijuujuu mno na usio uhalali wa 'haki' ila kwa 'maridhiano ya kijamii'. Ubepari hauwezi 'kukua na kuongezeka' bali kwa dhana, tafsiri na 'misingi mushkeli' ya utekelezaji wa maendeleo-uchumi... Ubepari unastawi kwa kunyonyana, kuzidiana kete na maarifa yenye hila hata pia njama...
Ujamaa kupitia Trizania, ni uhalisia wa 'Sovereini Jumuifu'--unawezekana kwa 'mifumo hai ya uchumi' na 'elimu ya kutosha ya kujitambua' na tena yenye kuujengea umma uweza wa 'kushtukia hila ama/na njama' za utu usio na chachu ya 'Haki ya Kweli' na 'Udugu wa Wanadamu wote'.
Kwa hivi, utu usio na chachu ya haki na udugu wa kweli, unaweza kudhibitiwa na mambo ya kimatiriali, visomo vya kimatiriali na hisia za hofu/kujihami... Huwa na upofu wa kiroho unaoweza kudhibitiwa vema na udini wa kimiundo dhibitifu.
Kuishi ni Duniani ni vema kutohaika na 'vitu na mali' ila kutambua maarifa halisi ya kujitambua ndiyo tunu kuu ya Uhuru--Mwenge wa Uhuru... Ni vema 'Kujisahihisha' kupitia Uono na Ufikirifu Mifumo ili kubaini vitu vya 'fahari mwili' na tena 'fahari ya roho'--kwa kuwa utashi wa kiroho ndiyo shughuli iliyodukuliwa na 'udini wa kimiundo-mifumo'.
Isijekushangaza wengi ikiwa mtu atatafuta kwa dhati nuru na mwangaza wa 'Mwenge wa Uhuru'; anaweza kuja 'kujua ilivyobora' kuliko anayodanganyika nayo kwa 'elimu za mchongo za kidunia'. Elimu za kidunia zinaigiza 'ukweli duni/hafifu' wa kiroho... Mwanadamu anayeishia na domaini za Elimu 1.0 bado 'si mtu huru'...
...
Miji na majengo makubwa ya kibiashara kwa mfano, hivi ni vielelezo vya 'uhifadhi wa ukwasi' wa kifedha na 'kujibana' ili kujiimarisha kimitaji na biashara; tafsiri ya kuhodhi mali kulingana na tamaa/hofu/ na kujitunza (Ilivyo labda ni uchoyo). Mambo ya msigano kati ya 'wenye nacho' na 'wasio nacho', epitomi ya akili ya kimaskini. Sheria za 'mali' na 'Jinai' si lolote basi ila muakisiko wa jamii iliyojikubali kwa mashauri mushkeli ya kiutu(kiutu/roho), ustawi na maendeleo kwa mwamvuli wa kuimarisha 'haki' ya 'kufurahia' matunda binafsi ya maisha.
Tanzania kwa mfano, kikatiba na chama, kuna angalizo la kuepusha njia kuu za uchumi kuwa mikononi mwa watu wachache; pia 'utajiri wa nchi' na fedha vitumike kutangamanisha maendeleo mjini na vijijini--lakini maendeleo kwa mashirikiano ya sekta binafsi na ya umma, katika mawezekano ya kibepari husukuma hata mawezekano ya sekta binafsi kujiingiza katika kuhodhi 'biashara' ya huduma za jamii/kuendesha njia kuu za uchumi kwa sura moja hata ingine... Mambo ya Fedha, uwekezaji na uwezeshaji...
Tanzania kujinasibu na mambo ya fedha, uwekezaji na uwezeshaji ni sehemu ya 'mikakati'--mikakati katika 'nadharia ya mchezo'. Hili halimaanisha Tanzania, kama nchi-dola inadumisha demokrasia liberali na masoko huria kama 'tunu' za taifa kimaendeleo ya jamii...
Ujamaa ni fahari ya utu bora wa kesho ya Tanzania kiwakati, japo kwa wengine kesho hiyo 'walishaiiona' na kuchora mrejesho wa mapito ya kitaasisi. Ndivyo basi, upo muktadha wa kidola uliokana kwamba kesho imeshathibitika ukweli wake na basi misingi ya nchi, watu, tawala na ustawi kuoneshewa njia pasi kujali 'upofu wa wengi' ama 'imani haba' kwa kesho hiyo yenyewe yenye utukufu... Upande wa muktadha wa kidola ambao 'haujajaliwa' kuona kesho ndiyo kujishughulisha 'mambo ya nadharia ya mchezo' hata 'maarifa na visomo 1.0 (mushkeli)' vya uchumi -- mikakati, ukuu kisiasa za kimaeneo na masuala yote ya 'mkuki'--yote kheri kwa namna fulani...
Kwa hivyo, kimsingi hasa, mataifa mengi duniani yanadumu kuwepo, kutenda na kujidadavua kwa 'utatu usiomtakatifu' wa dini, dola na elimu; ni muktadha wa Elimu 1.0, 2.0 na 3.0 ndiyo utakuja kuweka yote sawa na basi wengi watastaajabu kuja kufahamu ni kwa vipi mataifa, kidola, 'hufadhiliwa uwepo na nguvu zake' na 'dini', 'majeshi' na 'taasisi za elimu' -- kwa ufundi wa 'wadau' kwa ufundi wa hayo matatu 'kufichiana siri' kitaasisi kama miundo dhibiti.
Dini kwa mfano, zilivyo kama miundo ya kitaasisi, zinahofia 'elimu' inaweza kuibua mijadala na sintofahamu ikitokea kweli fulani za maisha zikiwekwa bayana ama kuachiwa kutafitiwa bila mipaka. mfano wa vitu hivyo ni kama vile ukweli juu ya 'viumbe-watu' wengine kutoka 'nje ya dunia' na walio 'ndani ya dunia yetu--juu na ardhini', ukweli wenye nasibu kuleta taharuki juu ya maisha duniani na kupita... Viumbe-watu hao wapo, na mambo yao yana 'kapu jingine la mashauri' kuhusiana na stawi za kimanyota' ambavyo jamii ya dunia 'bado kidogo haijawa tayari' kupokea habari zake na 'siasa za mambo yake'...
Dola kwa mfano, zilivyo ni taasisi ndani ya taasisi huwa na hofu na 'nchi kutotawalika'--anakia. Hili ndiyo kiufundi hubidi kutengeneza mazingira ya 'uhuru wa kuabudu' ama 'kujichagulia mfumo wa dola-dini'... Japo kuweka watu pamoja hubidi kutengenezwe 'itikadi' ama 'ufundi' ili kuwaunganisha watu na 'kuwauzia wazo' la 'Ujamhuri'. Hili ndilo linafanya kuwa na 'mataifa' na basi 'nchi nyingi duniani' na kumbe binadamu wote ni wale wale juu ya uso wa dunia... Mipaka ya nchi na rangi za ngozi, kwa mfano, ni mambo ya juu juu tu... Wenye kujua ilivyobora wanatambua dola ni 'matayarisho' tu ya kiutu ili kutokomeza kidogo kidogo tofauti za kimawazo za binadamu hapa duniani... Walimwengu wakijitambua na kuamka kikamilifu hakuta kuwa 'nchi' kama nchi-dola bali 'ubinadamu' na 'ujamaa' katika nia, vitendo na kheri ya utamaduni jumuifu...
Elimu kwa mfano, inadhibitiwa kwa ruzuku, mishahara, zawadi na sifa nyingi za kitaaluma ili isitokee 'watu kufundisha' ama 'kufundishana' mambo nje ya kanuni, taratibu na mamlaka ya taasisi za elimu duniani. Lakini yapo mengi tu yanayoweza kudadavuliwa kupitiliza 'mafundisho' ya darasani ama/na 'usahihi wa kisiasa'. Moja ya hilo kwa mfano, ni ubatili wa kuhofu ule muktadha wa watu kujua mambo zaidi ya 'kawaida ya miili' na 'fahamu za kawaida'. Hili huchukua sura ya kudai eti, 'elimu/sayansi' na 'dini' havipikiki chungu kimoja.... Huu kiufundi ni uwongo kabisa; binadamu akidanganyika asihoji kuhusu misingi ya 'dini' na 'sayansi' -- hata kupitiliza kawaida, ndiyo basi atapumbazwa na 'fikra za uongo-na-kweli' kuhusu 'dola', 'taasisi za miundo-dini' na 'sayansi za kimatiriali'... Sifa zote za kitaaluma na umaarufu wake ni 'hongo' kwa wanaofikiri wanajua--wajione wamejua vya kutosha na kumbe 'wamefaulu elimu ya mchongo' ili wacheze 'sikinde ya ngoma ya ukae'...
Kwa hivyo kiufundi, matatu haya huishia kusokotesha utatu wa 'majeshi', 'vyombo vya udhibiti wa uchumi kupitia sarafu za fedha' na 'Elimu za Mchongo'. Nguvu halisi ya dola yeyote ni jeshi--siyo serikali hasa; hakuna nchi-dola iliyohuru kiukweli kweli, kwa kuwa mwenye kutengeneza sarafu na kutengeneza 'masharti na miongozo' ya fedha ndiye 'dola halisi ya kidunia' na 'Mwenyehofu na Elimu' na 'mwangaza kwa watu' ndiye anayeratibu elimu na taaluma zote kuanzia sayansi za jamii hata 'kurusha roketi'... Uhuni wote wa 'kushindana kurusha roketi duniani' ni theata... Anayechezesha mchezo ni 'fundi wa dini' na 'kuchezea akili za kiimani' na kuwapanga watu duniani kwa 'amani' na 'upatanisho', kwa nje, japo ukweli mambo yake ni zaidi ya 'dini' na 'siasa za ndani kwa ndani' za watawala wa watawaliwa duniani... Na labda si 'watu/mtu' hasa...
Kwa hivyo, kwa Tanzania Ubepari ni 'namna' na si 'mwisho wa jambo'.
Katiba yetu, ni fupi na ni ya kiufundi hasa, ni rahisi wasio na meriti na uweza wa mafikara kudhani 'imepitwa na Wakati'--mapungufu yote yanayoweza kubayanishwa -- yanaweza kusahihishwa na 'Harakati na Utendaji wa Chama na Serikali'. Ingawaje, ushawishi kutoka nje ulitutaka tutoe siasa katika jeshi, katika kukubaliana na yale ya marekebisho ya kimuundo; kwa muktadha fulani jambo lile ilikuwa ni 'kutengeneza amani' na 'wakubwa'. Vivyo hivyo kujinasibu na ulimwengu wa soko huria ni tamu/chungu ya kukubaliana na kweli za kiufundi juu ya uduni wetu juu ya 'uwezo wa jamii' kupambana na ubeberu; suala linalotakana pia na muktadha wa wanajamii wenyewe, kupitia viongozi wake wawakilishi, kuridhia kujikwamua kiuchumi kwa ajili ya 'hisani ya misaada' -- pale 'kasi ya elimu ya watu wazima' na 'uzoefu wa kusimamia shughuli za chama na serikali' vilipokuwa vinachelewa 'kuoana'. Na basi kuruhusu milango ya unyonywaji na unyonyaji miongoni mwa 'jamii ya ndani' ama/na pia 'jumuiya ya kimataifa', imekuwa ni njia ya mkato, kwa masaibu ya maendeleo na ustawi wa jamii lakini haliondoi dhamira na mashauri ya miongozo ya taifa juu ya 'Ujamaa'.
Mwalimu Kambarage alipokiri kutojutia 'mwanzo' wa taifa letu kujinasibu na Ujamaa, ilikuwa hivyo kupitia 'mwili wa ufahamu' juu ya 'mbegu ya taifa changa la watu' ambavyo 'nia rafiki' haitetereki juu ya dhamira za kubangaizia ubepari: 'Hauwezi kuacha nchi changa isonge mbele kimaendeleo kwa nguvu ya masoko! Masoko ni fedhuli kwa watu maskini -- kwa maana hayana moyo wala akili... Mzee Mkapa naye pamoja na jitahada bora za kuendeleza marekebisho ya kimiundo, wakati wake ulifika hasa ambapo alikuwa anakiri hatuwezi 'kutoboa' kwa fedha za wafadhili! Na yeye, hapa na pale alipata kuzungumza mbele ya jumuiya ya kimataifa kwa nini, sisi mataifa machanga tumetegwa na tumejaa katika mtego... Umaskini wetu umekuwa ni wa kifikra na upeo wa mawazo zaidi juu ya watu, maendeleo na kujichagulia.
Sasa, haina maana tunavyokopa fedha leo kama taifa ili kujenga na kuimarisha miundo mbinu, lau katika hiraki za uchukuzi--ardhini, majini na hewani, ndivyo tunazidi kupotea katika 'Ubepari' na 'mtego wa Madeni'. Haya yanafanyika ndani ya misingi ya 'nadharia ya mchezo'. Ikiwa, kufikia ukubwa fulani wa utekelezaji wa mikakati hii ya maendeleo ya vitu, miradi ya kimkakati, itakamilishana na 'Elimu' basi huko mbele hatuna 'mzigo wa madeni' hasa. Kuna namna ya Elimu inayoweza kufanya madeni yote ya namna hii kuja kutokuwa mzigo wa 'serikali' ya siku zijazo...
Na kuna mengine leo, hii hayafikiriki -- na bora yasifikirike hivyo kwamba hata madeni siku za mbele yanayo nasibu ya kuyeyuka yenyewe (!)
Ubepari umefika mwisho, unaweza kutoweka siku si nyingi--kwa watu wa 'kimikakati ya mkakati', wale wa 'dola ndani dola', yapoyanayofahamika wazi kuwa yanaweza kuumaliza 'ubepari' hata sasa na leo. Mambo haya yapo, yanafahamika na yanadhibitiwa kote duniani. Ni kwa kuwa hata katika 'dola ndani ya dola' ya dunia kuna wenye 'nia rafiki' na wale wenye 'nia isiyo rafiki'.
2023/2024 tayari watu wa 'nia rafiki' wanapata ushindi na basi ulimwengu hautakuwa ule ule kama wa jana -- kesho ya karibu. Kuna viwili vinakwenda kuusumbua ubepari : 'Akili Bandia' na 'Tekinolojia za Kimapinduzi'. Hivi viwili havizuiliki na 'vinawatupa mkono' wadau wote wa 'Nia zisizo rafiki' kwa 'umma' na 'maendeleo' na 'ustawi'....
Tekinolojia za kimapinduzi zinakuja, na hizi zitabadili mengi ya uchumi, kazi, uchukuzi na uendeshaji wa shughuli za walimwengu. Moja la mfano, duniani wanajamii na wanataaluma hudanganywa kuhusu 'mafuta' kana eti ni 'rasilimali inayokwisha' na tena inatokana na 'masalia'--jambo hili si kweli--haijalishi linafundishwa shule ya msingi hadi chuo kikuu cha kiufundi...
Mafuta hayatokani na masalia, bali maji katika mgandamizo mkubwa mno chini ya miamba na nyufa za ardhini chini mno tena kwa mchakato 'alkimia' wa kimolekyuli. HIli linafanya mafuta kuwa s bidhaa inayokwenda ikiisha kupatikanaji wake, lakini upatikanaji wake unaweza kuwa wa kujijazia ikiwa matumizi duniani yatazidi sana. Hili kwa sehemu, limezaa 'siasa za mabadiliko ya tabia nchi' na 'hewa ya ukaa' japo kiukweli hasa haya ni sayansi ya uongo-na-kweli unaratibiwa kiufundi hasa kwa fedha za hongo (visomo kamisheni/ruzuku visomo mahsusi) kwa taasisi za elimu na wataalam na 'shule' za mataifa duniani...
Kutengeneza mchongo wa kuachana na 'matumizi ya mafuta' duniani ni moja ya jitihada na 'kuchezesha manufaa ya viwanda' na 'tekinolojia za mapinduzi ya mchongo'!. Hili litukumbushe, nishati ni rasilimali ya kimkakati na ufunguo kwa michezo na uhuni wote wa kibepari...
Tekinolojia zinazotumia vyanzo mbadala wa nishati kwa mfano, duniani kote ZINADHIBITIWA mikondo yake ya utafiti na urasmishaji. Marekani kwa mfano, hili linatendeka kwa udhibiti wa 'patenti za uvumbuzi' na kunyang'anya watafiti na wagunduzi wa tekinolojia zinazoweza kudaiwa kuhatarisha 'Usalama wa Nchi' kwa mapelekeo ya utengenezaji wa silaha ama vinginevyo. Kwa hivyo, inafahamika kwa wadau wa sayansi na tekinolojia--suluhu zinazoweza kumaliza kero za 'maji safi na salama' ama 'umeme wa kutosha', kwa kila nyumba zipo hapa duniani; na nyingine nyingi za ajabu kabisa (!) na tena 'zimekuwepo kitambo tu sasa'; na ni suala la muda tu, kupitia 'Nia rafiki' zitakuwa hadharani moja baada ya nyingine...
Kwa hivyo, tuwe macho na tusihadaike sana na 'siasa za walimwengu' bali tuitafute 'ELIMU' ilivyo muktadha wa 'Mwenge wa Uhuru'...
'Mfumo' ni sehemu ya Utamaduani, Maisha, Stawi na Maendeleo--si porojo za kuhorojoka.
Ukiona Elimu ni Kazi, endelea kujaribu Ujinga... Lakini si fahari, kuonesha viroja vya hoja na basi 'kuijaza seva kwa upupu' wa kuhorojoka.
'Mfumo' ni kishikizo cha 'falsafa' na 'filosofia'...
Filosofia: Mfumo ni Uono fasaha wa 'fikra, taasisi na sura mienendo ya jamii' kama 'kitu kimoja';
Falsafa: nje ya haya ni 'falsafa, urazini na udunya wa kujitakia--kutokuwa na nia ya dhati 'kujua ilivyobora'...
Hii post kama Ina Fanya trolling ambayo si nzuri wakati mwingine!ilivyobora