Angalia jinsi CCM wanavyochezea hela zetu hapa lazima deni la taifa lifike trilion 107

Angalia jinsi CCM wanavyochezea hela zetu hapa lazima deni la taifa lifike trilion 107

Nadhani kuna kitu hakiko sawa na huyu mwanamke, au hata washauri wake ni watu wenye upeo mdogo sana.

Ni kama hawa watu wanawaona waTanzania kuwa binaadam duni sana wasiokuwa na akili nzuri kichwani.
Hebu fikiria unampa mtu matakataka kama hayo yaliyojazwa kwenye huo mkoba, halafu kwa kufanya hivyo mtu huyo akupende na kufanya lolote utakalotaka akufanyie!

Lakini tuseme ukweli, hili lina tofauti gani na chumvi au shanga walizokuwa wakipewa mababu zetiu enzi zile?
Yaani waTanzania tumeporomoka haraka, toka enzi zile za Mwalimu Nyerere, tulipo amini na kujivunia utu wetu, na kuwa tayari kuwapigania hata wengine wajikomboe; hadi kufikia hatua hii ya leo Samia na wajomba zake kuja hapa na kutununua kwa kutumia takataka kama hizi?

Ni akina nani hasa wamelengwa kupewa 'package' kama hizo, na wao wanategemewa kuwasilisha nini kwa Samia? Viongozi wa Mashina na mitaa, ili wawaweke sawa watu walio kwenye maeneo yao?

Hawa viongozi wanao uwezo wa kuwaswaga watu na kuwasalimisha kwa Samia na Genge lake?

Samia Suluhu Hassan hayupo sawa kichwani, na hao washauri wake na Genge lote ni watu wasiokuwa na upeo wa kutosha wa kuwadanganya waTanzania.
Samiah anapenda sana watu wavivu
 
Back
Top Bottom