Rais Magufuli kakosea sana kwenye suala la PR kwa kudai COVID-19 haipo nchini.
Huwezi kudai kitu hakipo, hususan ugonjwa unaosababishwa na ki/virusi [ambavyo havionekani], bila ushahidi.
Rais Magufuli ni mwanasayansi wa wapi yeye?
Mimi bado naamini C-19 si kali wala hatari kama inavyotangazwa, lakini hiyo haina maana watu wasichukue tahadhari, hususan wale walio medically fragile.
Si alipima, akaona vipimo ni 'feki', kwa vile mapapai, mafuta ya oil navyo vilikuwa na corona. Akaachana na upimaji. Lakini kabla ya hapo, kuna picha za wafu walioanguka kwa ugonjwa zikionyesha maziko ya usiku..., hiyo ikiwa ni juhudi ya kuonyesha kaugonjwa hakapo, na kama kapo ni kadhaifu mno!
Halafu akaweka "maombi maalum" kwa mungu wake. Hata kama corona ilikuwa imeanza kuonekana kuwa ilikuwepo nchini, 'mungu wake' akaifutilia mbali na akatangaza "Tanzania isiyo na corona.
Baada ya "maombi maalum" kusikilizwa na 'mungu' hatua zote na juhudi muhimu zilizokuwa zimeanza kutumika (ambazo huenda ndizo zilizofifisha maenezi yale ya mwanzo zikatupiliwa mbali. Haya makorokoro ya kujikinga ya nini tena kama 'mungu' amekwishatuondolea corona.
Kampeni zote zikabuma.
Hili wimbi la pili, sio corona yetu hapa. Hii ililetwa na watu kutoka nje na wa hapa kwetu waliokwenda matembezi huko nje. Sisi hapa hatukuwa tumewahi kupata corona.
Hata hivyo, wananchi walishaambiwa waache woga/hofu; kwani woga/hofu ni hatari zaidi ya corona. Uoga hofu itawaua.
Na raia walimwelewa vyema kiongozi wao juu ya woga/hofu hiyo. Wakajiachia kwenye madaladala, mabaa, kule kwa akina machinga na kwenye sehemu zote za mikusanyiko.
Wananchi hawaiogopi corona tena, badala yake woha/hofu yao kubwa ipo kwa kiongozi wao. Kati ya corona na kiongozi, mwananchi ni bora aidharau corona kuliko kukabiliana na kiongozi na mashine zake.
Pamoja na corona "kutokuwepo kabisa, kuwepo kidogo sana...", wananchi wanahimizwa kulima mazao ya chakula kwa wingi, ili tuwauzie walioshambuliwa na corona na kushindwa kufanaya kazi. Lakini kama njaa ikiingia hapa, wananchi wanaambiwa wataachwa wafe kwa njaa!
Sasa tumefika hatua ambayo corona ni mipango ya mabeberu. Ni mbinu za kutushambulia katika vita vya kiuchumi. Hatutaki ma-barakoa yao. Chanjo zao ni njia ya kutuua ili waje kirahisi kubeba mali zetu. Wakati huo huo, juhudi kubwa zinafanyika kufufua dawa zetu za jadi kupambana na corona, ugonjwa ambao ni mafua tu kama mafua mengine.
Hata hivyo, kwani nani kauliwa na corona. Wanaokufa sasa hivi matatizo yao yanafahamika. Siyo corona ni changamoto tu za kupumua.
Tanzania Corona haipo! Kuvaa barakoa na kutumia njia nyingine za kujikinga ni alama ya kutokuwa na IMANI kwa 'mungu'.