DOKEZO Angalizo: Utapeli na wizi kwenye maduka ya Pharmacy/ biashara ya dawa za binadamu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mkuu usilaumu sana inawezekana angechoma hiyo sindano na angekata moto pia.
 
Mimi ilinikuta hospital kabisa dogo amepimwa amekutwa na PID nikaandikiwa dawa bei 93k sema siku na cash nkawaambia waniwekee kabisa dawa naenda ku draw ATM maana sinaga sim banking.

Nikawa nataka kutoka na cheti doctor akakomaa hichi huwez chukua unakiacha hapa hapa kuona vile chap nkakipiga picha fasta nkatoka na dogo mpaka ATM.

Sasa wakati narud nkasema heb ngoja nkaulizie hizi dawa pale amana kuna doctor mmoja wa muhas anaduka lake pale.

Kilichotokea kilibadilisha maamuzi yangu yote kwani mpaka leo napima hospital dawa na majibu naenda somewa pale na dawa pale.

Nmefika pale dawa zile zile dozi kamili nmepata kwa 22k tu.dah nili mind kinoma toka siku hyo manesi niliwawekaga kundi la pili la watu wasio na huruma
 
Dah!!
Pole sana ndugu........hawa wasiotaka mtu kuondoka na cheti ndio wezi namba moja......
 
Kufika kule (huko kwenye hilo duka kubwa maarufu)

"duka kubwa maarufu" ndio jina la hilo duka au?, na kama sio, uoni kuwa na ww ni sehemu ya tatizo kwa kutotaja jina halisi la hilo duka kwa manufaa ya wanajukwaa hapa ili na wao walijue?
 
Mi juzi nimeuliza mtaani Azuma paketi moja elfu sita,nikaenda duka moja kubwa azuma paketi tatu elfu tisa, sawa na elfu tatu kwa paketi,


Me binafsi ndio kawaida yangu dawa lazima nilinganishe maduka hata matatu,maana mi bahili sana
 
Kufika kule (huko kwenye hilo duka kubwa maarufu)

"duka kubwa maarufu" ndio jina la hilo duka au?, na kama sio, uoni kuwa na ww ni sehemu ya tatizo kwa kutotaja jina halisi la hilo duka kwa manufaa ya wanajukwaa hapa ili na wao walijue?
Nilishalitaja lakini mwanzo nilisita kutaja kwa kuwa nilidhani nitafikiriwa kama natangaza biashara si unajua hii ni sehemu ya watu.......na matangazo ni moja ya biashara yao kama unavyoona......

Lakini kuna mdau nilimtajia.......FARU PHARMACY ndipo nilinunua kwa bei chee.....

NB;
Mniwie radhi moderaters kama Kwa kutaja jina moja kwa moja nitakuwa nimevunja au kukinzana na utaratibu wa hapa jukwaani
 
Hii ni kweli kabisa na mimi nilikua namuuguza mzee wangu, bahati mbaya amesha fariki mungu amrehemu. Basi kipindi cha uhai alikua anahudhuria clinic ya mifupa pale kcmc kila mwezi, niliandikiwa dawa zinauza 150,000 kwenye kichupa ni dawa za kutumia mwezi mzima mara ya kwanzanilinunua, mwezi unaofuata sikuwa na pesa ya kutosha dawa nikaamua kuzunguka kwenye farmacy kubwa pale moshi mjini, karibu na police moshi mjini barabara ya kunjooka kuelekea kilimani mawenzi kuna duka niliingia nikawapa kile cheti cha dawa lakn pia nilikua na kile kichupa alicho maliza dawa, Yule muuzaji akaniletea vichupa 3 akasema dawa ni moja ila kampuni tofauti, nikachangua kama ile ya mwanzo aliyomaliza mgojwa, nashangaa ananiambia 46,700 nikahisi amekosea au sijasikia vzr, nikauliza tena bei akasema haipungui kaka ni sh 46,700 akijua kwamba nataka punguzo, nilishangaa mpaka dada mwingine aliyepo kwenye computer akawa ananiangalia tu. Jamani maduka ya dawa mumezidi kutuumiza kutoka 47,700 mpaka 150,000 kisa dawa ni mzuri. na risit ya efd nilipewa.

Sent from my SM-A235F using JamiiForums mobile app
 
Watu tulipigwa na mshangao asee, Baada ya vipimo na kupewa karatsi ya dawa tukanunue kulikuwa na watoa huduma wawili kwenye hiyo pharmacy kuna mmoja anamwambia mwenzake akijua hatusikii, "matilda niachie basi na mimi nipige kidogo nipate ya weekend niachie wale wanne wa mwisho" πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Naamni tulipigwa wote pale wahitaji huduma ya dawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…