Aonavyo Boniface Jacob kuhusu msanii kuvunjika jukwani Mapokezi ya Makonda

Aonavyo Boniface Jacob kuhusu msanii kuvunjika jukwani Mapokezi ya Makonda

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
59,045
Reaction score
94,974
Anasema hivi.....
See new posts

Nitoe pole kwa msanii aliyepata ajali ya kuvunjika uti wa mgongo katika jukwaa la CCMAkiwa anafanyia kazi ya kucheza muziki wa dansi wakati CCM ikimpokea Makonda.

Pole kwa msanii husika, wasanii wote na pole kwa familia yake. Nimesikitishwa na kauli za kejeli kutoka kwa katibu mwenezi Ally Bananga wa mkoa wa Dar es salaam baada kijana kupata ajali akiwa chini bila kupata huduma ya kwanza.

Bananga anasikika akisema anafamya usanii au ameenda (kufa) badala ya kumpatia huduma ya kwanza. Bananga anasikika tena akisema wamuulize aliyepata ajali ya kuvunjika uti wa mgongo kama amekula. Imeniuma sana, sawa inawezekana mnajua wasanii wa Tanzania wana njaa lakini haikutakiwa kutweza utu wa mtu wakati wa maumivu makali na ajali kama ile. Nimevaa uhusika wa yule msanii (kijana) kama ndiyo mimi nimejikuta nimelia sanaaaaaaaaa


My Take: Wasanii wawe waache kushobokea siasa za CCM.

 
Nimependa hapo kwenye Mytake, kwamba wasanii waache kushobokea siasa.
Na wala siyo wasanii waache kushobokea CCM.

Hiyo ajali inaweza kutokea akiwa anaitumikia Chama chochote, Iwe CHADEMA, ACT, CCM, nk.
 
Kipindi Cha marehemu captain Komba. Kuna vijana walikuwa wanatengeneza jukwaa kama sio kushusha vitu kwenye lile gari la burudani la T.O.T
Kijana mmoja akaumia,kiongozi mmoja wa pale akasema mnatafuta vijana legevu Wala unga.

Niliichukia CCM toka siku ile
 
Alikuwa hajafahamu kama ni serious case.

Ahsante kwa taarifa.
 
Back
Top Bottom