Arusha: Aliyekuwa Mgombea wa Ujumbe katika Serikali ya Mtaa akutwa kwake akiwa amefariki huku akiwa na alama kukatwa shingoni

"inawezekana pia amejidhuru mwenyewe kutokana na labda msongo wa mawazo” amesema Shana.

kamanda anapiga ramli kama mganga wa kienyeji
Kwajibu hilo la Kamanda ujue hakuna uchunguzi utakaofanyika hapo, zuga na gheresha mpaka watu wasahau. Ndio basi tena. Poleni sana kwa waliofikwa na Msiba.
 
Tunalazimishwa kuelekea tusipohitaji kufika. Inna lillah wa inna ilahi rajiun
 
Lisu hayupo hajaenda kufungua kesi kwa hiyo polisi haiwezi kufanya uchunguzi na huyo marehemu hayupo hawezi kufungua kesi kwa hiyo uchunguzi haupo vile vile. Polisi wataanzia wapi wakati marehemu hajafungua kesi kama Tundu Lisu?
 
vijana wadogo mnatafuta umaarufu kupitia siasa kama vile hamjui kua siasa ni.mchezo mchafu! hivi hakuna issue nyingine za kufanya??
Nyerere alianza siasa akiwa kijana mdogo kabisa na akafanya makubwa. Usiwakatishe tamaa vijana, cha msingi siasa ya nchi hii irudi kwenye misingi ya ustaarabu kuliko hii ya kuchinjana.
Rais wa nchi asiposimama kinyume na mauaji haya ya watanzania wasio na hatia nchi itapata laana na kuingia kwenye machafuko. JPM tafadhali kemea haya mauaji ya kisiasa hadharani nchi iweze kupona.
Rais Magufuli yafaa nini kupokea gawio kutoka katika mashirika ya umma ili hali walipa kodi na nguvu kazi ya taifa ndo hawa wanauawa? Kodi itakayoleta gawio mwakani itapakanaje kama walipa kodi wanapunguzwa kwa mapenzi ya wanadamu wachache?
 
Haya majibu ya RPC ni ya kijinga sana sana! Eti huenda MTU amejidhuru kutokana na msongo.....pumbavu kweli
 
vijana wadogo mnatafuta umaarufu kupitia siasa kama vile hamjui kua siasa ni.mchezo mchafu! hivi hakuna issue nyingine za kufanya??
Kwani wakina Salim a. Salim, kikwete etc walingia kwenye siasa wakiwa wazee

Ova
 
ACP aache visingizio na vitisho, kuwepo funguo ndani si hoja ya msingi. Yeye mwenyewe anadhani inawezekana amejidhuru mwenyewe labda kutokana na msongo wa mawazo. Sasa ikitokea mtu mwingine akadhani kuna walio mdhuru kwa sababu za kisiasa ama nyinginezo, uchochezi unatokea wapi hapo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…