Angela Kairuki amuwakilisha Dkt. Mpango kwenye mkutano wa TAWIRI

Mtu mpaka amekuwa kiongozi wa Kitaifa maana yake ni kwamba ana watu special wa kumsaidia majukumu.

Kwa hiyo hakuna haja ya kulazimisha kujua kila kitu. Tuliaaa
 
Shem tuombe. Sijui familia yake ina hali gani!
Wana hali nzuri kabisa, wataendelea kula mafao maisha yao yote. Changamoto ni kwetu sisi pangu pakavu, mzee wa kaya akitangulia, nyuma ni majanga matupu, familia nyingi upoteza kabisa mwelekeo haswa watoto.
 
Wana hali nzuri kabisa, wataendelea kula mafao maisha yao yote. Changamoto ni kwetu sisi pangu pakavu, mzee wa kaya akitangulia, nyuma ni majanga matupu, familia nyingi upoteza kabisa mwelekeo haswa watoto.
Sijamaanisha hayo boss
 
PM angesema tu Makamu ..... ameenda nje ya nchi kucheki afya yake. ingetosha kabisa kauli ya kidiplomasia na kiutu mzima.
Say whaaat? Hiyo kauli hawawezi kuitumia, ingekuwa ya hovyo na tungeilaani.

Ameenda kuchekiwa afya yake nje ya nchi kwa kodi zetu wakati sisi tunaumwa kama mbwa na hatuna access ya hizo tiba na ni yeye ndio ana dhamana ya kuleta hizo huduma?
??

Wananchi wanaokubali maelezo kama hayo mko wachache, wengi wetu sio mazuzu ndio maana hawawezi kuja na kauli ya kishenzi na kinyama kama hiyo unayopendekeza.
 
Mhhhhh nilikuwa napuuzia, now this is serious!
Lakini kuna sababu zipi hasa za hili jambo kuwa siri kubwa?

Dr Philip Mpango ni mmoja wa viongozi ninao wapa heshima kubwa ndani ya CCM na serikalini.
Matumaini yangu ni kwamba kama anaumwa, Mungu atamsaidia apone, na arudi kulitumikia taifa hili. Bado mchango wake unahitajika sana, hasa nyakati hizi.
 
Hivi huu usiri faida yake ni nini? Mkapa alienda kutibiwa mguu, mbona tuliambiwa. Kikwete alienda kutibiwa tezi dume, mbona tuliambiwa. What is wrong na hawa jamaa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…