Anthony Joshua afanikiwa kumtwanga Wladimir Klitschko katika pambano la uzito wa juu

Anthony Joshua afanikiwa kumtwanga Wladimir Klitschko katika pambano la uzito wa juu

Saa mbili ndo hii na TV 1 kimya..Luna matv mengine hata sio ya kuyapa guarantee,yani nmebaki home nikiyategemea afu yanazingua..!!
Hahaha....hakika inakera ... Clouds TV wanasema watarusha pambano kupitia tovuti yao.... !!!!!!!!!????????
 
Hili pambano si jpesi kama unavyodhan klitschko ni mmoja wa mabondia wenye hard chins. Anthony hajakumbana na watu wenye roho kama ya evander holyfield au huyu klitschko. Pambano ni gumu sabab jamaa ana uvumilivu wa maumivu kwa kiasi kikubwa sana. Wakat anthony joshua ana uoga kias wa kuharibiwa uso. Klitschko ni mgumu kuanguka pia.

Na ukichukulia na uzoefu wake wa kupigana mapambano zaid ya 60 usimchukulie rahisi hata kidogo.hili ni pambano kubwa la kimataifa
Tena Anthony akileta usharo yatakuta leo
 
Kila mtu anaongea muda wake , mara saa nne, mara saa tano, mara saa saba tuamini lipi?Maana huyu mnigeria wa uingereza ni hatari katika dunia ya sasa atamrarua huyo vladmir mapema kabisa.

1. Yeye ana uwezo wa kutumia mikono yote miwili kwa kasi na nguvu ya ajabu wakati KLITCHKO anatumia zaidi mkono wa kushoto

2. Yeye ana nguvu za mikono na kila kombora analorusha ni nusu ya kifo hata ukikinga kwa mikono utaumia hadi kuuacha uso wakati KLITCHKO ni wale wapiganaji wanaoyegemea point

3. Upiganaji wake ni ule wa kufuata adui kwa kumshambulia tofauti na mwenzake anayejihami na kushambulia kwa kuvizia

4. Ni mtaalamu saana wa kupiga mapigo ya combination kitendo ambacho akikubahatisha moja ujua kwa sekunde moja zitafuatia zaidi ya ngumi thelathini hapo hapo pona yako ni kujidondosha

5. Ni mtaalamu kweli kweli wa kupiga ngumi ya dharau " UPPERCUT" na kikuwasha kwenye kidevu lazima udondoke chini

6. POLE SANA CLITHKO kwa kipigo utakachokipata usiku huu ambao huku madongo kuinama hatujajua muda kamili wala TV gani itaonyesha maana TV za bongo hazijui chochochote kinachoendelea duniani kwenye michezo zaidi ya MPIRA WA MIGUU.
Hahahaaaa umechambua vzr sana mkuu. Huyu AJ anadunda ngumi kali sana ingawa kliitshko naye vipigo vyake ni vikali.

Yote uliyosema ni sawa kabisa, wachambuzi wengi wa ngumi wanadai kwamba stength kubwa ya Klitshko ni uwezo mzuri wa kuutumia urefu wake ingawa kwenye hapa AJ ana urefu sawa na jamaa. Pia unaambiwa kwamba ww km mwanamasumbwi ukitaka ujute kwenye maisha yako basi cheza mchezo wa kuattack mbele ya Klitchko kwa sababu huyu jamaa anacheza mchezo wa kujilinda ambao ni hatar sana coz ngumi anazorusha pindi unapomfuata ni Mungu pekee anayejua. Kwa hiyo sasa ili uweze kusurvive kidogo mbele ya huyu mUkraine inakubidi upambane nae kwa kujilinda zaidi, sasa kitu cha ajabu ni kwamba Antony Joshua yeye ni bingwa wa kushambulia na kwenye hapa yeye amebobea.



Stength kubwa ya AJ yeye ni bingwa wa kushambulia kwa ngumi nzito kwa kasi kubwa sana. Kwenye masumbwi hakuna kitu kinachotisha na kuwaogofya wanandondi pamoja makocha wao ni kupambana na AJ, Kupambana na AJ ni zaidi ya majanga. Huyu brother hajui kitu kinachoitwa kupigwa, ana mingumi mizito sana na ndiye anayeonekana kufanana zaidi na Mike Tyson toka astaafu ndondi. Huyu jamaa ana mingumi mizito haijapa kutokea.
 
Mkuu umeongea kishabiki...Klitschko mkono wake wa kulia hautumii mara nyingi.....ila akiutumia ujue una balaa zito. Joshua kwa mara ya kwanza anaenda kukutana na mpinzani mzoefu na mvumilivu.

Joshua atapoteza pambano hili raundi za jua kuzama.

Amini maneno yangu.
haha muongo
 
Saa mbili ndo hii na TV 1 kimya..Luna matv mengine hata sio ya kuyapa guarantee,yani nmebaki home nikiyategemea afu yanazingua..!!
wamezingua, walitangaza lakini
 
Huu ugomvi Tv1aupo au haupo?halafu nimeisaka hiyo channel ya sky sports box office mobodro haipo wapu naweza kuistream jamani
 
Kwese TV wataonesha lakini naona TV 1 wameshajiunga na KWESE TV hivyo sogeeni karibu msikae mbali. Pambano nadhan kuanzia saa tano litakuwa hewani
 
Back
Top Bottom