Angelina Jolie aanza kusumbuliwa na Mama wa mtoto aliyemuasili

Angelina Jolie aanza kusumbuliwa na Mama wa mtoto aliyemuasili

Damu inausikaje mkuu. Adoption ni mkataba. kama kipindi anakuadopted sehemu ya mazazi ilijanzwa amekufa. How comes awe amefufuka?
Kuna kitu kinakua katika makaratasi na kuna kitu kipo katika damu. Kimakaratasi ni mtoto wa Angelina. Lakini kidamu ni mtoto wa muethiopia hata aende wapi. DNA ndiyo kitu cha maana katika uhai wa binadamu.

Piga ua kuna siku akiwa na uwezo huyu mtoto, atamkumbuka biological mother wake pia. Naandika nafuta, ngoja niishie hapa. Mifano ninayo mimi mingi ya damu
 
Mimi mwenyewe nina mpango wa kuasili yatima kabisa. Ninaishi na watoto wa ndugu zangu na wengine wako chuo ila wana baba zao na mama zao, wakishafika malengo yao wanarudi kwa wazazi.
Tatizo sio kuasili . Tatizo linakuja wewe umeasili ili kuwa ondolea madhila hao ulio waasili kipindi ambacho hawajimudu wao kwa utoto wao na wazazi wao au walezi wao kwa kuwa na hali duni zaidi au hatarishi zaidi Sasa kabla malengo hayatimia jitu lina kuja na swaga zake za ama kukukatisha tamaa wewe au mtoto uliye muasili
 
Tujiulize je huyu Zahara angekuwa bado Yatima huyu bi mkubwa angeenda kuomba kuongea naye!? Afrika daah
Naona nyote mnafunga akili zenu. Twende taratibu. Huoni kitendo cha kumtoa mtoto wake akaasiliwe kilikuwa cha kumtakia mema mtoto wake? Si ajabu kama angalimg'ang'ania angelikufa kutokana na umaskini? Nyie vipi!
 
Kuna kitu kinakua katika makaratasi
bila makaratasi hakuna atakae kuamini. Mfano wewe unawatoto wako afu baada ya wao kukua wabadilishe jina lako kwenye vyeti (makaratasi) na lisomeke jina jengine.

Unadhani sisi tutaminivipi kuwa awo ni watoto wako ikiwa kwenye nyaraka muhimu hutambuliki na kipindi unapizi hatukuwepo.
 
bila makaratasi hakuna atakae kuamini. Mfano wewe unawatoto wako afu baada ya wao kukua wabadilishe jina lako kwenye vyeti (makaratasi) na lisomeke jina jengine.

Unadhani sisi tutaminivipi kuwa awo ni watoto wako ikiwa kwenye nyaraka muhimu hutambuliki na kipindi unapizi hatukuwepo.
Biological mother amewin hii game. Maana alitaka mtoto ajue kuna biological mother wake. Leo atamkataa ila akikua na kuanza kujitegemea utaona atakavyomnyanyua
 
Sheria haitambui hisia
Inaonesha bado wewe una akili za kitoto. Ubinadamu ni tofauti na makaratasi. Mtoto kimakaratasi ataitwa wa Angelina ila yeye atajua nilipita katika K ya muethiopia. Kitendo cha kukaa naye tumboni kwa miezi 9 ni cha muhimu maana kama asingetaka angeaboti. Ujue. Damu nzito kuliko maji bwashee
 
Mtoto kama ana maokoto amsaidie tu mama yake japo kuna uongo ulifanywa na kituo kilichokuwa kinamlea kwa angelina, na sidhani kama angelina atamkataza mtoto kumsaidia biological mother wake au kuwasiliana naye, japo kiukweli mtoto kwa sasa ni wa angelina.

Angalizo, huyo mama asije tu akaanza zile tamaa za kiafrica kumtaka mtoto kisa kaona anaweza kuponeapo


Ila mtoto kawa pisi aisee
Anaweza akamrudishia gharama alizomlelea kweli both emotions, monetary,time, mentally kweli
 
Mkuu kwa wabongo tunafanya au tuliwahi fanya hiyo mambo lakini kwakweli wabongo ni tatizo.
Mimi niliwahi kuasili watoto 3 wawili walikuwa ndugu na mmoja ni wa familia nyingine
Tatizo lilikuja pale wale wawili walipo fika chuo kikuu wana boom akijitokeza mtu kuwa ni mzazi wao na mambo kibaaao!
Nilipata usumbufu wa kila aina ikabidi niache watoto waamue kwasababu tayari ni wakubwa.

Akabaki 1 ambae sasa yupo kidato 4 huyu nae mlezi wake akaanza longolongo kwakuwa sipendi vyesi nikamburuza Ustawi wa jamii kwasababu sikumchukua mtoto kienyeji. Akasalim amri amuache mtoto asome Mtoto ataamua pa kwenda akifikisha miaka 18.

Kuasili watoto wa watu wasiojielewa ni mtihani.
Ukitaka kuasili nenda kaasili kutoka vituo vya watoto yatima tofauti na hapo fanya shughuli nyingine za kusaidia wasiojiweza. Lakini usiali mtoto mwenye wazazi hatakama hajiwezi kupindukia.
😍😍😍 Uko wapi uniadopt mkuu, hakuna wa kukusumbua ilo nakuhakikishia
 
Back
Top Bottom