Kati ya watu 9 walioshiriki uharamia huu, watatu ni mabaunsa wa Sabaya na wengine ni askari polisi wa kituo cha USA River. Huyu ni Profesa Justine Maeda, amekua Mhadhiri wa chuo kikuu cha UDSM kwa miaka mingi, baadae akateuliwa kuwa mshauri wa Rais Nyerere, na baadae akawa Mkurugenzi wa UNICEF nchini Zimbabwe hadi alipostaafu.
Sabaya akishirikiana na askari polisi wa kituo cha USA River, walichukua vipande viwili vya mhogo wakavikausha vizuri, wakavipiga msasa na kuving'arisha kwa polish. Kisha wakaingia shambani Profesa huyu na kuviweka kwenye mzinga wa nyuki bila yeye kujua.
Baada ya siku chache wakamfuata na kumtuhumu kwamba anamiliki nyara za serikali ambazo ni pembe za ndovu. Profesa akasema hajawahi hata kuona hizo pembe zinafananaje. Akawaruhusu wapekue nyumba, lakini hawakua na interest ya nyumba, wakaenda moja kwa moja shambani kwenye mizinga ya nyuki na kutoa vipande viwili walivyodai ni pembe za ndovu (kumbe ni mihogo wamepaka polish).
Wakamwambia mzee hii ni kesi ya uhujumu uchumi kwa hiyo ili asipelekwe mahakamani awape TZS 200M. Akasema hana kiasi hicho cha fedha, baada ya kujadiliana wakataka 100M. Mzee wa watu kwa kuogopa kufia jela akaenda bank na kukomba akiba yake yote na kuwapa.
Hivi ndivyo "jambazi" Sabaya alivyotumia mamlala yake vibaya kwa kulindwa na nguvu kutoka juu. Mtu anatoka Hai anaenda kufanya uhalifu mkoa mwingine lakini hachukuliwi hatua yoyote. Juzi nilipoweka orodha ya hoteli alizolala Arusha bila kulipa, nikaambiwa Mwanza, Dodoma, Moshi, Dar, Tanga kote huko amewahi kulala na kugoma kulipa bill ya mamilioni ya shilingi.
Ni aibu sana kwamba kati ya watanzania milioni 60, huyu "jambazi" alionekana anafaa
Credi Malisa GJ
My Take
Mnaomtetea Sabaya fikirieni kipimwa akili