Anguko la Diamond Platinumz kimziki

Anguko la Diamond Platinumz kimziki

Mmm kweli sio leo, ila kama kwa sasa anaimba vilevile alivyoimba jana

Ubunifu umepungua sana kwa Mr. Domo
Hujamsoma theki hapo juu?
hata chriss brown sio nyimbo zote anazotoa zinabamba
 
Nimesikiliza Ngoma aliyomshirikisha Inyaya wa Nigeria pia sio mkali kiviile.Lakini pia sio nyimbo zote anazotoa chriss brown huwa zina bamba.

Mkuu embu tupia link ya hiyo ngoma maana nime google bila mafanikio
 
Kusema ukweli huo wimbo wa mdogo mdogo uta hit kwasababu tu mwimbaji ni diamond ila there is nothing special on it..
Muda wa kusikiliza huo kitorondo ni bora nisikilize Ndege mtini ya ferooz..

Na kwanini mnavoleta mada za diamond mnamuhusisha na Ally k.?
 
Binafsi Kitorondo Naupenda Vibaya sana kuliko hata hiyo Number one ,Yaani Umenibamba kinoma Kijana yupo Juu lazima Utafute soko kwa Watu wa Aina zote ,Wa Nje ya Mipaka , Wa Masaki , Na sisi Wa Mwananyamala + Mtogole hiyo ndio Biashara , Vannesa Mwenyewe Kashituka katoa wimbo wa Mipasho sasa hata sisi wa Mwananyamala Tunamsikiliza ...Diamond Mungu akuzidishie Uzidi Kusimama Imara Mtoto wa Bi Sandraaa
 
Hii picha anaonekana kajengeka juu (sehemu ya kifua na tumbo) chini njiti (vimiguu vyembambaaaaaaa) awafate wataalam wa mazoezi wamuelekeze.
 
hahahaaaaa... man, unachekesha sana.. rudia utafiti wako na uusapoti na michoro kabisaaa.. ndo uulete hapa.
 
No hard feelings ila huu wimbo wake mpya ni wa kawaida sana ingawa utapata air time cuz jamaa ni anajua promo naamini video itakuja kuibeba hii ngoma ila kwa malengo ya kuipeleka kimataifa ngumu.
Ila nimependa kaenda USA kimyakimya bila mbwembwe wala upuuzi wa team nani na nani kwenye BET naamini ameanza kujitambua zaidi.
 
Kuna watu wana bahati tu kwenye maisha lakini sio wana vipaji sana, unaweza kuta mtu kichwa kimetulia sana lakini hatoki kimaisha.

Namkubali sana T.I.D ila unga na promo Hana ukweli Ana kipaji hata sauti yake imetulia sana.
 
Wakuu sishabikii ,ila I predict nyimbo zote zinazokuja za Diamond Platnumz hazitahit tena,Katoa wimbo unaitwa Kitorondo,nimesikiliza but kaimba rubbish ukifananisha na ''My number one''count one me hakutakuwa na wimbo mzuri na utakao mjulisha Diamond kimataifa kama ''My number one remix"now atafunikwa hata na wasanii wa kawaida wa hapa bongo.NB:ASIMDHARAU ALIKIBA WOTE WANAFANANA TU
Kaunginishe nguvu na Ustaadh Abdallah labda hivi sasa dua zenu zinaweza kutimia manake mwenzako alikuja na dua kama hizi miaka miwili iliyopita lakini badala ya kushuka, ndo kwanza akapanda!!
 
Hivi ule wimbo walio urekodi na Mafiki Zolo umeshatoka??? Vp ulishausikia uka judge tayari..
 
Watanzania hapana wanadamu kuna ambao hawapendi kuona flani akiwa pale.Ila lazima heaters wawepo ili watu wafanikiwe,ukiona watu hawapondi unachofanya hata kama ni kizuri jua something is wrong.

Haters will become believers tu.
 
Binafsi Kitorondo Naupenda Vibaya sana kuliko hata hiyo Number one ,Yaani Umenibamba kinoma Kijana yupo Juu lazima Utafute soko kwa Watu wa Aina zote ,Wa Nje ya Mipaka , Wa Masaki , Na sisi Wa Mwananyamala + Mtogole hiyo ndio Biashara , Vannesa Mwenyewe Kashituka katoa wimbo wa Mipasho sasa hata sisi wa Mwananyamala Tunamsikiliza ...Diamond Mungu akuzidishie Uzidi Kusimama Imara Mtoto wa Bi Sandraaa

Hahaaa Shaa mwenyewe Mbezi kumemshinda kakimbilia manzese... bongo hakuna uzungu show zenyewe wanajaza watu wa manzese.. buguruni.. mwananyamala na Tandale
 
Hahaaa umeona eeh
Ndio maana Pokello anapenda slogan yake "haters will become believers"

Anataka kila songi la Diamond limbambe
wakati kila mtu anabambwa na anachokiona bora kwake
kuna songi mi zinankera hadi kesho Rita,busu la pink na bembeleza za marlow ila kuna watu zinawakuna mbaya
 
Back
Top Bottom