Ansbert Ngurumo na Dkt. Minja mubashara kwenye Al Jazeera

Ansbert Ngurumo na Dkt. Minja mubashara kwenye Al Jazeera

Nchi ya kusadikika, nchi ya vipofu, nchi ya majuha...

Tusihangaike na wizi, kila mtu awe na jukumu la kulinda mali yake
Tusihangaike na mauaji, kila mtu awe na jukumu la kulinda maisha yake

Nilikuwa naota tu...
 
Yawezekana hulipendi sana kwa sababu unalikosea!

Mimi siikwepeshi lawama serikali pamoja na Rais Magufuli. Wanabeba lawama karibu zote.

Lakini pia, mimi kama raia huru mwenye akili timamu, sihitaji Rais Magufuli aniambie eti nivae barakoa au sijui ninawe mikono na maji tiririka au kuepuka misongamano.
Samahani kwa kukosea jina. Lakini hiyo Nyani ndiyo inayonikwaza, hasa kwa kuangalia tabiia ya nyani kwa sisi wakulima wa nyanda za juu kusini.

Nakubaliana nawe kwa 100% juu ya wajibu wetu. Lakini ufahamu kuwa katika jamii luna watu wa aina zote. Ndiyo maana mpaka kwenye majumba yetu tunaweka na mageti kwa sababu kuna irresponsible citizens.

Katika jamii kuna watu ni werevu, hawahitaji hata kufundishwa, kuna wanaohitaji elimu kisha wanabadilika, kuna wenye uelewa mdogo ni lazima wasukumwe, na kuna wabishi ambao ni lazima walazimishwe.

Kama Serikali isipofanya kitu, bita hii itapiganwa na hilo kundi la kwanza pekee. Na hilo kundi pekee haliwezi kufanikiwa kwa sababu jitihada zake zitaharibiwa na haya makundi mengine.

Fikiria unaenda kwenye basi, umejitahidi kutazama basi ambalo halijajaza abiria, mnaanza safari, dereva anasimama kila mahali hata wakati basi limejaa, wapiga debe wanazidi kuita abiria, nao kwa kuw ni wa yale makundi mengine, wanazidi kuingia, wewe uliyeingia mwanzoni, utafanya nini? Mazingira kama hayo, unahitaji mkono wa Serikali.
 
Kuna kiumbe anaitwa brazaj sijui Magufuli kamkosea nini yaani anaweza fungua nyuzi tano kwa mkupuo zote kulalamika.
Anyway tuchukue tahadhari na kuwa watulivu
Lakini hujajibu swali, nani kalalamika kuwa serikali imemzuia kuvaa barakoa?
 
Rais Magufuli kakosea sana kwenye suala la PR kwa kudai COVID-19 haipo nchini.

Huwezi kudai kitu hakipo, hususan ugonjwa unaosababishwa na ki/virusi [ambavyo havionekani], bila ushahidi.

Rais Magufuli ni mwanasayansi wa wapi yeye?

Mimi bado naamini C-19 si kali wala hatari kama inavyotangazwa, lakini hiyo haina maana watu wasichukue tahadhari, hususan wale walio medically fragile.
IMG_20210211_163253.jpg
 
Lakini mbona prime minister wa New Zealand alisema na wao Corona ilikwisha? leo hii wamerudi kwenye lockdown. Kama hakuna mgonjwa wa Corona hospitali utasemaje corona ipo? nchi nyingi zinapita humo humo kwenye vipindi vya Corona kupanda na kushuka, China, UK, Europe hata USA wote wameshawahi kupunguza makali ya lockdown wakidhani wako safe na Corona inatokomea for good. Watu wanang'ang'ania second wave kama ndio first wave, na yote hii ni kwasababu mwafrika kasema hakuna Corona.
 
Kwani, ili corona iwepo ni lazima awepo mgonjwa spitali?
 
Mambo hadharani, wanaokana uwepo wa Covid-19 Tanzania wanazidi kuumbuka.

Kubwa zaidi jumuiya ya ulimwengu wanaifuatilia Tanzania kwa ukaribu kuhusu hatua gani zitachukuliwa kuudhibiti ugonjwa huu na dunia pia maana Tanzania siyo kisiwa.

Mbinyo unazidi kuongezeka toka serikali za zinazotupa misaada, taasisi za kimataifa na sasa media kubwa kubwa ulimwenguni na mitandao ya kijamii isiyo na mipaka wote wameungana kuwa pamoja kuifuatilia serikali ya Tanzania inavyopambana na Covid-19 kwa njia zake ambazo dhahiri zinaonesha zimefeli ktk msimu huu wa wimbi la pili ya Covid-19 ilitojinyumbua yenye makali kuliko ile ya 2020.

Kazi kwenu serikali ya Tanzania na wizara ya afya ije na mkakati wa kueleweka na dunia kupambana kisayansi na Covid- 19 Toleo 2021.
 
Kuna kiumbe anaitwa brazaj sijui Magufuli kamkosea nini yaani anaweza fungua nyuzi tano kwa mkupuo zote kulalamika.
Anyway tuchukue tahadhari na kuwa watulivu
Unalaumu bure wanaolaumu au kulalamika. Wajiona wewe ndiye mwenye haki kulaumu na waliobaki hiyo haki hawana. Tatizo hapa ni thinking capacity yako kuwa na hitilafu. Haya mambo ya kuna kiumbe anaitwa au fulani anti- government yaonyesha defective thinking capacity. Kila kiumbe ana jina lake muite kwa hilo. Ni lake. Yeye ni yeye na wewe ni wewe. Hajafanya dhambi kuwa yeye. Wafanya dhambi wewe kumnyima yeye kuwa yeye.
Tujadili suala na sio watu. Hiyo kazi ina wenyewe na wanaiweza. Simple minds. Na mbona tunalo jeshi kubwa tu? Wanaolaumu/kulalamika hata kulalama si hoja. Hao ni watu tu. Hatupo hapa jf kuwajadili. Wanajadiliwa kwa kina na bashasha yote kule udaku. Hoja kwetu ni hicho wanacholaumu/kulalamikia kipo? Hilo ndilo suala. Hiyo saizi yetu. Tujadili. Hii ni hoja!
 
Hujajibu swali!
Kama hakuna wagonjwa hospitalini au kwenye vituo vya afya, inahesabika kama ugonjwa huo haupo nchini.

Au kwa lugha ya kitaalamu rate of infection (R number) ikiwa "chini" ya 0.9 then ugonjwa unaelekea kuisha na kutokomea.
 
Kipindi ni The Stream.

Kinaongozwa na Femi Oke.

Wageni ni Ansbert Ngurumo, akiwa yupo Stockholm, Sweden na Dkt. F. Minja, kutokea Atlanta, GA, USA.

Mazungumzo ni kuhusu madai ya Rais Magufuli kuhusu COVID-19.

Hawa Aljazeera ni wanafiki na wapuuzi, wanapaswa kupuuzwa kama ukoma.

Mwaka jana walionyesha video za watu wanazikwa usiku wakadai ni Tanzania. Wakamhoji Mbowe akadai watu elfu 30-40 wanakufa kwa siku.

Leo wanamhoji mkimbizi uchwara yupo Sweden. Anajua maisha ya Buza,Tandale na Tandika?

Kama Tanzania imefikia hatu anayodai kwa umaskini wa Tanzania hali ingekuwa hivi tunavyoona?
 
Umeshindwa kulijibu?
Kuuliza si ujinga lakini kuna swali la kijinga. Bahati yako kaliita duni. Hukuridhika. Ukauliza jingine. La kijinga hasa. Swali duni jibu pia duni. Wenye maswali duni na majibu duni nao ni duni. Don't argue with a fool, a passerby may not notice the difference!
Umefanya vizuri sana kwa ujumbe wako mzuri sana. Muda fulani Ngurumo na Minja wataongea. Kwani muda huo ni hao wawili tu watakaongea kuhusu suala husika? Kwa nini tuwasikilize hao na si wengine? Mwenyeji wetu katika hilo ni wewe. Unawajibika uwajue na hata kujua wataongea nini. Vinginevyo waweza tukaribisha kwenye karamu ya matango pori! Hujui Ngurumo ni mkimbizi? Kwa nini alikimbia? Unakuja na swali duni la alinusurikaje? Angalau ungegoogle na ni laptop yako tu ingejua ujinga wako. Sasa dunia nzima twajua ni ujanja wa nyani tu!
 
Back
Top Bottom