Anwani za makazi za aina hii tuseme wote hapana

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Anwani za makazi ni jambo jema lenye Nia njema. Lengo lake ni kutambua tunapatikana wapi ndani ya mitaa, kata, tarafa, wilaya, mikoa ndani ya Tanzania. Kila mkoa, wilaya, tarafa, kata, vijiji na mitaa ina majina yake maalumu ambayo kama ukiyataja kila mtu atajua ni la mkoa na wilaya gani,

Lakini hali ni mbaya sana kwenye zoezi hili. Nimezunguuka jijini dar es salaam nikakutana na majina ya mitaa na barabara kama MT. Mchambawima, Ugweno, rombo, usangi, morogoro, ubena, Nyaishozi, maganzo, Kwamkunga, nk. Hii haikubaliki kabisa watu kuipa mitaa majina ya walikozaliwa na walikoolea wake zao, haileti maana kabisa na inachanganya watu. Wewe uko dar es salaam jina la Ugweno la nini huku gongolamboto? Uko kigamboni jina la morogoro kwenye mtaa ni lanini?

Majina haya yatazamwe upya.
 
Hilo siyo baya hata US kuna Oxford, (New) York, (New) Hampshire. Ila pia hapa hapa Dar kuna Lugalo, Kagera, hadi kwa Aziz Ally, Kwa Msuguri n.k

Huko mikoani nako kuna Oyster bay (Dodoma), Manzese (Kahama), Nyegezi (Shinyanga), Mtwango (Dodoma), Chamwino (Tabora) hali majina haya yana asili ya mikoa mingine.

Hata jina lako la ubatizo ni la kizungu au kiarabu!! Wabongo hatupendi majina yetu kwa hiyo tuendelee tuiga yale mazuri mazuri
 
Halafu mie nilijua serikali itatengeneza Barabara za mitaa maeneo ya fikike kama ile miradi ya World bank ya kule Temeke , Sandari, mikoroshini , Manzese n.k miaka ile ya Kikwete,

Badala yake kumbe ni mambo yale yale kuchukua majina ya watu ili wapate kodi !
 
Maeneo yako kienyeji badala ya kusimamia upimaji na kuweka barabara za mitaa ili miji ikae kwa mpangilio na kufikika ,

Watu magari wanalaza ofisi za CCM mbali na makazi, gereji, n.k sababu maeneo hakuna barabara za mtaa,

Ikitokea dharura ya ajali ya moto au mgonjwa itakuwaje Mungu aepushe mbali,

Eti badala yake wanachukua idadi ya watu sijui nini hata havieleweki.
 
Anwani za makazi ni jambo jema lenye Nia njema. Lengo lake ni kutambua tunaoatikana wapi ndani ya mitaa, kata, tarafa, wilaya, mikoa ndani ya Tanzania. Kila mkoa, wilaya, tarafa, kata, vijiji na mitaa ina majina yake maalumu ambayo kama ukiyataja kila mtu atajua ni la mkoa na wilaya gani,

Lakini hali ni mbaya sana kwenye zoezi hili. Nimezunguuka jijini dar es salaam nikakutana na majina ya mitaa na barabara kama MT. Mchambawima, Ugweno, rombo, usangi, morogoro, ubena, Nyaishozi, maganzo, Kwamkunga, nk. Hii haikubaliki kabisa watu kuipa mitaa majina ya walikozaliwa na walikoolea wake zao, haileti maana kabiza na inachanganya watu. Wewe uko dar es salaam jina la Ugweno la nini huku gongolamboto? Uko kigamboni jina la morogoro kwenye mtaa ni lanini?

Majina haya yatazamwe upya.
Kwa hiyo wewe hilo ndio umeona kwako ni tatizo Sana au? Ulitakaje sasa?
 
Ikiisha sensa lazima ulipe kodi, usipolipa kwa kutumia anuani ya makazi wanakuja home, pia ukiweka deni siku ukinunua gari au kuanzisha biashara mpya utalipa madeni yote,
Kumbuka TIN number ina taarifa zako zote
 
Anwani za makazi ni jambo jema lenye Nia njema. Lengo lake ni kutambua tunaoatikana wapi ndani ya mitaa, kata, tarafa, wilaya, mikoa ndani ya Tanzania. Kila mkoa, wilaya, tarafa, kata, vijiji na mitaa ina majina yake maalumu ambayo kama ukiyataja kila mtu atajua ni la mkoa na wilaya gani,

Lakini hali ni mbaya sana kwenye zoezi hili. Nimezunguuka jijini dar es salaam nikakutana na majina ya mitaa na barabara kama MT. Mchambawima, Ugweno, rombo, usangi, morogoro, ubena, Nyaishozi, maganzo, Kwamkunga, nk. Hii haikubaliki kabisa watu kuipa mitaa majina ya walikozaliwa na walikoolea wake zao, haileti maana kabiza na inachanganya watu. Wewe uko dar es salaam jina la Ugweno la nini huku gongolamboto? Uko kigamboni jina la morogoro kwenye mtaa ni lanini?

Majina haya yatazamwe upya.
Nilishangaa kuona huko mikoani eti mtaa wa kinondoni nikajiuliza maswali mengi sana sikupata jibu.
 
Nimezunguuka jijini dar es salaam nikakutana na majina ya mitaa na barabara kama MT. Mchambawima, Ugweno, rombo, usangi, morogoro, ubena, Nyaishozi, maganzo, Kwamkunga, nk. Hii haikubaliki kabisa watu kuipa mitaa majina ya walikozaliwa na walikoolea wake zao, haileti maana kabiza na inachanganya watu. Wewe uko dar es salaam jina la Ugweno la nini huku gongolamboto? Uko kigamboni jina la morogoro kwenye mtaa ni lanini?

Majina haya yatazamwe upya.
Hii bongo ina vituko kweli kweli...

Ulitaka mitaa yetu tuipe majina ya viongozi ?
 
Mimi kinachoniboa zaidi ni kuweka waandishi wa vibao VILAZA. Wanaharibu sana majina ya mitaa. Lakini pia napata changamoto ya kuelewa kipi ni kipi, mfano utakuta pameandikwa,' SHONVI ROAD, SHONVI MT, SHONVI ST. Tushike lipi?
 
Anwani za makazi ni jambo jema lenye Nia njema. Lengo lake ni kutambua tunaoatikana wapi ndani ya mitaa, kata, tarafa, wilaya, mikoa ndani ya Tanzania. Kila mkoa, wilaya, tarafa, kata, vijiji na mitaa ina majina yake maalumu ambayo kama ukiyataja kila mtu atajua ni la mkoa na wilaya gani,

Lakini hali ni mbaya sana kwenye zoezi hili. Nimezunguuka jijini dar es salaam nikakutana na majina ya mitaa na barabara kama MT. Mchambawima, Ugweno, rombo, usangi, morogoro, ubena, Nyaishozi, maganzo, Kwamkunga, nk. Hii haikubaliki kabisa watu kuipa mitaa majina ya walikozaliwa na walikoolea wake zao, haileti maana kabiza na inachanganya watu. Wewe uko dar es salaam jina la Ugweno la nini huku gongolamboto? Uko kigamboni jina la morogoro kwenye mtaa ni lanini?

Majina haya yatazamwe upya.
Zaidi ya kuwa affected emotionaly, sidhani kama kuna athari nyingine unaipata kutokana na hayo majina.

Binafsi kinachonitatiza ni kodi za hivyo vibao au hizo beacon. Wananchi bado wanaganga njaa, serikali inazidi kuwaongezea kodi na tozo.
Nchi hii! Yaani viongozi wanacopy na kupaste mifumo ya ukusanyaji kodi kutoka kwenye nchi zilizoendelea. Ilihali nchi hii ina rasilimali nyingi
 
Kwani hayo si majina tu.na inawezekana hiyo ugweno ya daresalamu ikawa ni kongwe kuliko ugweno unayoijua.Sio lazima morogoro iwe moja duniani,cha msingi nikujua maana na sababu za hayo maeneo kuitwa hayo majina.
 
Hilo siyo baya hata US kuna Oxford, (New) York, (New) Hampshire. Ila pia hapa hapa Dar kuna Lugalo, Kagera, hadi kwa Aziz Ally, Kwa Msuguri n.k

Huko mikoani nako kuna Oyster bay (Dodoma), Manzese (Kahama), Nyegezi (Shinyanga), Mtwango (Dodoma), Chamwino (Tabora) hali majina haya yana asili ya mikoa mingine.

Hata jina lako la ubatizo ni la kizungu au kiarabu!! Wabongo hatupendi majina yetu kwa hiyo tuendelee tuiga yale mazuri mazuri
Kwa musuguli, kwa Aziz ally, kwa kimaro, kwa msuya hiyo ni sawa kwakuwa huyo mtu ni maarufu kwenye huo mtaa na anafahamika, lakini kuita mtaa jina la morogoro, Ugweno, maganzo. Hayo majina ya Kagera, Kampala University, nk ni majina yaliyopewa majengo kama guest, chuo, daraja, saloon, kiwanda, soko au garage, hivyo watu wakapazoea kwa kija hilohilo la jengo au taasisi. Lakini hii ni mtu TU anaamua TU aite mtaa mpya jina la morogoro, shinyanga. Huu ni upuuzi sawa na upuuzi mwengine mtaani,
 
Kwa hiyo wewe hilo ndio umeona kwako ni tatizo Sana au? Ulitakaje sasa?
Majina yalipaswa yatolewe kutokana na matukio na vitu halisi na maarufu kwenye eneo lile kama vile tukio, mti mkubwa, mtu maarufu, jengo maarufu, taasisi maarufu kwenye mtaa ule na sio mtu asiyekuwa maarufu Wala msaada wowote kwenye mtaa ule kutoa hongo na kutoa jina lake la alikozaliwa hawala yake.
 
Maeneo yako kienyeji badala ya kusimamia upimaji na kuweka barabara za mitaa ili miji ikae kwa mpangilio na kufikika ,

Watu magari wanalaza ofisi za CCM mbali na makazi, gereji, n.k sababu maeneo hakuna barabara za mtaa,

Ikitokea dharura ya ajali ya moto au mgonjwa itakuwaje Mungu aepushe mbali,

Eti badala yake wanachukua idadi ya watu sijui nini hata havieleweki.
Du..!! Kunawatu kumbe hawapo serious kabisa. Unamiliki mpaka gari lakini unaishi sehemu ambayo gari halifiki nyumbani. Watanzania wengi wanazitumikia pesa badala ya pesa kuwatumikia wao.
 
Hilo congo lilikuwa jina la studio, yaani kama ukianzisha saloon yako ukaipa jina la nguchilo na watu wengi wakazoea na kufurahia huduma zako hilo jina linaweza kuwa maarufu kwenye eneo hilo automatically. pale Kagera ni jina la guest moja ya zamani sana pale.
 
Kwani hayo si majina tu.na inawezekana hiyo ugweno ya daresalamu ikawa ni kongwe kuliko ugweno unayoijua.Sio lazima morogoro iwe moja duniani,cha msingi nikujua maana na sababu za hayo maeneo kuitwa hayo majina.
Hilo jina halikuwepo kabisa kwenye mtaa huo bali ni jipya lililokuja na zoezi la anwani za makazi.
 
Back
Top Bottom