Andiko hili katika Biblia ndio kifungu katili zaidi kuwepo Duniani. Je, ni kweli Mungu aliamrisha ukatili wa namna hii?

Andiko hili katika Biblia ndio kifungu katili zaidi kuwepo Duniani. Je, ni kweli Mungu aliamrisha ukatili wa namna hii?

Status
Not open for further replies.
Mungu haonei.

Biblia Iko wazi.

Kwa vipindi tofauti Waamaleki waliwavamia Wana Israel na kuwapiga na kuwapora mali zao kipindi hiko waisrael wamemwasi Mungu.

Waliipoanza kumlilia Mungu na kumwomba Awasamehe dhambi zao.

Ndio Mungu anawaamuri wawachakaze Waamaleki.

Kwa msiiosoma maandiko, Waamaleki walikua eneo la NEGEV NA SINAI YA SASA..

Waamuzi 6:3---7 ....
Basi ikawa, hapo Israeli walipokuwa wamepanda mashamba, Wamidiani wakakwea, na Waamaleki, na hao wana wa mashariki; wakakwea juu yao;

wakapanga marago juu yao, na kuyaharibu hayo maongeo ya nchi, hata ufikapo Gaza,( Gaza hii ndio hii hii ya Leo ambayo Wapalestina wanasema ni yao, hakika Israel aendeleze kichapo tu na aichukie Gaza) wala hawakuacha katika Israeli riziki ziwazo zote; kondoo, wala ng'ombe, wala punda.

Kwa maana walikwea na ng'ombe zao na hema zao, wakaja mfano wa nzige kwa wingi; wao na ngamia zao pia walikuwa hawana hesabu; nao waliingia katika hiyo nchi ili kuiharibu.

Israeli walitwezwa sana kwa sababu ya Wamidiani; nao wana wa Israeli wakamlilia Bwana.


Baada ya hapo Kichapo kikawashukia Waamalaki na Mungu akakifita kizazi chote Cha Amaleki, uzao wa ESAU.🤣🤣🤣

Hili Taifa ni la Mungu
Sijui wafia dini mlilogwa wapi, yaani wewe utende kosa, then waje kuadhibiwa wajukuu wako ambao hawahusiki na Ushenzi wako wala makosa yako, hii Ndio haki?.

Alafu mujue kuwa huyo Mungu wenu hajifunui kama Mungu wa waisrael pekee Bali dunian nzima, Sasa anapochagua upande wa watu wa kuwafanyia unyama hii inaleta mashaka kuwa huyo Mungu wa ukristo na uyahudi si Mungu wa dunia nzima wala si Muumba bali ni Mungu wa jamii Fulani tu, ambayo hapendi kuona ikionewa na wala hutoona akiwasaidia watu wa jamii zingine wanapopata shida kama anavyowasaidia hao wayahudi,

je hao watu wa mataifa mengine si viumbe wake?, hana huruma nao? Mifano hata hapa Afrika ambapo Kuna mamilion ya watu ambao wameteseka kuliko jamii yoyote Ile duniani, je huyo Mungu wa uyahudi aliingilia Kati kuwasaidia Hawa waafrika ambao mpaka Leo wanaonewa ama ni Israel pekee inapoonewa ndipo anaingilia Kati?.

Kuna namna mtu ukiruhusu matumizi sahihi ya akili utaona mapungufu ya hizi dini na mfundisho yake ya kipuuzi yanayohamasisha utengani, ubaguzi, mauwaji, ugaidi, na Ushenzi wa Kila aina.

Mungu wa ukristo+uislam si Muumba wa Ulimwengu na wala hausiki na maisha ya viumbe dunian, Bali ni Miungu ya watu weupe, ambayo imepandikizwa mpaka kwa watu weusi waache uhalisia na kukumbatia uongo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom