Arusha: Afisa Upelelezi (Omary Mahita) akamatwa kwa tuhuma za kumvunja Mguu raia

Arusha: Afisa Upelelezi (Omary Mahita) akamatwa kwa tuhuma za kumvunja Mguu raia

Yaani polisi kama taasisi wamekuwa hawaaminiki hadi kila mtu ana comment negative walahi dah!

Badala watu ku sifia hatua ya jeshi kumkamata ofisa wake kwa hilo kosa watu wote wana dauti uhalisia wa habari yenyewe.

Polisi mna la kujifunza sana yaani
Na wewe umeamini hilo mkuu?

Unafikiri huyo atalala lupango kama ambavyo ugelala wewe?
 
Yaani polisi kama taasisi wamekuwa hawaaminiki hadi kila mtu ana comment negative walahi dah!

Badala watu ku sifia hatua ya jeshi kumkamata ofisa wake kwa hilo kosa watu wote wana dauti uhalisia wa habari yenyewe.

Polisi mna la kujifunza sana yaani
Ndugu yako akikamatwa na Polisi na kurudi salama ni kushukuru Mungu.
Hawa watu sijui wanalishwa roho gani.
 
Afisa Upelelezi Wilaya ya Arusha Mjini, Omary Mahita anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumpiga hadi kumvunja mguu mtuhumiwa wakati wa mahojiano akiwa kituo cha polisi.

Askari huyo anatuhumiwa kumvunja mguu wa kushoto Peter Charles (21), mkazi wa Daraja II, jijini Arusha Juni 6, 2024.

Akizungumzia tukio hilo leo Alhamisi Agosti 15, 2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amesema wanamshikilia ofisa huyo wa polsi na kwamba uchunguzi umeshaanza na endapo atabainika kuwa na kosa, atachukuliwa hatua za kisheria.

"Ni kweli hilo tukio liko ofisini kwangu na tumeanza uchunguzi tangu Agosti 8, 2024 nilipopata taarifa kwa simu kutoka kwa ndugu wa huyo kijana akimtuhumu askari wangu kumpiga hadi kumvunja mguu,” amesema Masejo alipozungumza na Mwananchi.

Mwananchi
Bado ni afisa! Alitakiwa avuliwe cheo na asimamishwe kazi mpaka tuhuma zake zitakapokwisha.
 
😆😆😆
Screenshot_20240815-201804_Chrome.jpg
 
"Ni kweli hilo tukio liko ofisini kwangu na tumeanza uchunguzi tangu Agosti 8, 2024 nilipopata taarifa kwa simu kutoka kwa ndugu wa huyo kijana akimtuhumu askari wangu kumpiga hadi kumvunja mguu,” amesema Masejo alipozungumza na Mwananchi.

Mwananchi
Hii ya tuna fanya uchunguzi!!! tunafanya uchunguzi.!!
Ni ishara ya watu wenye utamaduni wa kutojiamini kwenye kufanya maamuzi.
Au ni namna ya kuhalalisha uovu uonekane halali, kwa kutuoa majibu ya uchunguzi miaka 3 ijayo.
wakati huo muathirika amekata tamaa ya kufuatilia madai yake.

Iko siku kutakua na ulazima wa kuunda tume ya kufuatilia uchunguzi unao chunguzwa.
 
Back
Top Bottom