Anwani za makazi za aina hii tuseme wote hapana

Una tatizo si bure
 
Du..!! Kunawatu kumbe hawapo serious kabisa. Unamiliki mpaka gari lakini unaishi sehemu ambayo gari halifiki nyumbani. Watanzania wengi wanazitumikia pesa badala ya pesa kuwatumikia wao.
Nyumbani anaacha elfu 5000 ya matumizi lakini kwenye gari anaweka mafuta ya sh 10000. Familia inalalamika na watoto wananyimwa hela ya shule. Watu wanarukia kununua magari yanayowatesa wao na familia.
 
Waliopendekeza ndio wenye mitaa sasa kama inakuboa wewe hilo ni swala lako binafsi.
 
Uelewa wako mdogo. Dar kuna mtaa ya Lindi kuna ubaya gani kwa majina hayo kuwepo.
 
Huu ni uvivu wetu waswahili hata kufikria majina tumeshindwa, ukienda Arusha kuna sehemu inaitwa Uzunguni, ndiyo yale yaleee wazungu walipojenga reli wakaweka vibao vya kuonya madereva maeneo ya kukatisha reli kikasomeka "check rail" mswahili akapaita "chekereni", kwenye round about pakawekwa kibao kuelekeza "keep left" mswahili akapaita "pale kiplefti" hahaaaaa..
 
Du..!! Kunawatu kumbe hawapo serious kabisa. Unamiliki mpaka gari lakini unaishi sehemu ambayo gari halifiki nyumbani. Watanzania wengi wanazitumikia pesa badala ya pesa kuwatumikia wao.


Hilo halina jibu la aina moja!

Wengine wanalala na magari ya kazi kutokana na jeographia ya anapoishi na aina ya kazi zake,

Wengine ni Nyumba za kurithi za wazazi wao , Je wahame wakapange wakati Nyumba za urithi za kuishi bure ?

Pia Gari ni kitendea kazi si anasa, mtu anaweza kuamua kuanza kununua gari kabla ya kujenga ili gari imrahisishie follow up mbalimbali.

Tafakari Kwa mapana!
 
Kama haujapata mtaa unaoitwa jina lako makasiriko ni lazima.
 
mmm unakichwa kigumu haya tupe majina unayoyataka wewe
 
Mimi kinachoniboa zaidi ni kuweka waandishi wa vibao VILAZA. Wanaharibu sana majina ya mitaa. Lakini pia napata changamoto ya kuelewa kipi ni kipi, mfano utakuta pameandikwa,' SHONVI ROAD, SHONVI MT, SHONVI ST. Tushike lipi?
Jambo limishaaachiwa Halmashauri huwa linakuwa takataka kabisa utafikiri huko Halmashauri hakuma.watu went akili timamu.

Majina ya Mitaa yalipatikana kupitia Wananchi wenyewe hasa Diwani, Watendaji na Wenyeviti wa Vijiji.

Sasa Kama wao wenyewe wameamua kuita hayo majina wewe Ni Nani ukatae
 
Sasa wewe ulitaka majina yatoke wapi? Na wewe nenda ukalipie halafu uandike jina lako hapo mtaani, usiwaonee wivu wenzako.
 
Kama ni nyumba ya urithi uza kanunue sehemu inayofikika Jenga hapo nyumba nyingine.
 
mitaa imekutwa na majina yake halisi yaliyozoeleka,sasa unaleta mapya ya nini lengo si kwa manufaa ya wakazi wa pale? Huu ni upimbi wa kiwango cha daraja la mgugale
 
Yes watoe majina Yao sio wa mikoa na miji nje Jiji
 
mitaa imekutwa na majina yake halisi yaliyozoeleka,sasa unaleta mapya ya nini lengo si kwa manufaa ya wakazi wa pale? Huu ni upimbi wa kiwango cha daraja la mgugale
Kama kulikuwa na jina lililokuwa linatumika kwa ajili ya mtaa fulani kabla ya kuanza kwa usjili wa anwani za makazi na wakati wa isajili, wasajili wakaja na jina lao la mchongo; hapo kuna tatizo kubwa.

Hiyo nimeiona sehemu boya mmoja msajili kaweka jina la baba yake kwenye barabara ya mtaa fulani wakati baba yake hajawahi hata ishi mitaa hiyo.
 
mie nmecheka juzi nmeenda nliponunua kiwanja kukifanyia usafi nakuta wameweka kibao cha oysterbay street
 
Ujinga tu na bado tunauziwa hadi namba za kubandika kwenye mjengo kwa lazima
 
kwani anwani ya makazi haina sheria,kanuni,taratibu na muongozo? kama ndo zinasema hivo basi kosa lipo kwa watunga sheria but kama hamna regulation ya hili zoezi then it is very absurd to implement public projects without regualation, watu wataweka hata majina ya michepuko yao
 
Kama ni nyumba ya urithi uza kanunue sehemu inayofikika Jenga hapo nyumba nyingine.



Unaweza kuuza iwapo ni mmoja na uko peke yako kitu ambacho ni nadra kutokea vinginevyo huwa sio rahisi sana kama unavyoandika hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…