Anguko la Ndugai: Somo la Katiba, viongozi na nchi

Embu lete ushahidi ni wapi nimesema Kauli ya Magufuli haijaathiri chochote.

Nimekuambia Vitendo vyake vimesahihisha kauli yake. Sio vile unavyodai wewe.

Mbona nimekubaliana nawe kwa wazi kabisa kuwa Wavivu wa Kufikiri na Waliojaa Fikra Potofu na wenye Upeo mdogo wameitafsiri vibaya kauli hiyo.

Ushaanza kulisha watu maneno.

Kama ni Kasi basi ndio Ukuu wake huu. Lakini hatupo kusema nani ni bora zaidi ya mwingine. Mimi nasemea Ukuu wa Magufuli. Hope Ukarabati wa reli ya Kaskazini ulianza na Mkapa.
 
Nimekuambia Vitendo vyake vimesahihisha kauli yake. Sio vile unavyodai wewe.
Ndio maana nakuuliza vitendo gani vimesahihisha kauli yake?
Hakuanzisha miradi kama ulivyosema! hukuonyesha. Alichofanya ni kudandia miradi ya JK
Na mradi mwingine atakokumbukwa nao na watu wa kaskazini ni '' kuwahimiza waache kujiletea maendeleo wakisubiri wengine'' chuki iliyokithiri
Kama ni Kasi basi ndio Ukuu wake huu.
Kasi yenyewe ilikuwa na tija? Kwa mfano kufunga biashara za watu kwa kasi tunaweza sema ni jambo jema? Kuua Bank (Mwigulu) kwa kasi ilikuwa jambo jema? Kasi inaweza kuwa pande zote
Lakini hatupo kusema nani ni bora zaidi ya mwingine.
Ahaa sasa mnajirudi, si mlisema amefanya mengi makubwa kuliko Watangulizi wake
Tumewaonyesha kwamba hakuna jipya alilofanya, hakujenga hata sentimita moja ya reli
Hope Ukarabati wa reli ya Kaskazini ulianza na Mkapa.
Ukarabati wa reli ya kaskazini ilikuwa ni seheu ile ile ya kufunika kombe kwa aibu.
Reli ilitakiwa iwe SGR kwa umuhimu wake kiuchumi kama ya kati.
Wakati wa Nyerere ilikuwa inafanya kazi 24/7 .

Tunachokubaliana na ambacho si mjadala tena ni haya
1. JPM hakufanya kitu tofauti na watangulizi wake
2. Hakuwahi kujenga kitu chochote na mfano ni reli. Hakujenga hata sentimita moja ya reli
 
Kipi sasa ambacho utasema si kufunika Kombe?

Umeshapita walau Wami hivi karibuni?

Hivi kweli unataka tushindane juu ya Magufuli Kujenga reli?

Ni wewe uliyesema alitekekeza kwa kasi kubwa. Kama hiyo kasi ni ya kufunga biashara, basi aliwazidi wenzake kasi tu ila wamezifunga wote.

USIPOKIRI HADHARANI, MANENO YAKO YATAKUUMBUA.
 
Ame na a4afrika hamisheni bandiko#25 lenu katika uzi husika tafadhali.

Ahsante
Je, una uhakika wowote juu ya chanzo cha kutokea kwa Corona Virus?

Je, umeshawahi sikia uwepo wa virus vilivyotengenezwa maabara?
 
2. Hakuwahi kujenga kitu chochote na mfano ni reli. Hakujenga hata sentimita moja ya reli
Umesahau kidogo, alijenga kitu kimoja tu... Chato International Airport. Ni hill tu kwa miaka yake yote 6 madarakani.

Sasa utuambie, tunavyoviona vikikuwa vimejengwa na nani? Mfano ni hiyo reli.
 
Kipi sasa ambacho utasema si kufunika Kombe?
Umeshapita walau Wami hivi karibuni?
Daraja la Wami limejengwa na Nyerere. Ni Mwalimu Nyerere aliyejenga barabara ya Segera-Chalinze kuanzia studies, kuvunja pori na kujenga barabara ikiwemo daraja la Wami
Daraja la Wami halikuwepo kabla ya Uhuru

Nyerere alijenga Barabara na daraja likiwemo.
Hili linalojengwa sasa lilianza wakati wa Kikwete, alichofanya magufuli ni kuendeleza

Nyerere pia alijenga reli ya Mnyuzi- Ruvu.

Hapa unaleta hoja nyingine, tuonyeshe barabara ialiyojenga magufuli

Hivi kweli unataka tushindane juu ya Magufuli Kujenga reli?
Yes kwasababu watu wasiojua wanasema amejenga SGR! Uongo mkubwa
Nyerere alijenga Tazara ikiwa SGR tayari ndiyo maana tunaweza kusafiri hadi South Africa

Magufuli alikarabati reli katika kiwango cha SGR, hakujenga hata sentimita moja! none, zero

Nyerere alijenga Mnyuzi-Ruvu na Tazara
Mwinyi akajenga 10KM Manyoni

Magufuli hajajenga reli hata sentimita moja, kukarabati si kujenga
Ni wewe uliyesema alitekekeza kwa kasi kubwa. Kama hiyo kasi ni ya kufunga biashara, basi aliwazidi wenzake kasi tu ila wamezifunga wote.
USIPOKIRI HADHARANI, MANENO YAKO YATAKUUMBUA.
Kuna kasi njema na kasi mbovu, hilo halibadilishi maana ya kasi

Magufuli hakujenga hata sentimita moja ya reli, sijui kama kuna barabara ya km1 sina uhakika

Lete mradi mwingine! aliofanya! ambao watangulizi hawakufanya
 
Umesahau kidogo, alijenga kitu kimoja tu... Chato International Airport. Ni hill tu kwa miaka yake yote 6 madarakani.
Yes alijenga Chato! Je, hakukuwepo viwanja kabla yake? Ni vingapi! zaidi ya 20
Hoja ni kueleza kitu ambacho watangulizi wake hawakuwahi kufanya

Tuonyeshe sentimita moja ya SGR aliyejenga JPM! cm moja tu wala si rula, hapana! one centimeter
 
Duuuuuhhhhhh! Umetokea wapi Mkuu?

Basi iwe hivyo usemavyo. Je, huo ukarabati au uendelezwaji kwako si Makuu?

Nilishawahi kukuliza, Je, upo hapa Tz au nje ya nchi?
 
Umesahau kidogo, alijenga kitu kimoja tu... Chato International Airport. Ni hill tu kwa miaka yake yote 6 madarakani.

Sasa utuambie, tunavyoviona vikikuwa vimejengwa na nani? Mfano ni hiyo reli.
Mtazungusha sana

Tunachosema hapa ni kuwa ujenzi na ukarabati ni vitu viwili tofauti.

Tumeshamaliza mjadala kwamba JPM alifanya mengi kuliko Watangulizi wake

Tumeonyesha kuwa hakuna alichokifanya kipya hata kimoja
 
Yes alijenga Chato! Je, hakukuwepo viwanja kabla yake? Ni vingapi! zaidi ya 20
Hoja ni kueleza kitu ambacho watangulizi wake hawakuwahi kufanya

Tuonyeshe sentimita moja ya SGR aliyejenga JPM! cm moja tu wala si rula, hapana! one centimeter
Hiyo hoja ya Kitu ambacho wenzake hawajawahi kufanya Unaitoa wapi? Mbona unatapatapa mno?
 
Yes alijenga Chato! Je, hakukuwepo viwanja kabla yake? Ni vingapi! zaidi ya 20
Hoja ni kueleza kitu ambacho watangulizi wake hawakuwahi kufanya

Tuonyeshe sentimita moja ya SGR aliyejenga JPM! cm moja tu wala si rula, hapana! one centimeter
Usilazimishe hoja za ajabuajabu, hatuwezi kukaa chini kuanza kupeana hoja za namna hiyo. Tutakuwa tunajiabisha tu.
 
Mtazungusha sana

Tunachosema hapa ni kuwa ujenzi na ukarabati ni vitu viwili tofauti.

Tumeshamaliza mjadala kwamba JPM alifanya mengi kuliko Watangulizi wake

Tumeonyesha kuwa hakuna alichokifanya kipya hata kimoja
Nikuridhishe labda, japo hakika ni utoto. Electrified SGR. Je, kuna iliyowahi kuwepo?
 
Je, huo ukarabati au uendelezwaji kwako si Makuu?
Sasa kama huo ni ukuu, je ule Nyerere aliyevunja pori, akajenga barabara na daraja na reli tutaita nini. Ndio maana tunasema msilete ukuu na sifa zisizo na ithbati! umbuko

Hakuna jipya alilofanya JPM ambalo JKN, AH, BWM, JKN hawakufanya ! hakuna!
 
Nikuridhishe labda, japo hakika ni utoto. Electrified SGR. Je, kuna iliyowahi kuwepo?
Mtasumbuka sana kutafuta vishikizo, ukisema electrified tunauliza cm ya reli !
Halafu kuna mengine tunasitiri !

Haya turudi kwenye
Mahusiano ya kitaifa, kikanda na kimataifa
Halafu rekodi ya haki za binadamu

Of course kitaifa yalikuwa na matatizo kama kuwasumanga watu wa kaskazini

Tuendelee na mengine ya kikanda na kimataifa halafu rekodi yake katika demokrasia, haki za binadamu. Utu tulishamaliza na kufunga mjadala! hakukuwepo kitu hicho
 
Sasa kama huo ni ukuu, je ule Nyerere aliyevunja pori, akajenga barabara na daraja na reli tutaita nini. Ndio maana tunasema msilete ukuu na sifa zisizo na ithbati! umbuko

Hakuna jipya alilofanya JPM ambalo JKN, AH, BWM, JKN hawakufanya ! hakuna!
Ndugu umeishiwa mno....

Ni nani amesema watangulizi wa Jpm hawakufanya Makuu yoyote? Nao wana vitabu vyao.

Tunachowashangaa ni nyinyi kukataa na kujaribu kuchafua Ukuu wa Magufuli kwa hoja dhaifu.

Chutama.
 
Mtasumbuka sana kutafuta vishikizo, ukisema electrified tunauliza cm ya reli !
Halafu kuna mengine tunasitiri !
Wewe umesema kama kuna chochote kipya, nami nimekupa hicho. Bado unasumbuka na nini Mkuu?

Sisi Ukuu wa Magufuli haupo kwenye kufanyia Tz jambo jipya.

Ukuu wake upo kwenye vyote, Uendelezwaji, uboreshaji, upangaji na zaidi katika kushiriki nasi katika kuota ndoto ya Kujitegemea, walau tu kwa kuhubiri kwake Ukuu Wetu kama Taifa. Hata Nyerere ana Ukuu huo.

Hayo unayositirivni yako mkuu, sisi hayatuhusu mpaka pale utakapoyaletavhapa. Ni we we uliyedai usizuiwe kumsema marehemu, ajabu unajizuia mwenyewe.
 
Kama determinant yako itakuwa ni Demokrasia na Haki za Binadamu, basi nikuombe ubaki na maono yako. Maana kwa wazi kabisa mimi sio Muumini wa hivyo Viini Macho.
Ila kama ni kwa Misingi ya Utu/Wajibu, basi nilishatolea maelezo yakutosha.

Tafuta hoja nyingine. Au uliza maswali usipoelewa!
 
Ni nani amesema watangulizi wa Jpm hawakufanya Makuu yoyote? Nao wana vitabu vyao.
Soma hapo chini bandiko lako , na rudi bandiko 21 pia
Tunachowashangaa ni nyinyi kukataa na kujaribu kuchafua Ukuu wa Magufuli kwa hoja dhaifu.

Chutama.
Hapana hakuna mtu anayetaka kuchafua ukuu wake. Tunachosema hapa hatukubali ''collective imbecilisation'' tukiambiwa '' Marehemu hasemwi'' wakati huo huo tunahubiriwa uongo wa makubwa aliyofanya ambayo si makubwa ni marudio tu ya kawaida

Mfano ni wewe kueleza kuhusu Wami, wakati hakuna alichofanya zaidi ya kusimamia mradi wa JK
Kutetea kauli yake ya kuwasema watu wa kaskazini wakati ulikuwa ni kauli ya ajabu sana ya Rais wa nchi yoyote kuitoa! orodha inaendelea

Tunataka rekodi ya JPM isiishie flyover ya Tazara, twende kwenye rekodi yake ya haki za binadamu, kujali usalama wa raia, mahusiano ya kitaifa aliyobomoa na leo tunaongelea kanda ya kaskazini, mahusiano ya kimataifa n.k.

Hatuwezi kuficha rekodi katika mwamvuli wa '' Marehemu hasemwi'' halafu tunahubiriwa uongo
6. Urasimi wenu ulitufanya kuwa na Viongozi wa Ajabu huko nyuma, na wakafanya ya ajabu. Ukiukaji wa Magufuli umefanya tushuhudie yaliyo Makuu katika Taifa. Hilo linahalalisha MENGI sana kwake.
Hapa ndipo mjadala ulipo, kwamba, tuonyeshe basi nje ya urasimu Magufuli alifanya nini tofauti?
Hakuna jibu! hamkuweza kuonyesha hata kimoja
 
Yes! hutajadili unajua rekodi ilivyo , tutasikia ''marehemu hasemwi''
Rekodi ya haki za binadamu, utu, demokrasia, mahusiano ya kitaifa, kikanda na kimataifa hayasemwi kwasababu kwa mujibu wako! '' ukiukaji wa hayo umefanya afanye makuu''

Kwamba ni haki kuvunja umoja wa kitaifa ili kufanya maajabu! yapi ! huwezi ku point out!
 
''Hatapeleka maendeleo maeneo waliochagua wapinzani'' wakati anachukua kodi maeneo hayo ni dhulma na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Kutamka wazi ''nikupe gari halafu umtangaze mpinzani'' ni kukiuka misingi ya demokrasia na utawala bora.

Kuzuia wananchi kufanya shughuli 'wasubiri wengine'' kuwagawa wananchi, kupanda chuki, kunyima fursa ya kujiendeleza wakati wakilipa kodi

Utaratibu wa ''plea bargaining '' hauzingatia haki, ulijenga mwanya wa uonevu
CAG kasema hata pesa hazijulikani zilipo

Kuondoa wasio na vyeti ni zoezi halali, kuondoa kwa upendeleo ni kukiuka dhana ya haki

Sheria ya ' money laundering' ilitumika kubambikiza kesi na kuwanyima watuhumiwa dhamana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…