Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

TAKWIMU ZA MECHI KATI YA AC MILAN NA ARSENAL.
tokea nizaliwe sijapata kuona mpira ambao kwa namna moja au nyingine mwenyezi mungu akinipa mtoto basi ni lazma nije nimuadisie.
mpira ulikuwa nikati ya vijana na wazee ambao wamekuwa wakiogopewa na vilabu vingi barani europa na dunia kwa ujumla.
nimeshuhudia vipaji vya hali ya juu toka kwa timu zote mbili, na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja na timu zote kwa ujumla.
pia katika pambano hili nimemsifu refa ambaye ameonyesha ukomavu wa hali ya juu na ni refa aliyejuwa kuwa dunia nzima mpaka mbinguni watu wanaitazama mechi hii, hivyo hakuwa na maamuzi ya kipuuzi kama ya yule refa aliyeiharibu mechi ya fainali ya champions ligi kati ya arsenal na barcelona mechi ambayo wataalamu na wachambuzi wa maswala ya soka wameweka wazi kuwa mechi ile iliisha katika dakika ya 18 ya kipindi cha kwanza pale refa ambaye uwezo wake ni wa kuchezesha mechi ya abajalo na sinza star alipotoa maamuzi ya kipuuzi yaliyoharibu radha ya mechi na kufanya mechi iwe ya upande mmoja.
awali ya yote ntakuwa si mwenye busara kama sintamsifu refa huyu aliyeshika kipyenga kati ya wazee milan na vijana arsenal.

FIRST HALF.
mechi ilianza na milan walionekana kana kwamba wanataka kupata kitu ambacho kitawalinda na kuwafanya vijana wa arsenal wanyong'onyee na kupoteza mwelekeo.
lakini haikuwa hivyo kwani katika dakika za mwanzoni tu za kipindi kwa kwanza arsenal walionekana nao kuto kubaki nyuma na kupeleka mashambulizi langoni mwa wazee milan, kitu kilichowafanya waondokane na hali ya woga na kuanza kujenga kujiamini kuwa nao wanaweza.

UNTOUCHABLE UNSTOUPABLE ARSENAL.
ni wazi kuwa mabeki wa milan wamepata tabu kutokana na kushindwa kutambua wamkabe nani na wamwache nani.
Diaby, Hleb, Adebayol, Eboue, Flamini na man of the Match Cesc Fabregas ndio waliohusika haswa kutia pilipili machoni kwa milan. ama kwa hakika wachezaji hawa ndio waliotimiza maandiko ya biblia yanayosema "MZEE ATAPELEKWA ASIPOTAKA".

MILAN NA UKUTA WA CHUMA.
hakuna ubishi kuwa simba hazeeheki meno.
milan wana ukuta imara na usiopenyeka kirahisi.
wanao uwezo wa kucheza mipira ya kichwa, wanao uwezo wa kuzuia pasi za chini za adui, wana mabeki wa pembeni wenye uwezo wa kupanda na kupiga krosi na kurudi kuzuia, na pia wana mabeki wa kati wenye mbio na mbinu za kuwazuia washambuliaji.
kitu hiki ndicho kilichopelekea mechi kuwa ngumu na yenye msisimko.

FABREGAS ANAGONGESHA MWAMBA.
hii ilikuwa ni katika kipindi ambacho kama refa angekuwa ni trafiki basi tunaweza kusema ameruhusu magari ya upande mmoja na kuzuia mengine, kwani kilikuwa ni kipindi ambacho "msako ulifanyika haswa golini kwa milan".
kuanzia dakika ya 25 milan walikimbizwa sana na kupelekea baadhi ya mabeki wao wazee kuanza kuinama na kujishika vichomi.
man of the match Fabregas alipiga mashine (shuti) ambalo liligonga mwamba na kutaka kupeleka msiba mapema kwa milan al maarufu kama (rosonelli) na hii ilikuwa ni salam tu.
si hilo tu kwani vijana wa arsenal waliendeleza msako wa kila upande na kufanya baadhi ya washabiki wa milan kuanza kuvua jezi zao ili wasijulikane wapo upande upi.

HALF TIME NA UKAGUZI WA ANCELLOTTI.
kocha wa milan amekiri kuwa alisimama mlango wa kuelekea vyumba vya mapumziko na kuanza kuwahesabu wachezaji wa arsenal ambao yeye binafsi alikuwa anawaona kama vile wapo 17 uwanjani.
lakini mwisho wa yote alikuja gundua kuwa arsenal wako 11 kama walivyo wazee wenzake milan.

SECOND HALF.
hiki naweza kusema ndo kipindi kitamu katika mechi hii.
ni kipindi tulichoshuhudia magoli maridhawa ambayo hakuna mchezaji yeyote wa milan aliyediriki kumkimbilia refa ili kubisha.
na pia ndo kipindi tulichoshuhudia mchezaji bora wa dunia Ricardo Kaka' akipewa kadi ya njano kwa kuonyesha wazi kuwa amezidiwa mbinu na amechanganyikiwa.

MILAN WANAAMKA.
moja kati ya vitu tulivyotaraji kuviona mapema katika mechi hii ni milan kutawala kiungo.
hii inatokana na milan kuwa na viungo wanaoheshimika na wenye ujuzi na uzoefu wa hali ya juu.
Ambrosini, Pirlo, Ivan Genarro Gatusso na Ricardo Kaka' ni viungo wanaoelewana sana na wenye uwezo wa hali ya juu, kiasi kwamba mara nyingi wamekuwa wakitawala kiungo katika mechi nyingi.
wanajua kukaba, kutoa pasi za mwisho nabaadhi yao wanajua kuendesha timu ipasavyo.
na mwanzo wa kipindi hiki cha pili ni kuwa milan walionyesha kweli pale ni uwanjani kwao na si kwa vijana wa arsenal.
milan walionekana kupanga mashambulizi mazuri lakini mwisho wa yote yalikuwa ni mashambiulizi yaliyoishia kwa mabeki imara wa arsenal Sanderous, Clichy, Sagna chini ya captain "nguli" William Gallas.
na katika muda huu ni wazi kuwa kama arsenal wangerudi nyuma basi wangewapa fursa wazee hawa wa milan kutawala mchezo nakupelekea kuanza kupanga mipango yao ya ushindi na hata kuifanikisha.

USIPOUANIKA UTAUTWANGA MBICHI.
kama milan wangekuwa wanamahusiano na msemo huu basi wangejitahidi zaidi katika kipindi hiki na kutumia uzoefu walionao kuweza "kuepuka kufika karivali"
lakini kadri muda ulivyozidi kwenda wenyeji milan walionekana kana kwamba walikuwa wameshinda mechi yao ya kwanza wiki mbili zilizopita katika uwanja wa kisasa wa Emirates lakini la hasha.

TALLENTED VS EXPERIENCE.
kadri giza linapozidi kuwa nene ujue alfajiri inakaribia, milan mara kadhaa walikuwa hatari katika lango la arsenal, na mara kadhaa walipata kona zilizotaka kubadili hali ya hewa lakini uimara wa golikipa Manuel Almunia ulizidi kuwapa ubishi arsenal.
ni wazi experience ya milan ilionekana kupungukiwa na mbinu kiasi kwamba walishindwa hata kuelekezana wapi kuna mapungufu, na hii ilipelekea vijana wenye tallent wa arsenal kuonekana kama vile wapo nyumbani kwao.

KWA NINI HAKUKUWA NA MASHUKA MAKUBWA YANAYOWATUKUZA WAKINA KAKA'?
mmiliki wa timu Silvio Bellusconi pamoja na swahiba wake asiyekaukwa na maneno ya kujisifu bwana Adriano Galliani haijulikani ni kwa nini hawakuwepo uwanjani.
ila utamaduni wa washabiki wa milan ni kushika mashuka makubwa uwanjani yenye maneno yanayowatukuza wachezaji wao kama vile (siempre Nesta) (pena inzaghi) (sforza maldini) (gilamania) (galacticous fantasticous kaka') lakini ni wazi kuwa hakukuonekana kitambaa chenye udogo sawa na leso chenye kuisifu milan, je ni kwa nini?
akili kichwani mwako.

MATESO YAKIZIDI JUWA WOKOVU UNAKARIBIA.
katika dalika za 70-80 milan walifanya mashambulizi mengi kiasi wanaojua hadithi za wazee hawa walianza kukaa sawa wakitaraji muda wowote mambo kuiva na mara kadhaa yalikuwa ni mateso makubwa kwa washabiki wa arsenal.
lakini kama nilivyosema hapo awali mashambulizi ya milan mara zote yaliishia kwa wachezaji wa arsenal.

FLAMINI NI ZAIDI YA GATTUSO.
flamini mara kadhaa amekuwa akimnyang'anya mipira kiungo tegemeo wa milan kaka', lakini gattuso mara zote alipomfuata fabregas alipata aibu.
na hii iko wazi hata ukienda kumuuliza gattuso akiwa peke yake atakudhihirishia hilo.

ITALIAN JOB.
kuanzia dakika ya 80 arsenal sasa walionyesha kuamka na kuudhihirishia ulimwengu nini kimewapeleka italy, na wao walianza kujibu mashambulizi kuelekea golini mwa milan na kuanzia hapa sasa ndipo mambo yalipoanza kuwachachia mambingwa hawa watetezi.

THE CIRCLE IS COMPLETE.
man of the match cesc fabregas akiwa anakabwa na kiungo mwenye bugudha gennaro gattuso anapiga shuti maridhawa linalompita kipa mrefu kiumbo na kiumri na kutinga katika nyavu za uwanja uliozungukwa na nyavu za kuwazuia wahuni wa sansiro wenye uwezo wa kubeba watazamaji takriban 90 elfu.
na hii ilimaanisha ili mabingwa hawa watetezi wafuzu hatua ya robo fainali basi ni lazima wafunge magoli mawili.
swali ni je wangeweza kupenya ngome imara ya arsenal na kufunga magoli hayo?

MGONJWA ATAKA KUTEMA DAWA.
hapa wazee waliamka na kutapatapa tena na kuanza mashambulizi yao ambayo ili yawarudishe mashabiki wao ambao walishaanza kutoka uwanjani ilikuwa ni lazima washinde magoli mawili.
lakini kwa hali ilivyokuwa sizani kama kuna mtu alifikiria kuwa hilo lingewezekana.
na kuanzia muda huu sikumuona tena bingwa wa mbinu Carlo Ancelotti na sina taarifa zake zozote.

DOCTOR ANAKUFA, MGONJWA ANABAKI.
adebayol yule anayepondwa na mashabiki wenzetu kuwa hana lolote la ajabu anawadhihirishia mahasidi kuwa yeye hakununuliwa kimakosa na ndiye anayeandika bao la pili linalowauwa mabingwa mara 7 na goli hilo linawalazimu milan wafunge magoli matatu ili wafuzu.
kwa kifupi katika mechi hii hata kipa angekaa Sanderos basi arsenal wasingefungwa.

FULL TIME.
refa anamaliza mechi iliyokuwa na mikiki na kiwango cha hadhi ya nyota 5 na kupelekea arsenal wafanye kile walichoshindwa timu zoote za uingereza toka karne ya 19.

KINYWA CHA MTU MZIMA KINANUKA ILA MANENO YAKE HAYANUKI.
baada ya mechi kocha wa arsenal mfaransa Arsene' Wenger amesema kuwa alichokifanya sansiro ni salam kwa timu yoyote ambayo itakutana na arsenal katika kombe hili.
na ameweka wazi kuwa timu atakayopangwa nayo robo fainali "itachambia upawa badala ya kopo".

MUHIMU:
1) arsenal wamewafungwa na kuwatoa mabingwa watetezi wa klabu bingwa barani ulaya.
2) arsenal wamewafunga mabingwa wa dunia.
3) arsenal wamevunja mwiko wa milan kutofungwa kwao na klabu za uingereza.
4) arsenal ndio timu inayocheza soka ambalo inasemekana linachezwa mbinguni.
5) arsenal imeifunga timu yenye wachezaji wenye umri mkubwa barani ulaya.

VISINGIZIO LUKUKI.
wengi wa wasiojua soka watauponda ushindi huu wakijitetea kuwa milan wamemkosa Dida na Serdolf.
ila wakumbuke pia arsenal wamewakosa Toure, Rosicky na kamanda Robin van Persie.

uchambuzi huu umeandikwa
na shabiki mwenye kadi
Gang Chomba
.....................
 
Hodi watani wa jadi!
Binafsi nawashukuru kwa kutuondolea Milan katika kinyang'anyiro, mwaka huu lazima kombe liende Man U.
Hongereni sana watani wa jadi.
Big up sana.
 
Wakuu heshima yenu na nawaunga mkono kwa furaha tuliyo nayo wana Gunners.

katika mchi ya kwanza mpira ukichezwa kwa kuviziana mno na ingawa watu hawakuwa wakipia nafasi Arsenal kutokana na umaarufu wa AC Milan na intimidation ya footbalmad fans wao, Wenger alikuwa na imani na chipukizi hawa.

Ac Milan waliacha mbinu yao ya kujilinda na wakajaribu kucheza kwa kushambulia huku Kaka bado akiwa hayuko "fit" na Alexandro nesta pia alikuwa amepasi "fitnes test" usiku kabla ya mechi yenyewe, kwa hiyo kwa mtindo wa Arsenal wa kumtumia Adebayo mbele huku Alex Hleb akiwa anamsaidia kumeleta matokeo mazuri ambayo yalikuwa yakingojewa pale San Siro.

Sasa tunakwenda Wigan tupate pointi tatu na kuwa 4 points clear kabla ya kuwakaribisha Middlesbrough hapa Emirates.
 
Arsenal tunasonga tu mbele mzee bila taabu hakuna cha Milan au nini- mambo mwendo mdundo tu!

MU mpo?
 

April

1st. Tue Champions League (Home) Arsenal Vs Liverpool
(Match to be played on either Tue 1 or Wed 2 April)

5th. Sat Barclays Premier League (Home) Arsenal Vs Liverpool 12.45pm SS1

8th. Tue Champions League (Away) Arsenal Vs Liverpool
(Match to be played on either Tue 8 or Wed 9 April)


Duuuuh! wazee hii naona haijatulia sana, in one week tunakumbana nao hawa 'bwawa la maini' mara tatu!? ...mmmnh!
 
Pole Ganaz, pia pole Liva! Hapo inamaanisha kukosa ubingwa kwa mmoja wao.
 
Jamani Arsenal kunani??

...kuna 'bundi' anayetuletea 'Gundu'...! au ndio skills zinaanza kuzidiwa na experience? machungu ya kupoteza 'kila' kitu kama last season yanaanza kuninyemelea.
 
Jamani Arsenal kunani??

Mambo mazito lakini bado tuna timu nzuri tu ya kuweza kumuaibisha Sir Ferguson nyumbani kwake April 13th, 2008 na pia kuwachapa Chelsea next Sunday na hatimaye kuwachapa L'pool hapo April 5th, 2008. Jana referee kafuta goli la wazi kabisa na kutunyima penalty nayo ya wazi kabisa, labda na wao wameanza kampeni ya kuhakikisha MANU wanatetea taji lao. Kazi yetu imekuwa nzito zaidi lakini I still believe we can do it, it is just a matter of determination.
 
Sack off GALLAS to be ur skipper!!, he is spoiling your team!!,sor fellas.... lets forget about title this season!
''you can win nothing with kids&thin squad like ours!
 
Arsenal itachukua Ubingwa wa Champions League mwaka huu. Na final wataingia na barcelona kwa maoni yangu. Kwenye EPL naona wataishia wakiwa wa pili nyuma ya Man Utd.
 
Sack off GALLAS to be ur skipper!!, he is spoiling your team!!,sor fellas.... lets forget about title this season!
''you can win nothing with kids&thin squad like ours!
I dont think the problem is Gallas, the kids can play football but the main problem is in their heads.
 
I dont think the problem is Gallas, the kids can play football but the main problem is in their heads.

Unafikiri wanatatizo gani kichwani mwao?au wanamawazo gani wawapo uwanjani?Kuna mdau mmoja juu ameongea nukta kuwa ujuzi umeanza kuzidiwa na uzoefu..ingawa sometimes its not true...maana pale san siro vijana wa gunners walionesha ujuzi upo juu zaidi ya ukongwe..so kwa sasa nikuweweseka tu.Nasikitika kwa kukata tamaa mapema wakati ligi bado inaendelea..
 
Wazee wa kikosi cha mizinga msinyong'onyee sana, we have already beaten the best team in europe tena in their backyard sasa sioni kwanini tuwashindwe hawa Liverpool. We are going to score at Anfield coz we have always done that, its gonna be an early goal and that will force them to come forward- this will give us a chance to score another goal. Im a bit dissapointed bse we have drawn a game we should have won, yule refa ni mholanzi na ni kweli kwamba anatokea kijiji kimoja na Kuyt ndio maana katubania ile penalty.Msife moyo watu wangu.
 
Wazee wa Arsenal msijali sana.....

So far mahali tulipofika ni pazuri sana, na tumeonyesha kwamba ile timu ambayo haikupewa nafasi mwanzo wa msimu imekuwa tishio msimu wote.

Watu wanailaumu timu isivyo kihalali....tumepata majeruhi wengi sana esp kwenye striking force, ukianza na van persie(ambaye mpaka saivi hajacope vizuri), rosicky and eduardo. Pili angalia kukosekana kwa Sagna na Flamini. Hao ni watu wa nne wa timu ya kwanza wamekosekana.

Tafuta timu yoyote duniani, watoe 4 key players nje, then utaona matokeo yatakavyokuwa.

Hongera sana Gunners, with all happening around, you are the best team on earth.
 
mara kadhaa nimekuwa nikijiuliza hivi ni kwa nini washabiki
huingia uwanjani na kutoa mkong'oto kwa waamuzi?
na mara kadhaa marefa wamekuwa wakilaumiwa
kwa vitendo vyao vya upendeleo dhahiri?


jibu nimelipata usiku wa kuamkia jana tarehe 8 april....
jibu hili nimelithibitisha jana katika uwanja wa Anfield
uliopo katika viunga vya jiji linaloongoza kwa vijana wasio na kazi
na matukio ya mara kwa mara ya kubakwa wanawake na watoto hapa uingereza.


ni wazi kuwa mechi kati ya arsenal na liverpool ilipoanza
kama kuna mtu alikuwa hajacheza kamali kabla
basi angeweka kucheza na hata kuweka dau la hati ya nyumba nyuma ya arsenal
kwa jinsi vijana hao wa emiraa walivyoweza tawala mpira
na hata kupelekea kupata goli saafi
ambalo halikuwa hata na chembechembe yoyote ya dhuluma.


na ni wazi kuwa mambo yalionekana dhahiri kumuendea kombo kocha wa liverpool
kwani mpaka dakika ya 30 kipindi cha kwanza alikuwa amekwishajaza counter book
makosa yaliyofanywa na timu yake ya liverpool.


lakini wachambuzi wenzangu wa maswala ya soka wameweka wazi kuwa
matukio ya kuibeba liverpool yanayoendelea kufanywa na marefa mara kwa mara
yanaonekana ni kumbeba kocha wa liverpool Rafa Benitez asipoteze ajira yake
ambayo mpaka sasa hana uhakika nayo, na wazi kuwa amekalia kuti kavu.


kocha wa inter milan Roberto Mancini aliilaumu bodi nzima ya UEFA
kwa kile alichookiita kuwa ni "uzembe wa waamuzi"
pale refa asiyekuwa na hadhi aliyechezesha mechi kati ya inter na liverpool
alipomtoa kwa kadi nyekundu beki wa kati wa inter milan
jogoo marco materrazzi kufuatia kujiangusha
kwa mshambuliaji Fernando Torres.


na kama haikuishia hapo kocha wa arsenal mfaransa Arsene' Wenger
pia alipeperusha malalamiko yake kwa ulimwengu pale kiungo wa Arsenal
Alexandr Hleb kuvutwa na kupelekea kuangushwa ndani ya eneo la hatari
katika mechi ya kwanza ya klabu bingwa barani europa
iliyofanyika katika dimba la kisasa kabisa la Emiraa.
lakini mpaka tukio hilo linatokea ambapo lilitokea mbele ya macho yake, mwamuzi huyo
aliamuru ipigwe kona huku akijificha nyuma ya wachezaji kwa kuikimbia camera huku akiona haya.


lakini hatujui mwamuzi huyu wa mechi hii ya pili ya klabu bingwa barani europa
aliahidiwa nini pale walipokwenda vyumbani half time,
bali kipindi cha pili tulikuja kuona mwendelezo wa yale yaliyosemwa
na baadhi ya makocha kuwa marefa wana Agenda ya kulinda kitumbua cha Benitez
na ndio maana wamekuwa wakiwabeba liverpool katika kila mechi barani europa.


wakiwa 2-2 na matokeo hayo ambayo yangepelekea liverpool kuaga mashindano
refa anakumbuka kile alichoahidiwa walipokuwa vyumbani
na kuwapa liverpool penati ambayo kama refa
angekuwa Pieluigi Corrina basi Ryan Babel angezawadiwa kadi ya njano
na faulo ingepigwa kuelekea golini kwa liverpool.
ni dhahiri kuwa Babel hakufanyiwa madhambi, la alikwishaona
kuwa mpira ule hawezi kuufikia na kufanya anachotaka
kutokana na William Gallas kuwahi kuufikia mpira ule
na badala yake akajiangusha na kumpa mwanya
refa kutimiza andiko.


wengi tunajua liverpool walikopitia msimu huu
kwani mpaka wanamaliza roundi ya kwanza walikuwa na point 1 tu
hivyo basi kama mambo yatakuwa yakiendelea hivi
basi liverpool atachukua ubingwa wa ulaya kila msimu.


vyombo vya habari kadhaa hapa europa viliwahi kushinikiza
kuwa marefa wapimwe akili, kabla ya mechi
na pia wachunguzwe kama wanakuwa wamelewa au la.
na kwa shinikizo hilo naungana na wanahabari hao
walioona mbali kwani matukio ya kizembe na ya makusudi
toka kwa marefa yanazidi kushamiri na kupelekea
kupunguza radha ya soka barani humu.
arsenal wamewahi kuwafunga mabingwa mara 9
real madrid nyumbani kwao el' santiago bernabeu
lakini walivyofika fainali na barcelona refa aliharibu
mpira katika dakika ya 18.
na msimu huu arsenal wamewafunga mabingwa mara 7
na mabingwa wa dunia kwa sasa AC milan
katika dimba ambalo hakuna
timu ya kiingereza imewahi kupata ushindi
la sansiro.
na matokeo yake tumeona jinsi refa alivyowaua
katika mechi ya liverpool.
hivyo ni wazi kabisa marefa hawana nia nzuri na arsenal.


shukrani za pekee ziwafikie marefa waliokuwa na akili timamu
mr Pieluiggi Corrina, mr Nilsen, na mr Andreas Frinks popote pale mlipo
wapenzi wa soka la uwanjani tunawakumbuka sana kwa maamuzi yyenu imara
na yasiyo na upendeleo na tunawaomba
mrudi kwa sababu soka la ulaya linaharibiwa na marefa wabovu
waliostaafishwa kwa uzembe huko walikokuwa wakifanyia kazi
na sasa wameamua kujiunga na urefa.
 
Duu Mkuu gang Chomba, pole sana. Utapaswa kutambua kwamba Arsenal haiwezi Liverpool. Kwani ni mara yenu ya kwanza kufungwa na Liva? lini mmewafunga Liverpool! Nadhani muihurumie Chelsea sasa kwani nayo itakwatuliwa hivyo hivyo. Karibuni Old Traford Jumamosi.
 
Back
Top Bottom