Arusha, amuua kaka yake kwa kisu baba yake akishuhudia

Arusha, amuua kaka yake kwa kisu baba yake akishuhudia

Kijana James mwenye umri wa miaka 16 anatuhumiwa kumuua kaka yake anaitwa Zakayo huku baba mzazi akikiri kushindwa kuwaamua ndugu hao wawili waliokuwa wakigombana kisa mifugo.

Mimi naitwa Paulo Sindio, ni baba mzazi wa watoto hao, walianza kugombana mbele yangu kisa kikiwa ni uswagaji wa mifugo kurudi porini, wote ni Watoto wangu wa mama mmoja.

Akielezea tukio hilo, Paulo amesema: “Walikorofishana baada ya mkubwa kumwambia mdogo kuwa anatakiwa kwenda kuswaga mifugo kauli ambayo ilipingwa na James na baada ya muda wakaanza kupigana.

“Walipigana, mimi nikanyanyuka kwa ajili ya kwenda kuwaamua, kumbe mwenzake tayari alikuwa ameshamchoma kisu kwenye moyo, tulivyompeleka hospitali ikakutwa ameshafariki.

“Sina la kusema, wazee wa ukoo wapo wataamua wenyewe, sina la kufanya, na sijui alipo, kama ameenda kujiua au la sijui alipo. Polisi tayari wana taarifa na wanalifuatilia.”


Source: Globaltv
This is sad
 
Uache uongo!

Usikute kesi yenyewe ikawa "manslaughter" na ukizingatia ni mtoto, hakuna hukumu.

Kama hujui Criminal Laws just be quiet. Tukuelimishe!
Unaweza kaa mahabusu miaka hadi 3 na ukafungwa gerezan hadi miaka 5 piga hesabu hapo
 
Unapoambiwa zama za mwisho dont think of 10 - 20 years to come. Kwa sasa unaona jambo la uzinzi na wanawake kutembea uchi lilivyo? Bas jua ni bado sana itafika wakati uzinzi utakua unafanyika barabarani na wanawake watatembea uchi kabisa na hapo ndo hasira ya mungu itashuka
Uchi wa mnyama au vimini, au ulienda beach, sema usodoma na ushoga vimetia fola
 
Ila hii nchi bana
Yan haya mauaji kuna watu wanalaumu serikali [emoji23][emoji23]
Sasa sijui jukumu letu kama jamii kwenye hii nchi ni ipi
Ilo tu?hata swala la matengezo ya umeme wana laumu.
 
Hii roho ya mauaji Mungu atunusuru nayo

Shetani ameamua kututumia na atutumie tena
Roho ya mauaji muasisi wake ni baba yenu jiwe, aliunda kikosi cha wasiojulikana na kurasimisha mauaji ya wananchi. Mwenyezi Mungu atajua namna ya KUSHUGHULIKA naye huko aliko.
Tuombe sana na kufuata mapenzi ya Mungu ili kuishinda roho ya mauti inayotembea kwa kasi sana ili kushindana na roho ya uhai roho ya Mungu. Yaani kuzimu imefungua mdomo kumeza... tuombeane rehema za mungu

Ufunuo 6:4
"Akatoka farasi mwingine, mwekundu sana, na yeye aliyempanda alipewa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa."
 
haiwezekani kabisa Mimi niswage huku unauza ng'ombe na ukiuza unakula na wanao baba ukiambiwa eti mkubwa ,mkubwa kwake na familia yake .........una umri miaka 45 au 47 bado unatamani kupigana na mtu miaka 20 na huna mazoezi yakutosha !

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Taifa limemuacha Mungu limegeukia Uchifu...
kutoka kupiga goti kanisani, kanzu msikitini mpaka ngozi za chui...
Mambo ya Mizimu na makafara...
Kifupi tunavuna tulichopanda na tujiandae kwa Mengi zaidi....
Maandiko yanasem kila wana wa izrael walipoanza kuabudi sanamu Mungu aliwaacha wakapokea kichapo na kuchukuliwa utumwani ila kila walipomlilia aliwasikia akawanusuru.
 
Hivi huwa hawakazii sana kuwa ukiuwa ni dhambi kubwa sana?
Huko huwa kwenye kuabudu huwa mnaenda kujifunza nini?

Mbona mauwaji yametamalaki hivyo?

Mjitafakari sana huu sio mda wa kuulizana kwanini yanatokea haya bali mumrudie Mungu sana na muogope sana dhambi period
Hao ukute hata dini hawajui
 
Mauwaji ya Arusha yananikumbusha yale ya mwishini mwa December, 2021 ambapo mama Jane Rose Dewasi aliuwawa pale Njiro Arusha. Hadi sasa ndugu wa marehemu wanataka kujua polisi wamefikia wapi kuhusu upelelezi kwa kuwa serikali ya mtaa haijui lolote na haijapata mrejesho toka polisi.
 
Ifike mahali raisi samia aanzishe wizara ya Mauaji

This is too much[emoji3525]
 
Roho ya mauaji muasisi wake ni baba yenu jiwe, aliunda kikosi cha wasiojulikana na kurasimisha mauaji ya wananchi. Mwenyezi Mungu atajua namna ya KUSHUGHULIKA naye huko aliko.

Unatia huruma sana. Pole mwaya😂
 
Unatia huruma sana. Pole mwaya😂
Familia ya Ben Saanane, Azory Gwanda na wengineo waliopotezwa na mwendazake wanakushangaa sana kwa kicheko chako rafiki.
 
Back
Top Bottom