TAKWIMU ZA MECHI KATI YA AC MILAN NA ARSENAL.
tokea nizaliwe sijapata kuona mpira ambao kwa namna moja au nyingine mwenyezi mungu akinipa mtoto basi ni lazma nije nimuadisie.
mpira ulikuwa nikati ya vijana na wazee ambao wamekuwa wakiogopewa na vilabu vingi barani europa na dunia kwa ujumla.
nimeshuhudia vipaji vya hali ya juu toka kwa timu zote mbili, na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja na timu zote kwa ujumla.
pia katika pambano hili nimemsifu refa ambaye ameonyesha ukomavu wa hali ya juu na ni refa aliyejuwa kuwa dunia nzima mpaka mbinguni watu wanaitazama mechi hii, hivyo hakuwa na maamuzi ya kipuuzi kama ya yule refa aliyeiharibu mechi ya fainali ya champions ligi kati ya arsenal na barcelona mechi ambayo wataalamu na wachambuzi wa maswala ya soka wameweka wazi kuwa mechi ile iliisha katika dakika ya 18 ya kipindi cha kwanza pale refa ambaye uwezo wake ni wa kuchezesha mechi ya abajalo na sinza star alipotoa maamuzi ya kipuuzi yaliyoharibu radha ya mechi na kufanya mechi iwe ya upande mmoja.
awali ya yote ntakuwa si mwenye busara kama sintamsifu refa huyu aliyeshika kipyenga kati ya wazee milan na vijana arsenal.
FIRST HALF.
mechi ilianza na milan walionekana kana kwamba wanataka kupata kitu ambacho kitawalinda na kuwafanya vijana wa arsenal wanyong'onyee na kupoteza mwelekeo.
lakini haikuwa hivyo kwani katika dakika za mwanzoni tu za kipindi kwa kwanza arsenal walionekana nao kuto kubaki nyuma na kupeleka mashambulizi langoni mwa wazee milan, kitu kilichowafanya waondokane na hali ya woga na kuanza kujenga kujiamini kuwa nao wanaweza.
UNTOUCHABLE UNSTOUPABLE ARSENAL.
ni wazi kuwa mabeki wa milan wamepata tabu kutokana na kushindwa kutambua wamkabe nani na wamwache nani.
Diaby, Hleb, Adebayol, Eboue, Flamini na man of the Match Cesc Fabregas ndio waliohusika haswa kutia pilipili machoni kwa milan. ama kwa hakika wachezaji hawa ndio waliotimiza maandiko ya biblia yanayosema "MZEE ATAPELEKWA ASIPOTAKA".
MILAN NA UKUTA WA CHUMA.
hakuna ubishi kuwa simba hazeeheki meno.
milan wana ukuta imara na usiopenyeka kirahisi.
wanao uwezo wa kucheza mipira ya kichwa, wanao uwezo wa kuzuia pasi za chini za adui, wana mabeki wa pembeni wenye uwezo wa kupanda na kupiga krosi na kurudi kuzuia, na pia wana mabeki wa kati wenye mbio na mbinu za kuwazuia washambuliaji.
kitu hiki ndicho kilichopelekea mechi kuwa ngumu na yenye msisimko.
FABREGAS ANAGONGESHA MWAMBA.
hii ilikuwa ni katika kipindi ambacho kama refa angekuwa ni trafiki basi tunaweza kusema ameruhusu magari ya upande mmoja na kuzuia mengine, kwani kilikuwa ni kipindi ambacho "msako ulifanyika haswa golini kwa milan".
kuanzia dakika ya 25 milan walikimbizwa sana na kupelekea baadhi ya mabeki wao wazee kuanza kuinama na kujishika vichomi.
man of the match Fabregas alipiga mashine (shuti) ambalo liligonga mwamba na kutaka kupeleka msiba mapema kwa milan al maarufu kama (rosonelli) na hii ilikuwa ni salam tu.
si hilo tu kwani vijana wa arsenal waliendeleza msako wa kila upande na kufanya baadhi ya washabiki wa milan kuanza kuvua jezi zao ili wasijulikane wapo upande upi.
HALF TIME NA UKAGUZI WA ANCELLOTTI.
kocha wa milan amekiri kuwa alisimama mlango wa kuelekea vyumba vya mapumziko na kuanza kuwahesabu wachezaji wa arsenal ambao yeye binafsi alikuwa anawaona kama vile wapo 17 uwanjani.
lakini mwisho wa yote alikuja gundua kuwa arsenal wako 11 kama walivyo wazee wenzake milan.
SECOND HALF.
hiki naweza kusema ndo kipindi kitamu katika mechi hii.
ni kipindi tulichoshuhudia magoli maridhawa ambayo hakuna mchezaji yeyote wa milan aliyediriki kumkimbilia refa ili kubisha.
na pia ndo kipindi tulichoshuhudia mchezaji bora wa dunia Ricardo Kaka' akipewa kadi ya njano kwa kuonyesha wazi kuwa amezidiwa mbinu na amechanganyikiwa.
MILAN WANAAMKA.
moja kati ya vitu tulivyotaraji kuviona mapema katika mechi hii ni milan kutawala kiungo.
hii inatokana na milan kuwa na viungo wanaoheshimika na wenye ujuzi na uzoefu wa hali ya juu.
Ambrosini, Pirlo, Ivan Genarro Gatusso na Ricardo Kaka' ni viungo wanaoelewana sana na wenye uwezo wa hali ya juu, kiasi kwamba mara nyingi wamekuwa wakitawala kiungo katika mechi nyingi.
wanajua kukaba, kutoa pasi za mwisho nabaadhi yao wanajua kuendesha timu ipasavyo.
na mwanzo wa kipindi hiki cha pili ni kuwa milan walionyesha kweli pale ni uwanjani kwao na si kwa vijana wa arsenal.
milan walionekana kupanga mashambulizi mazuri lakini mwisho wa yote yalikuwa ni mashambiulizi yaliyoishia kwa mabeki imara wa arsenal Sanderous, Clichy, Sagna chini ya captain "nguli" William Gallas.
na katika muda huu ni wazi kuwa kama arsenal wangerudi nyuma basi wangewapa fursa wazee hawa wa milan kutawala mchezo nakupelekea kuanza kupanga mipango yao ya ushindi na hata kuifanikisha.
USIPOUANIKA UTAUTWANGA MBICHI.
kama milan wangekuwa wanamahusiano na msemo huu basi wangejitahidi zaidi katika kipindi hiki na kutumia uzoefu walionao kuweza "kuepuka kufika karivali"
lakini kadri muda ulivyozidi kwenda wenyeji milan walionekana kana kwamba walikuwa wameshinda mechi yao ya kwanza wiki mbili zilizopita katika uwanja wa kisasa wa Emirates lakini la hasha.
TALLENTED VS EXPERIENCE.
kadri giza linapozidi kuwa nene ujue alfajiri inakaribia, milan mara kadhaa walikuwa hatari katika lango la arsenal, na mara kadhaa walipata kona zilizotaka kubadili hali ya hewa lakini uimara wa golikipa Manuel Almunia ulizidi kuwapa ubishi arsenal.
ni wazi experience ya milan ilionekana kupungukiwa na mbinu kiasi kwamba walishindwa hata kuelekezana wapi kuna mapungufu, na hii ilipelekea vijana wenye tallent wa arsenal kuonekana kama vile wapo nyumbani kwao.
KWA NINI HAKUKUWA NA MASHUKA MAKUBWA YANAYOWATUKUZA WAKINA KAKA'?
mmiliki wa timu Silvio Bellusconi pamoja na swahiba wake asiyekaukwa na maneno ya kujisifu bwana Adriano Galliani haijulikani ni kwa nini hawakuwepo uwanjani.
ila utamaduni wa washabiki wa milan ni kushika mashuka makubwa uwanjani yenye maneno yanayowatukuza wachezaji wao kama vile (siempre Nesta) (pena inzaghi) (sforza maldini) (gilamania) (galacticous fantasticous kaka') lakini ni wazi kuwa hakukuonekana kitambaa chenye udogo sawa na leso chenye kuisifu milan, je ni kwa nini?
akili kichwani mwako.
MATESO YAKIZIDI JUWA WOKOVU UNAKARIBIA.
katika dalika za 70-80 milan walifanya mashambulizi mengi kiasi wanaojua hadithi za wazee hawa walianza kukaa sawa wakitaraji muda wowote mambo kuiva na mara kadhaa yalikuwa ni mateso makubwa kwa washabiki wa arsenal.
lakini kama nilivyosema hapo awali mashambulizi ya milan mara zote yaliishia kwa wachezaji wa arsenal.
FLAMINI NI ZAIDI YA GATTUSO.
flamini mara kadhaa amekuwa akimnyang'anya mipira kiungo tegemeo wa milan kaka', lakini gattuso mara zote alipomfuata fabregas alipata aibu.
na hii iko wazi hata ukienda kumuuliza gattuso akiwa peke yake atakudhihirishia hilo.
ITALIAN JOB.
kuanzia dakika ya 80 arsenal sasa walionyesha kuamka na kuudhihirishia ulimwengu nini kimewapeleka italy, na wao walianza kujibu mashambulizi kuelekea golini mwa milan na kuanzia hapa sasa ndipo mambo yalipoanza kuwachachia mambingwa hawa watetezi.
THE CIRCLE IS COMPLETE.
man of the match cesc fabregas akiwa anakabwa na kiungo mwenye bugudha gennaro gattuso anapiga shuti maridhawa linalompita kipa mrefu kiumbo na kiumri na kutinga katika nyavu za uwanja uliozungukwa na nyavu za kuwazuia wahuni wa sansiro wenye uwezo wa kubeba watazamaji takriban 90 elfu.
na hii ilimaanisha ili mabingwa hawa watetezi wafuzu hatua ya robo fainali basi ni lazima wafunge magoli mawili.
swali ni je wangeweza kupenya ngome imara ya arsenal na kufunga magoli hayo?
MGONJWA ATAKA KUTEMA DAWA.
hapa wazee waliamka na kutapatapa tena na kuanza mashambulizi yao ambayo ili yawarudishe mashabiki wao ambao walishaanza kutoka uwanjani ilikuwa ni lazima washinde magoli mawili.
lakini kwa hali ilivyokuwa sizani kama kuna mtu alifikiria kuwa hilo lingewezekana.
na kuanzia muda huu sikumuona tena bingwa wa mbinu Carlo Ancelotti na sina taarifa zake zozote.
DOCTOR ANAKUFA, MGONJWA ANABAKI.
adebayol yule anayepondwa na mashabiki wenzetu kuwa hana lolote la ajabu anawadhihirishia mahasidi kuwa yeye hakununuliwa kimakosa na ndiye anayeandika bao la pili linalowauwa mabingwa mara 7 na goli hilo linawalazimu milan wafunge magoli matatu ili wafuzu.
kwa kifupi katika mechi hii hata kipa angekaa Sanderos basi arsenal wasingefungwa.
FULL TIME.
refa anamaliza mechi iliyokuwa na mikiki na kiwango cha hadhi ya nyota 5 na kupelekea arsenal wafanye kile walichoshindwa timu zoote za uingereza toka karne ya 19.
KINYWA CHA MTU MZIMA KINANUKA ILA MANENO YAKE HAYANUKI.
baada ya mechi kocha wa arsenal mfaransa Arsene' Wenger amesema kuwa alichokifanya sansiro ni salam kwa timu yoyote ambayo itakutana na arsenal katika kombe hili.
na ameweka wazi kuwa timu atakayopangwa nayo robo fainali "itachambia upawa badala ya kopo".
MUHIMU:
1) arsenal wamewafungwa na kuwatoa mabingwa watetezi wa klabu bingwa barani ulaya.
2) arsenal wamewafunga mabingwa wa dunia.
3) arsenal wamevunja mwiko wa milan kutofungwa kwao na klabu za uingereza.
4) arsenal ndio timu inayocheza soka ambalo inasemekana linachezwa mbinguni.
5) arsenal imeifunga timu yenye wachezaji wenye umri mkubwa barani ulaya.
VISINGIZIO LUKUKI.
wengi wa wasiojua soka watauponda ushindi huu wakijitetea kuwa milan wamemkosa Dida na Serdolf.
ila wakumbuke pia arsenal wamewakosa Toure, Rosicky na kamanda Robin van Persie.
uchambuzi huu umeandikwa
na shabiki mwenye kadi
Gang Chomba
.....................