APHFTA: Tutasitisha huduma za NHIF kuanzia saa sita usiku, wagonjwa mahututi tutawaongezea saa 48

Bima Tanzania? Nchi ambayo serikali inachota pesa kila sehemu na hatujui huwa zinapelekwa wapi. Watakwambia tunajenga barabara, Siko Report ya CAG ikitoka unaambiwa hiyo barabara imefadhiliwa na Bank ya Dunia.

Unaanza kujiuliza zile pesa zilienda wapi, walisema walijenga barabara, hapo sasa utapata mvi na vipara ukiwa kijana mdogo kabisa kwa kutaka kuwaelewa ccm.

Serikali kazi yao kulazimisha tu, utasikia pokeeni wagonjwa, Hospitali zinapokea na kutoa huduma. Hospitali zikipeleka bill huko NHIF unaanza kusikia ohoo, tunahakiki, mara bill kubwa utadhani huduma walitoa wao.

Mkitaka vitu rahisi wapelekeni wagonjwa wenu wa NHIF wote hospitali za serikali, huko mdaiane wenyewe, mlipe msilipe sawa.

Mkitoa huduma hafifu, mtajuana huko huko na siasa zenu. Pesa mchukue nyie huduma watoe wengine, mkiambiwa mnaleta ujanja ujanja, na mapambio ya Anaupiga mwingi.

Serikali iboreshe huduma hospitali za umma ili na wao viongozi watibiwe huko, ndio nchi itapendeza. lakini hili la class A na class Z, tutashuhudia mengi sana.
 
Serikali imetoa sera mpya za bima, ikaziita maboresho. Madaktari wanaovutana na serikali nao wamekariri, wanatumia neno hilo hilo maboresho! Unapinga maboresho! Basi huna akili kichwani kama unapinga kitu ambacho wewe mwenyewe unakiita maboresho... Waandishi wa Kayumba nao wamemeza, wakakitema, kama kilivyo, vile vile kilivyotangazwa na serikali, maboresho! Watu wasomi, madaktari, waandishi wazima, logic vichwani zero. Hawana sense ya kutumia neno mabadiliko ya sera!
 
Wewe umeongea point
 
Julius akirudi leo hii atashangaa sana jinsi watoto na wajukuu zake walivyobadilika na kuwa mamangimeza zaidi ya alivyokuwa mkoloni!

Watu wanaendekeza tamaa binafsi za kuchuma hata wasipostahili hata kwenye uhai wa binaadam[emoji848]!
 
Hiyo sio sera mkuu..
Ungekuwa Mfatiliaji tu ukajua ni nini..
Hicho ni kitita ambacho huwa kinatoa Mwenendo wa bei za Bidhaa na huduma kwa Hospitali
 
Magufuli angetatua huu mgogoro wote kwa sentensi moja tu, tena akiwa barabarani.

Ulale salama Magufuli, tutakukumbuka daima.
Angesema waache wagome. Serikali ina hospitali nyingi. Wagonjwa wataenda hosp za serikali.
 
Sio Bure Wanakatwa mshahara wao kila mwezi..
UKiangalia makato mwaka inaweza kufika laki sita mpaka laki saba...
Kwa sio mtu anakatwa laki sita kwa Mwaka ili atibiwe
 
mzee MAGU angekuwepo huyu jamaa 2ngemuokota kwenye kiroba!!
 
Lakini wanatoa huduma Bora kuliko vituo vya serikali
Sio kweli ni dhana tu,ni kama kipindi kile tulipokuwa tunaamini Kila kinachotengenezwa tz ni feki Kwa Sasa huduma Bora za kibingwa zinapatikana hospitali za serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…