GE2025 Angalizo Kabla ya Shari: Masaa 48 Kabla ya Uamuzi wa Uchaguzi au Maandamano

GE2025 Angalizo Kabla ya Shari: Masaa 48 Kabla ya Uamuzi wa Uchaguzi au Maandamano

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kuna scenario moja tu, nayo ni kwamba maandamano hayatafanyika na kura tutapiga kwa amani japo turn out itakuwa ndogo.

Hili limekwisha, tuangalie tunavuka vipi 2030.

..Maandamano kiduuchu.

..Na wapiga kura kiduuchu.

..Katika mazingira hayo watakaotangazwa watakuwa ni watu wasioungwa mkono.

..Je, hatutarudi kwenye mduara uleule wa harakati, hofu, kutekana, na kupotezana?
 
Maandiko yako yameshapitwa ma wakati. Staafu tu.

Maandamano hayatakuwepo, kwasababu wabongo wengi wana akili kama zako.

KUSIKILIZIA mtu fulani afanye, wao wanajiona hawahusiki.

Kila mtu atakaa kwake KUSIKILIZIA kama wewe, kwahiyo maandamnao hayatakuwepo.

Kuelekea 2030 kutakuwa na UTEKAJI JUU YA UTEKAJI, kila mmoja ataokotwa kwa wakati wake.

A nation with NYUMBU DNA.

Scenario nyingine ni Kama ilivyotokea Kenya. Maandamano yanaanzshwabna Gen Z wanauwawa, Kwa hasira maandamano yanachukua sura nyingine vurugu na Bungeni kinavamiwa, linachomwa. Hatimaye zinakoma Hali kuwa vifo na uharibifu mkubwa wa mali imetokea. Cha ajabu Rais unayetegemea atajiuzuru anaendelea kudunda na nchi inarudu Kama kawaida😩😩
This is the worst case kwa namna nyingi tu...lakini unaona Ruto alivyodhoofishwa...
 
Kama watu hawatatoka kabisa au mwitikio ukawa mdogo .... ni kweli kabisa hawa CCM watajimilikisha nchi rasmi na kuanzia siku hiyo watafanya lolote na chochote kama wanavyopenda.
Sidhani. Kwa mazingira yoyote yale reforms zitakuwepo ila sio reforms mnazotaka nyie Chadema bali reforms za kukidhi matakwa ya watanzania.
 
Sidhani kama number zinazingatiwa hapa kitendo cha watu kwenda kutimiza wajibu wao kikatiba Hata wakiwa wachache namna gani kwa nyakati hizi inatosha... !

..namba hazizingatiwi ktk kumtangaza aliyeshinda.

..lakini namba zina umuhimu katika namna watakavyoongoza baada ya kutangazwa.

..namba zingekuwa hazina umuhimu kabisa, usingewasikia wakiweka msisitizo na kubembeleza watu wakawapigie kura.

..umeona wapi ilani ikasahauliwa na focus ikawa kuswaga watu kwenda vituo vya kura watake, wasitake?
 
29 ,Waandamani Muwe wa moja UMOJA ndio maana Kwenye Askari Nembo zao Zimeandikwa umoja . Msitoke kama kuku jikusanye muwe wengi . Beba silaha kujihami Kuwa Shujaa Kataa uovu back up ipo kubwa hawa watu 28 ,30 ni wachache sana ndio maana hawajiamini wanauza UOGA
 
Mkuu tutarudi hapa tena. Mimi nakuhakikishia kuwa maandamano hayatokuwapo. Unachokiona kwenye mitandao ya Jamii (Twitter, Instagram, FB na Tiktok) hizo ni kama challenge tu za nani ana maneno makali kuhusu "maandamano". Wanarekodi ma ku post sawa na wanavyojirekodi nyimbo za wasanii
Naunga mkono hoja, hakuna maandamano yoyote, October 29 ni kazi moja tuu, kupiga kura kuwachagua viongozi tunao wataka
P
 
Sidhani kama number zinazingatiwa hapa kitendo cha watu kwenda kutimiza wajibu wao kikatiba Hata wakiwa wachache namna gani kwa nyakati hizi inatosha... !
Kama idadi ya wapiga kura itakuwa chini sana kuliko miaka mingine basi ujumbe mwingine utakuwa umetumwa kuhusiana na uhalali wa aliyechaguliwa. Of course hakuna threshold iliyowekwa wa wapiga kura wanaofanya uchaguzi uwe halali as long as anayechaguliwa amepata kura nyingi zaidi (50%+1)
 
Best case scenario
1. Maandamano kufanikiwa.
2. Vituo vya kupigia kura kuchomwa moto
3. Utawala dhalimu wa ⌚️100 kuangushwa
4. Watesi wote kuuwawa
5. Tanzania kuwa taifa huru.

Worst case scenario
⌚️100 kurudi madarakani hadi 2030, that's the worst case scenario.
 
Kama idadi ya wapiga kura itakuwa chini sana kuliko miaka mingine basi ujumbe mwingine utakuwa umetumwa kuhusiana na uhalali wa aliyechaguliwa. Of course hakuna threshold iliyowekwa wa wapiga kura wanaofanya uchaguzi uwe halali as long as anayechaguliwa amepata kura nyingi zaidi (50%+1)
Mshindi wa uchaguzi wetu ni by a simple majority, hata kama wapiga kura ni million 30, kisha wakajitokeza wapiga kura watatu tuu, mgombea mmoja akapata kura 2, mwingine kura moja, yule mwenye kura moja, ni mshindi halali kisheria ila bila kuwa na legitimacy, yaani legally right but without legitimacy.

Ila kwa Tanzania, Usipopiga, then utapigiwa, ballot papers zote zitapigwa na atapigiwa na tutaionyesha dunia jinsi anavyopendwa na anavyo kubalika, Thread 'Kuna Vitu Ili Maisha Yaende, Lazima Upige!, Usipopiga, Utapigiwa! na Maisha Yataendelea!. Sasa Kati ya Kupiga na Kupigiwa, Bora Kipi? Nakushauri Piga!' Kuna Vitu Ili Maisha Yaende, Lazima Upige!, Usipopiga, Utapigiwa! na Maisha Yataendelea!. Sasa Kati ya Kupiga na Kupigiwa, Bora Kipi? Nakushauri Piga!

Tena juzi kati nilikuwa huko, hata diaspora wetu wanamkubali sana! Thread 'Usichojua Kuhusu Diaspora wa Tanzania, Wanamkubali Sana Samia, Wangekuwa Wanapiga Kura Kama Diaspora wa Wenzetu, Samia Angevuna Kura Nyingi za Kutosha' Usichojua Kuhusu Diaspora wa Tanzania, Wanamkubali Sana Samia, Wangekuwa Wanapiga Kura Kama Diaspora wa Wenzetu, Samia Angevuna Kura Nyingi za Kutosha

P
 
..Maandamano kiduuchu.

..Na wapiga kura kiduuchu.

..Katika mazingira hayo watakaotangazwa watakuwa ni watu wasioungwa mkono.

..Je, hatutarudi kwenye mduara uleule wa harakati, hofu, kutekana, na kupotezana?
Hapo sasa italazimu tukae chini kwa ajili ya maridhiano
 
Historia ya darasani,na katika vitabu vya dini inaonesha kua kila mateso,unyanyasaji yalipozidi kwa tabaka la chini,watu walinyanyuka na kudai haki zao..

Kutoka 3:7-10 “I have seen the misery of my people… I have come down to rescue them.”

French Revolution (1789–1799) ilianza kama hivi,watawala mara zote wanafikiri kua kila ukizidi kukandamiza tabaka la chini,ndio wanazidi kua waoga,lakini history haioneshi hivyo,wanazidi kujaza watu Chuki,ujasiri,Na Uasi dhidi ya mamlaka(Nicola Machiavelli)..

Hata kama sio tarehe 29,ila Hawa wahuni siku zao zimefika mwisho..
 
Hapo sasa italazimu tukae chini kwa ajili ya maridhiano

..Maridhiano ni baina ya pande zinazohasimiana, zilizokosana,au zilizoumizana.

..Sasa madai ya Ccm dhidi wapinzani yatakuwa ni nini?

..Kwa mfano, Ccm wamekosewa nini na wapinzani?

..Nina wasiwasi huenda kukawa hakuna hicho kinachoitwa maridhiano.
 
Maridhiano hutokea baada ya mapigano na michafuano...ndiyo yaliyotokea Zanzibar wakati ule na hivi karibuni huko Kenya. Kama hakuna maandamano yenye kutikisa nchi hakutakuwa na maridhiano.
 
Maridhiano hutokea baada ya mapigano na michafuano...ndiyo yaliyotokea Zanzibar wakati ule na hivi karibuni huko Kenya. Kama hakuna maandamano yenye kutikisa nchi hakutakuwa na maridhiano.

..sasa suala la wanaharakati, na wapinzani, waliotekwa, kuteswa, na kupotezwa, litatatuliwa, au kufungwa, namna gani? Je, litaachwa tu kama jeraha lililo wazi?
 
Back
Top Bottom