GE2025 Angalizo Kabla ya Shari: Masaa 48 Kabla ya Uamuzi wa Uchaguzi au Maandamano

GE2025 Angalizo Kabla ya Shari: Masaa 48 Kabla ya Uamuzi wa Uchaguzi au Maandamano

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kama Mtanzania huwezi kuandamana basi ni kheri usipige kura.

Kupiga kura ni kubariki waliotekwa wamalizwe huko walipo. Kupiga kura ni kubariki mwanao atekwe.

Sio lazima uingie barabarani angalau tulia nyumbani ila usiwe sehemu ya kuhalalisha USHETANI.
Kwani usipo piga kura utasaidia nini??,wakijitokeza 200 tutaandika 20M.
 
Kwenye hiyo idadi ya vifo na Mangekimambi, Maria Sarungi nao waje wawe miongoni mwa watu watakao kufa kwenye maandamano
 
Haya yanhesbabisha maandamano wakati yametokea na kulazimisha watawala wazungumze. Labda kama itafanikiwa Jumatano kudai haya basi maridhiano yanaweza kutokea..nje ya hapo...
 
20251027_183623.jpg
 
Kama Mtanzania huwezi kuandamana basi ni kheri usipige kura.

Kupiga kura ni kubariki waliotekwa wamalizwe huko walipo. Kupiga kura ni kubariki mwanao atekwe.

Sio lazima uingie barabarani angalau tulia nyumbani ila usiwe sehemu ya kuhalalisha USHETANI.
Kuongezea; hata kama itakulazimu kufika kituoni kupiga kura hasa ukiwa kada basi haribu kura, ujumbe ufike.
Hii ni kwa wale makada waandamizi kama mawaziri n.k ambao wasipofika kituoni wakapigwa na picha, watajulikana hawakushoriki uchafuzi
 
Tumefikishwa kwenye gambling. Kulikuwa na umuhimu gani wa kufika huku? NRNE kwa nini ni mwiba kwa awaye yote? Wanayo kesi nzito ya kujibu!

Wengi wameumizwa na watazidi wengine kuumizwa
Mwisho wa dhambi ni mauti
 
Mkuu tutarudi hapa tena. Mimi nakuhakikishia kuwa maandamano hayatokuwapo. Unachokiona kwenye mitandao ya Jamii (Twitter, Instagram, FB na Tiktok) hizo ni kama challenge tu za nani ana maneno makali kuhusu "maandamano". Wanarekodi ma ku post sawa na wanavyojirekodi nyimbo za wasanii
Mzee Mwanakijiji. Nilikuambiaje?? Je huko kuliko kuna maandamano? Hebu yaweke hapa tafadhali
 
Na. M .M. Mwanakijiji

Kuna kitu kinaitwa "best case scenario na worst case scenario". Kutegemea unayemuuliza kuelekea keshokutwa mitazamo inaweza kutofautiana.

Kwa uapnde wa serikali best case scenario ni kuwa uchaguzi utafanyika kwa amani, hakuna maandamano na Rais Samia atachaguliwa na nchi itaendelea kwenye utulivu kuelekea kuapishwa kwake na kuandika historia.

Kwa upande wa worst case scenario ni kuwa siku inafika na mara maandamano yanaanza kwanza kidogo kidogo na mara makundi ya vijana katika majiji na miji mikubwa wanaanza kuzuia upigaji kura hadi uchaguzi unavurugika.

Katika hili jeshi la polisi linaingia kudhibiti waandamanaji lakini kwa zaidi ya masaa 24 hali haijatulia. Taarifa za watu kuuawa na video za mauaji hayo zinaanza kusambaa na kusababisha vurugu zaidi. Mwisho wa siku IGP na wakuu wa wengine wanalazimishwa kujiuzulu na nchi au sehemu ya nchi inawekwa kwenye hali ya hatari.

Kutangazwa kwa hali ya hatari kuna lazimisha JWTZ kuitwa kusaidia kutuliza nchi. Hii italeta jambo baya zaidi kuweza kutokea..Jeshi kuchukua nchi. This is the worst case scenario. Binafsi sioni uwezekano wa hatua hizi mbili za mwisho kufikiwa unless polisi watumie nguvu zaidi kudhibiti waandamanaji kuliko inavyohitajika na hivyo wachochee wenyewe kuiangusha serikali.

Kwa Waandamanaji, kwa kweli the best case scenario ni kufanikiwa kwa maandamano. Kwamba vijana wengi wajitokeze, waingilie upigaji kura na kusababisha uchaguzi mkuu uvurugike na kumlazimisha Rais Samia ama kukaa chini na kusikiliza malalamiko yao au wamlazimishe aamue kuachia madaraka na kukimbia nchi kama yaliyomkuta Rais wa Madagascar siku chache zilizopita.

Katika best case scenario hii, waandamanaji wanalazimisha kuachiliwa kwa Tundu Lissu, Heche, Polepole na wengine kama mojawapo ya masharti ya vijana kutulia. Katika hili mabadiliko yanakubaliwa katika muda uliowekwa ikiwemo kurudiwa kwa uchaguzi katika mazingira bora ya kisiasa na kisheria. Hivyo best case scenario kwa hawa ni kwa kifupi kufanikiwa kwa NO REFORMS NO ELECTIONS.

Kwa upande wa worst case scenario kwa waandamanaji ni kuwa pamoja na promotion yote iloyofanyika kwenye mitandao ya kijamii kufika October 29 hakuna maandamano yoyote ya maana. Wachache watakaojaribu watadhibitiwa kwa haraka na hivyo uchaguzi ukaenda kufanyika katika hali ya utulivu bila fyoko yoyote toka kwa yeyote.

Lakini baya zaidi ni kuwa endapo maandamano haya hayatafanyika au yakafanyika na kuzimwa kabla chai haijapoa ina maana harakati za mabadiliko kwa njia ya mkato hazina nafasi jwa Watanzania. Kama mtu mmoja alivyosema kama siyo sasa basi "never". Tundu Lissu na wenzake wataozea jela, na wale waliotoweka ndio watapotea milele.

Kwa maneno mengine kutokufanikiwa kwa maandamano kutaipa CCM mamlaka(mandate) kubwa na kiburi kuwa haiwezi kuondolewa kwa mbinde wala upinde. Kwamba njia ya mkato ya kuitoa CCM madarakani haijapatikana na kuwa jeshi letu bado halijaweza kuingizwa kwenye kuingilia siasa kama baadhi wanavyoombea.

Baya zaidi ni kuwa kutokufanikiwa kwa maandamano kutaleta kisasi ambacho hatujawahi kukiona isipokuwa kama Rais Samia mwenyewe ataamua kusamehe. Hili historia inasubiria.

Vyovyote vile ilivyo masaa 48 yajayo yataamua mbele ya dunia Tanzania inaenda wapi na kwa vipi kuanzia tarehe 30 Oktoba. Kama walivyosema wahenga..tutaamua kusuka au kunyoa. Ila kuamua tutaamua tu..na kama hatutaamua nako ni kuamua kutokuamua.
You said...
 
Back
Top Bottom