ARUSHA: Askari Polisi 7 waliombambikia pembe za ndovu Prof. Justin Maeda na kuchukua milioni 100 wafukuzwa kazi, Profesa afunguka

ARUSHA: Askari Polisi 7 waliombambikia pembe za ndovu Prof. Justin Maeda na kuchukua milioni 100 wafukuzwa kazi, Profesa afunguka

View attachment 1821643

Kati ya watu 9 walioshiriki uharamia huu, watatu ni mabaunsa wa Sabaya na wengine ni askari polisi wa kituo cha USA River. Huyu ni Profesa Justine Maeda, amekua Mhadhiri wa chuo kikuu cha UDSM kwa miaka mingi, baadae akateuliwa kuwa mshauri wa Rais Nyerere, na baadae akawa Mkurugenzi wa UNICEF nchini Zimbabwe hadi alipostaafu...
Diktetea alikuwa anafuga majambazi sn
 
Malisa ni masikini ambae anahisi umasikini wake umesababishwa na Sabaya

Sabaya ni Jambazi ,alitaka kumuua Malisa GJ.....Jambazi alitoki tena kuna kesi 7 mafaili yanaandaliwa aingizwe kwenye 18 bado za ubakaji sema hizi za ubakaji hazina ushahidi wa moja kwa moja labda watumie busara ya kuwasikiliza wabakaji na kuyafanyia kazi malalamiko yao maana waliobakwa ni zaidi ya mademu 44.
 
View attachment 1821643

Kati ya watu 9 walioshiriki uharamia huu, watatu ni mabaunsa wa Sabaya na wengine ni askari polisi wa kituo cha USA River. Huyu ni Profesa Justine Maeda, amekua Mhadhiri wa chuo kikuu cha UDSM kwa miaka mingi, baadae akateuliwa kuwa mshauri wa Rais Nyerere, na baadae akawa Mkurugenzi wa UNICEF nchini Zimbabwe hadi alipostaafu...
Viongozi wote wa ccm waliokuwepo pamoja na Magufuli makao makuu wakamatwe
 
Kwa maovu ya Sabaya ni hakika alikuwa analindwa Sana na Baba take. Babaha wezi kupanda maharage avune mahindi. Hayo ndiyo maharage yake. Chomwa milele.
Siyo kwamba alikuwa analindwa Ila aliujua udhaifu wa boss wake ni kugombana na wapinzani na kumsifia boss kinafiki na boss anafarikika na kutulia na yeye anatenda mambo yake bila buguza, ukiwa kiongozi wa kitu chochote unatakiwa uwakemee wale wanaokusifiasifia maana badala ya kusifiwa wanatakiwa wakuonyeshe wanafanya nini kulingana na kazi ulizowapangia Ili isiwe ngumu kwako kuongoza hata uchaguzi nguvu kubwa ilitumika kujinadi kwasababu ya watu kama Sabaya.
 
Dogo anakwenda kufia jela....sioni namna ya kuchomoka kwenye hizi tuhuma nzito namna hii... huu ni Ujambazi kabisa.
 
OCD na OC CID
Askari Polisi saba wakiwemo watano wa kituo cha Polisi Usa Wilayani Arumeru Mkoani Arusha na wawili wa Kituo Kikuu cha Polisi Arusha wamefukuzwa kazi kwa fedheha kwa kosa la kushawishi na kuomba rushwa ya shilingi milioni 100...
OCD na OC CID wa kituo Cha polisi USA river Arusha,walihusika 100%, tunaomba wasimamishwe kazi kupisha uchunguzi.
 
View attachment 1821643

Kati ya watu 9 walioshiriki uharamia huu, watatu ni mabaunsa wa Sabaya na wengine ni askari polisi wa kituo cha USA River. Huyu ni Profesa Justine Maeda, amekua Mhadhiri wa chuo kikuu cha UDSM kwa miaka mingi, baadae akateuliwa kuwa mshauri wa Rais Nyerere, na baadae akawa Mkurugenzi wa UNICEF nchini Zimbabwe hadi alipostaafu.

Sabaya akishirikiana na askari polisi wa kituo cha USA River, walichukua vipande viwili vya mhogo wakavikausha vizuri, wakavipiga msasa na kuving'arisha kwa polish. Kisha wakaingia shambani Profesa huyu na kuviweka kwenye mzinga wa nyuki bila yeye kujua.

Baada ya siku chache wakamfuata na kumtuhumu kwamba anamiliki nyara za serikali ambazo ni pembe za ndovu. Profesa akasema hajawahi hata kuona hizo pembe zinafananaje. Akawaruhusu wapekue nyumba, lakini hawakua na interest ya nyumba, wakaenda moja kwa moja shambani kwenye mizinga ya nyuki na kutoa vipande viwili walivyodai ni pembe za ndovu (kumbe ni mihogo wamepaka polish).

Wakamwambia mzee hii ni kesi ya uhujumu uchumi kwa hiyo ili asipelekwe mahakamani awape TZS 200M. Akasema hana kiasi hicho cha fedha, baada ya kujadiliana wakataka 100M. Mzee wa watu kwa kuogopa kufia jela akaenda bank na kukomba akiba yake yote na kuwapa.

Hivi ndivyo "jambazi" Sabaya alivyotumia mamlala yake vibaya kwa kulindwa na nguvu kutoka juu. Mtu anatoka Hai anaenda kufanya uhalifu mkoa mwingine lakini hachukuliwi hatua yoyote. Juzi nilipoweka orodha ya hoteli alizolala Arusha bila kulipa, nikaambiwa Mwanza, Dodoma, Moshi, Dar, Tanga kote huko amewahi kulala na kugoma kulipa bill ya mamilioni ya shilingi.

Ni aibu sana kwamba kati ya watanzania milioni 60, huyu "jambazi" alionekana anafaa

Credi Malisa GJ

My Take
Mnaomtetea Sabaya fikirieni kipimwa akili
.
 
Askari Polisi saba wakiwemo watano wa kituo cha Polisi Usa Wilayani Arumeru Mkoani Arusha na wawili wa Kituo Kikuu cha Polisi Arusha wamefukuzwa kazi kwa fedheha kwa kosa la kushawishi na kuomba rushwa ya shilingi milioni 100.

Wiki iliyopita Kamanda wa TAASISI ya Kuzuia na kupambana na Rushwa Nchini {TAKUKURU}Mkoani Arusha,James Ruge alikiri kuwakamata askari hao kushawishi na kupokea kiasi hicho Cha fedha ili wasimfungulie Kesi ya uhujumu uchumi ambapo angefia gerezani.

Hata hivyo Ruge alisema uchunguzi wa kesi hiyo bado haujakamilika na ukikamilika atatoa taarifa kwa vyombo vya Habari juu ya makasa mzima.

Vyanzo vya Habari vilisema kuwa mienendo ya mashtaka ya kijeshi ya kipolisi ilifanyika katika tarehe Aprill 22,23,24 na tarehe 25 mwaka huu , ambapo Askari hao walifukuzwa kazi rasmi ndani ya jeshi la polisi na sasa wanasubiri kushitakiwa katika Mahakama za kiraia wakati wowote.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Justin Masejo alipoulizwa juu ya jeshi hilo kuchukua hatua hizo alisema kuwa hayo ni mambo ya ndani ya Polisi na sio rahisi kutolewa hadharani kwani ni kinyume na maadili ya kazi.

Naye mhanga wa tukio hilo ambaye ni mfanyabiashara wa mji wa Usariver,Profesa Justin Maeda{77}akizungumza nyumbani kwake katika Kijiji cha Nshuku kata ya Nkoaranga wilayani Arumeru alisema pamoja na mkasa wote alioupata na kuishukuru Polisi kwa hatua walizochukua ila amesikitishwa na kitendo cha polisi hao kukiuka maadili ya kazi na kuomba rushwa katika kituo cha Polisi Usa hatua ambayo ilimshangaa na kushindwa kujua OCD na OC CID washindwe kujua tukio hilo.

Profesa Maeda ambaye alianza kufundisha UDSM Mwaka 1970 na kuwafundisha viongozi wengi wa serikali kabla ya kuwa Mshauri Mkuu wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1981-1985 Ikulu sasa ameanza kuamini maneno ya watu wa Usa kuwa ndani ya kituo cha polisi Usa kinanuka rushwa na kuna askari wa kituo hicho kitendo cha upelelezo ni miungu mtu kwani wako hapo kwa miaka mingi sasa wamejivika ufalme wa kuomba kiasi chochote cha rushwa ndani ya kituo mhicho bila kuogopa chochote.

Alisema kama yeye amebambikiwa kesi ya nyaraka za serikali na kuchomekewa shambani kwake na kutakiwa kutoa rushwa ya shilingi milioni 200 kabla ya kufikia makubaliano ya shilingi milioni 100 kuna raia gani Arumeru wameshafanyiwa unyama wa aina hiyo kwani hiyo ni hatari na viongozi wakuu wa polisi Mkoani Arusha na Makao makuu wanapaswa kutupia macho zaidi kituo hicho maana dhuruma na uhuni umekithiri kupita kiasi hivyo hatua zinapaswa kuchukuliwa sasa.

Profesa Maenda ambaye ana Mke na Watoto watatu ambao wote wako nje ya nchi alisema polisi hao ambao walikuja nyumbani kwake na gari mbili za polisi marchi 19 mwaka huu majira ya kati ya saa 7 mchana na saa 8 wakiwa wamejaa kwenye gari na wakiwa na silaha na gari ndogo aina ya Rv4 ambayo hakufanikiwa kushika namba walijitambulisha kuwa ni polisi ya Us ana makao makuu na alimtambua mmoja{jina tunahifadhi} wameagizwa kwenda kwake kupekua kwa kuwa wanataarifa za kiitelejesia kuwa anafanya biashara ya nyara za serikali ikiwemo meno ya tembo na Ngozi za chui.

Alisema kwa kuwa hajawai na hajui kitu kinaitwa Nyara za serikali na hajawahi kufanya biashara hiyo aliwaruhusu kufanya upekuzi lakini cha kushangza hawakufanya ndani ya nyumba bali walikuwa wakipita nje ya kwenda moja kwa moja shambani kwenye mizinga ya nyuki.

Profesa ambaye ameshafanya kazi UN hususani UNICEF nchi mbali za kiafrika na kumalizia nchi ya Zimbabwe mwaka 2002 alion aaskari mmoja akichukua mzinga na kutoa ndani ya mzinga kitu alichodai ni meno ya tembo na kusema hicho ndio kitu walichokuwa wakikitafuta.

Alisema kuwa yeye alisema shambani kwake hukaa zaidi ya miezi miwili au mitatu kuingia hivyo aliwauliza askari hao hii imeletwa na nani kwani hajawahi kufanya biashara hiyo ila alijibiwa na askari hao kuwa hiyo imekula kwake kwani hii ni kesi ya uhujumu uchumi na angefungwa Maisha hivyo anatakiwa kuweka mambo sawa.

Mzee huyo ambaye isema alistaafu miaka ishirini iliyopita alilipwa kiinua mgongo chake{PENSHENI} cha kiasi cha shilingi milioni 74 na kuweka benki ya CRDB na NMB alichukuliwa hadi kituo cha polisi Us ana kuanza kuchukuliwa maelezo na kuombwa rushwa ya shilingi milioni 200 wakati akitoa maelezo.

Profesa alisema yeye aliwaambia kuwa jana yake yaani marchi 18 mwaka huu alikwenda benki na kuchukua kiasi kidogo cha pesa hivyo kiasi hicho hana na kuwataka wapokee milioni 100 na ndipo alipokwenda benki akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi na kuchukua shilingi milioni 74 na baadae alikwenda dukani kwa mdogo wake hapo Usariver na kuchukua kiasi cha shilingi milioni 30 na zote aliwapa polisi katika kituo cha Usa kwani rushwa ilifanyika hapo.

Alisema na kuiomba serikali iweze kumrudishia kiasi cha pesa yake kwani ni kiunua mgongo cha utumishi wake wa kazi wa miaka mingi kazi.

Mwisho



Kwa hakika mwendazake alikuwa kiongozi mzigo!
 
Ukute hawa nao ni mpango wa Sabaya kwa kushirikiana na mwendazake.
 
Sabaya anazidi kuaibika.
Wasiishie hapo na waliokuwa wakimpa silaha nao
 
Back
Top Bottom