Anna Tibaijuka: Kuchukua umeme kutoka vyanzo mbalimbali nafuu, ni kwa usalama wa Taifa letu

Anna Tibaijuka: Kuchukua umeme kutoka vyanzo mbalimbali nafuu, ni kwa usalama wa Taifa letu

Pakitokea dharura Rufiji basi nchi nzima inaingia gizani. Inaitwa diversification. Kwa hiyo tuombe serikali ije na tangazo rasmi kuelezea kwa utaalamu zaidi jambo hili la kimkakati na mustakabari wa umeme wa ziada utakaozalishwa kama upo.
Sio kweli, kuna Kidatu, kihansi, Pangani, Nyumba ya MUNGU, kuna Mradi wa umeme jua, kuna Yale Majenereta ya Kigoma, Profesa nae kaandika as if Tanzania hatukua na umeme kabla ya Rufiji......kapuyanga
 
Uwekezaji wa transmission line ni wa muuzaji ingawaje ataikomboa kupitia bei itakayokubaliwa. Pili. Siyo sahihi kutegemea chanzo kimoja kwa grid ya taifa.
Huyu nae alee Wajukuu
IMG-20250310-WA0037.jpg
 
Tuliambiwa tule manyasi ili tuchimbe bwawa kuuuubwa kumaliza haja ya umeme nchini na kuuza mwingine nje ya nchi. Mzee Magufuli alidanyanywa na wataalamu wetu?
 
Kwa kiwango fulani nayaelewa mawazo ya Mh. Anna lakini nimeilewa zaidi sentensi ya mwisho
 
Sio kweli, kuna Kidatu, kihansi, Pangani, Nyumba ya MUNGU, kuna Mradi wa umeme jua, kuna Yale Majenereta ya Kigoma, Profesa nae kaandika as if Tanzania hatukua na umeme kabla ya Rufiji......kapuyanga
Mkuu, huoni mbali, kabisa, huko kihansi na kidatu kwa jua hili kuna maji?, Tusolve matatizo ya Taifa kwa ukubwa na upana fulani,sasa nyumba ya mungu Pana umeme gani pale, kumbuka hii ni Tanzania ya VIWANDA NDIO MWENDO WA TAIFA LETU
 
Hausafirishwi moja kwa moja kutoka Ethiopia hadi Tanzania, ila Ethiopia watunga kwenye gridi ya Kenya huku Tanzania ikipokelea Namanga kwa gridi pia. Wataalamu wa mambo watafafanua zaidi.
 
Sawa kabisa, tupe mahitaji yake na sababu za Sisi kushindwa Kufanya kama Ethiopia! Wanatumia hydro powers na wenyewe. Je Vipi kuhusu Ile Mradi wa umeme jua? Hapana, hii hoja bado
 
Hapa ndo unaona aina ya wasomi tulionao uwezo wa kufikiri ni duni

Huo mradi umeletwa kimkakati ili watu fulani wapate chochozo .

Miradi Kama hii ambayo ilikuwa ilikuwa ikiliingiza Taifa Karina hasara ilikuwa ikifanyika kipindi cha mzee Msata.

Kuna mambo yamekaa kiujanja Sana hapo
Kama jambo gani lililokaa kiujanja?tuelimishe nasisi
 
Vipi kuhusu power loss kutoka Ethiopia hadi Tanzania? Maana tunaambiwa kutoka Station kubwa ya Chelinze hadi Kilimanjaro kuna changamoto ya umeme kupotea njiani....

Na kwa nini kipindi hiki? Kuna harufu ya upigaji wala hakuna kingine.
 
Hausafirishwi moja kwa moja kutoka Ethiopia hadi Tanzania, ila Ethiopia watunga kwenye gridi ya Kenya huku Tanzania ikipokelea Namanga kwa gridi pia. Wataalamu wa mambo watafafanua zaidi.
Hausafirishwi Moja Kwa Moja Toka Ethiopia Bali wanatumia bloototh?

Halafu anataka agombee Ili iweje?

HATOGOMBEA!
 
Kwani diversification haiwezi kufanyika kwa vyanzo vya ndani? Such backup plan Kwa nini isiwe kwa mitambo ya gesi au uranium ambazo zinapatikana nchini? Nyie endeleeni tu
 
Hausafirishwi Moja Kwa Moja Toka Ethiopia Bali wanatumia bloototh?

Halafu anataka agombee Ili iweje?

HATOGOMBEA!
Jiwe Alisema Kosea Kuoa/Kuolewa Maana Mtaachana Tu
Ukikosea Kuchagua Rais/Mbunge/Diwani Ujue Mpaka Miaka 5 Iishe
 
Da, siasa nyingi sana hapa. Hivi kabla ya bwawa la nyerere kuanza kuzalisha umeme tulikuwa tunaupata kutoka vyanzo gani?
 
Ameandika prof. Ann tibaijuka katika ukurasa wake wa X:

UMEME KUTOKA ETHIOPIA (km 1500) HADI ARUSHA UNAKUWAJE RAHISI KULIKO WA KUTOKA RUFIJI (Km 650)?

Taarifa hii ilitushangaza na hata kutushtua wengi. Nikaona nijielimishe kwa wahusika Wizarani. Nikaelezwa umeme utanunuliwa kutoka Station ya kusambaza umeme hapo Namanga kupitia Grid ya Kenya.

Uwekezaji wa transmission line ni wa muuzaji ingawaje ataikomboa kupitia bei itakayokubaliwa. Pili. Siyo sahihi kutegemea chanzo kimoja kwa grid ya taifa.

Pakitokea dharura Rufiji basi nchi nzima inaingia gizani. Inaitwa diversification. Kwa hiyo tuombe serikali ije na tangazo rasmi kuelezea kwa utaalamu zaidi jambo hili la kimkakati na mustakabari wa umeme wa ziada utakaozalishwa kama upo.

Uwe wa vyanzo vya maji au gesi au jua kwa ujumla wake. Usalama wa nishati ni usalama wa taifa.

Soma pia: Rais Samia: Tanzania inayo nafasi ya kuuza umeme nje

My Take:
CHADEMA hawawezi kutambua hili, hawaelewi juu ya udharura unaweza kutupata wakati wowote, Akili zetu zote tukizilaza rufiji, na unfortunately ika burst, ndiyo nchi yote iingie gizani?

Yaani hawa chadema akili zao sijui zipoje, hopeless, hawaoni mambo kwa kina na kwa marefu.
-------
Kuhoji jambo ni kutaka kuelewa zaidi kama prof. Anna alivyosema. Ina maana Chadema wana akili kuliko hao wengine wanaokaa kimya kama mabubu.
 
Hivi Ethiopia hawazalishi umeme kwa kutumia maji yanayoanzia ziwa victoria kweli?

Back
Top Bottom