The Monk
Platinum Member
- Oct 12, 2012
- 20,242
- 45,930
===
Mmm! unachosema ni moja ya njia lakini si hiyo pekee.
Wewe ulipoteuliwa, haikutangazwa kwanza. Jina lako likapelekwa katika nchi ulikokuwa unapangwa kupelekwa. Nchi hiyo baada ya kufanya vetting ikatoa green light. Ukatangazwa na kuapishwa. Ukaenda na sasa uko huko.
Kuna wanaotangazwa kuwa wameteuliwa lakini wanakaa muda mrefu mpaka nchi husika ziridhie ndipo mabalozi waende. Hata waambata wanakataliwa kama rekodi zao zina matege.
Huo ndio utaratibu na ndivyo inavyofanyika mkuu. Sijaona haja ya kubishana sana. Nchi husika lazima iridhie kumpokea balozi au muwakilishi wa mashirika kama UN na mengine.