Andika neno lolote chungu, zito, lenye maumivu ambalo hautakujaa kusahau mtu alikutamkia


Uliwaroga nini??πŸ€”
 
Siwezi kuolewa na wewe nimeenda kwa mganga nimeambiwa mama yako mchawi anataka kuniuwa au kunipa stroke,endelea kuwaendekeza ndugu zako utazeeka bila kuoa.
 
Niko nje ya mada kidogo ila naomba niteme nyongo yangu hapa

Niliwai kumuandalia mtu ambaye nilikua nikimpenda sana birthday party ila hakujali na wala hakuja .Nilijinyima sana kumfanikishia ilo jambo ila hakujali niliumia mno mapenz haya baunsa
 
"Hujachangia hata tofali moja wakati najenga nyumba yangu"
" Hamna kazi ambayo utaweza kuifanya wewe ngoja tuone"

Namshukur Mungu niliondoka home leo nipo mkoa mwingine najitegemea na kuilisha familia yangu na mengine mengiπŸ™πŸ™
 
Wakati naendesha bolt, mama mmoja anaitwa Evelyn, anakaa ilazo, tulishindwana nikamshusha kwenye gari kabla hata ya kufanya safari. Akaondoka zikapita dk 2 akatuma msg hutakaa ufanikiwe mbwa wewe.

Leo namalizia nyumba ya binti yangu itega, block ambayo kwa plan ya jiji, ni marufuku kujenga flat house.

Ipo siku nitampigia yule mama nimshukuru. Namba yake nilihifadhi mahali pa muda wote
 
Siku nyingine mkianzisha nyuzi kama hizi mnatutag na sisi watumishi tupate points za kusadia watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…