MLUGURU
JF-Expert Member
- Mar 30, 2012
- 2,929
- 3,710
Naona Magu amekuacha na kijacho sasa umebaki kuweweseka tu.Magufuli ndo alilea huu ujinga sasa kama huna habari
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naona Magu amekuacha na kijacho sasa umebaki kuweweseka tu.Magufuli ndo alilea huu ujinga sasa kama huna habari
usipo ibiwa na mwizi itaibiwa na polisiHawa askari wa Kizazi hiki, ukiona una Mali na Majambazi yamekutinga ni bora Mara 100 kukimbilia Porini kuliko kujisalimisha kwao..,
Waliosimamishwa inamaanisha nn, maana kuna kufukuzwa na kusimamishwa hapo[emoji848][emoji848]Askari wanne wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha wamefukuzwa kazi na maofisa wawili wa jeshi hilo wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya Sh100 milioni.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo ametoa taarifa hiyo leo Alhamisi Aprili 29 ,2021 na kubainisha kuwa walipokea taarifa kuhusu askari hao Aprili 19, 2021 kwamba wameomba na kupokea rushwa na uchunguzi ukaanza.
"Baada ya uchunguzi jeshi limewafukuza kazi askari wanne na kuwasimamisha kazi maofisa wawili kwa kuwa haliwezi kuvumilia tuhuma hizi,” amesema.
Amebainisha kuwa baada ya uamuzi huo hatua nyingine za kisheria zinafanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Askari hao wanadaiwa kuomba rushwa kwa Profesa Justine Maeda ambaye amewahi kuwa mshauri wa uchumi wa rais wa awamu ya kwanza, Hayati Julius Nyerere.
Wanadaiwa kuomba fedha hizo na kupatiwa baada ya kumpekua nyumbani kwake na kudai kukuta vipande viwili vya meno ya tembo vikiwa kwenye mzinga wa nyuki.
Profesa Maeda ameieleza Mwananchi Digital kuwa alitoa fedha hizo ili ajinusuru asifunguliwe kesi ya uhujumu uchumi kama alivyoelezwa na polisi hao.
Chanzo: Mwananchi
nadhani vyeo vimewabeba hao waliosimamishwa. Kuna rank ukufikia huwez kufukuzwa kama hao wwngineWaliosimamishwa inamaanisha nn, maana kuna kufukuzwa na kusimamishwa hapo[emoji848][emoji848]
Nimekupata mkuu,nadhani vyeo vimewabeba hao waliosimamishwa. Kuna rank ukufikia huwez kufukuzwa kama hao wwngine
Namfaham sana mzee maeda nishafanya kibarua kwake. Yuko straight na mambo yake. Ni msomi na ana IQ kubwa (intelligent). Ni mpole lakini ana authority. Hapendi kujionyesha yeye ni billionaire. Ila wabongo kwa kuchunguza tuwakagundua ile kushindia mahindi ya kuchoma hadharani ni kuzuga watu tukajua nyumbani kwake ana special menu anaandaliwa na mpishi maalum. Kwenye shelves kumejaa jack danieles, coniaks, masmirnoff na whisky za ghali.
Kweli mkuu ila kuna kipindi nimezinguana nao nilikuwa na jamaa yangu yupo na manzi wake sasa jamaa huwa mzee wake ana store ya mazao maeneo ya Mbauda Arusha.
Siku hiyo jamaa kamwita manzi akaja mtaa na mimi huwa nampa company msela mda mwingi tupo wote mpaka leo hii. Basi siku hiyo akapigiwa simu ilikuwa usiku saa mbili kuwa kuna gari ina gunia kama kumi na mbili za maharage ila ji gari ya majani ya chai hivyo itafika si muda akagungue store mzigo ushushwe.
Tukatoka pale tulipokuwa na jamaa na manzi wake (sio mbali na store) kufika mara gari kweli ikaja mzigo ukashushwa chap na makuli wawili. Ile tumefunga tunataka kuondoka mara ikaja defender huku Arusha naonaga wanatumiaga za Sunny Safari sijui wanakodi au wanahongwa sijui.
Jamaa wakakomaa fungueni kuna mzigo wa magendo umeingizwa ndani. Hapo nilikuwa nishatupia kinywaji moja inatwa zanzi ipo kama amarula siku hizi hakipo vilikuwa vinawekwa kwenye kiroba.
Nikamwambia jamaa yangu usifungue. Halafu hao polisi nikawachana kuwa hatufungui mpaka mtupe search warrant. Jamaa wakakomaa pale nikawaambia tupelekeni mnapotaka hatufungi hapa bila search warrant.
Yule manzi akaanza kulia anaomba watusamehe akakatwa kofi akatulia [emoji23]. Wale askari wakaanza kusema "unajifanya unajua sasa twende pandeni kwenye gari" nikawaambia poa twendeni ila nikawaambia kabla ya hapo ngoja tutoe taarifa home kuwa tumekamatwa.
Jamaa akampigia mshua wake simu akamweleza mshua akasema poa anakuja central. Basi tukapanda kwenye pira manzi alikuwa wa kwanza kupanda akakalia seat zile kama bench nikamwambia akae chini maana jamaa wangemzingua (kama hujawahi pakiwa kwenye pira siku ukikamatwa ukipakiwa usikalie seat utapigwa kama mbwa koko, kaa kwenye floor ya body ya gari).
Basi jamaa wakatekenya ndinga wakaanza kuondoka tumetoka hata sio mbali kabla ya kuingia lami mijamaa ikaona hatulainiki ikatuachia tukasepa zetu.
Sometimes ukiwa na ujasiri na kujua sheria inasaidia. Ila angalia na watu wenyewe kuna askari wengine yupo radhi akuchape shaba ukimbishia.
Madhara ya kuwapeleka Depo watu wasio na maadili ndiyo haya sasa.
Tatizo kubwa ni njaa mkuu. Nadhani (sina uhakika) polisi ni moja ya makundi ya watumishi wanaolipwa mishahara midogo hapa TZ. Sasa kwakuwa wana mamlaka fulani ya kudeal na uhalifu ndio njia wanayotumia ili kupiga vi deal anagalau ku supplement mshahara kiduchu ili kujikimu.Sijui polisi wa bongo wanafundishwaga kumjaza kwanza mtu upepo kabla hawajamkandamiza au wanaambukizana tu hiyo tabia. Karibia polisi wote ukikutana nao kwenye tukio lazima wakupanikishe kwanza bila kujali wewe ndio mhalifu mwenyewe au upo tu eneo la tukio!
Wapumbavu wamekutana na Afisa usalama wa Taifa mstaafu kawala vichwa waoDuh hao polisi walimgusa mtu ambaye hawakumjua, Prof huyo lazima atakuwa na connection.
Sasa polisi hao wamembambikia nyara hizo ili wamtemeshe pesa dah.
Ova
Mzee wa watu alionewa bure,wale Ni majambazi na Ni matapeli,fukuza kazi funga jela maishaAskari Polisi saba wakiwemo watano wa kituo cha Polisi Usa Wilayani Arumeru Mkoani Arusha na wawili wa Kituo Kikuu cha Polisi Arusha wamefukuzwa kazi kwa fedheha kwa kosa la kushawishi na kuomba rushwa ya shilingi milioni 100.
Wiki iliyopita Kamanda wa TAASISI ya Kuzuia na kupambana na Rushwa Nchini {TAKUKURU}Mkoani Arusha,James Ruge alikiri kuwakamata askari hao kushawishi na kupokea kiasi hicho Cha fedha ili wasimfungulie Kesi ya uhujumu uchumi ambapo angefia gerezani.
Hata hivyo Ruge alisema uchunguzi wa kesi hiyo bado haujakamilika na ukikamilika atatoa taarifa kwa vyombo vya Habari juu ya makasa mzima.
Vyanzo vya Habari vilisema kuwa mienendo ya mashtaka ya kijeshi ya kipolisi ilifanyika katika tarehe Aprill 22,23,24 na tarehe 25 mwaka huu , ambapo Askari hao walifukuzwa kazi rasmi ndani ya jeshi la polisi na sasa wanasubiri kushitakiwa katika Mahakama za kiraia wakati wowote.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Justin Masejo alipoulizwa juu ya jeshi hilo kuchukua hatua hizo alisema kuwa hayo ni mambo ya ndani ya Polisi na sio rahisi kutolewa hadharani kwani ni kinyume na maadili ya kazi.
Naye mhanga wa tukio hilo ambaye ni mfanyabiashara wa mji wa Usariver,Profesa Justin Maeda{77}akizungumza nyumbani kwake katika Kijiji cha Nshuku kata ya Nkoaranga wilayani Arumeru alisema pamoja na mkasa wote alioupata na kuishukuru Polisi kwa hatua walizochukua ila amesikitishwa na kitendo cha polisi hao kukiuka maadili ya kazi na kuomba rushwa katika kituo cha Polisi Usa hatua ambayo ilimshangaa na kushindwa kujua OCD na OC CID washindwe kujua tukio hilo.
Profesa Maeda ambaye alianza kufundisha UDSM Mwaka 1970 na kuwafundisha viongozi wengi wa serikali kabla ya kuwa Mshauri Mkuu wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1981-1985 Ikulu sasa ameanza kuamini maneno ya watu wa Usa kuwa ndani ya kituo cha polisi Usa kinanuka rushwa na kuna askari wa kituo hicho kitendo cha upelelezo ni miungu mtu kwani wako hapo kwa miaka mingi sasa wamejivika ufalme wa kuomba kiasi chochote cha rushwa ndani ya kituo mhicho bila kuogopa chochote.
Alisema kama yeye amebambikiwa kesi ya nyaraka za serikali na kuchomekewa shambani kwake na kutakiwa kutoa rushwa ya shilingi milioni 200 kabla ya kufikia makubaliano ya shilingi milioni 100 kuna raia gani Arumeru wameshafanyiwa unyama wa aina hiyo kwani hiyo ni hatari na viongozi wakuu wa polisi Mkoani Arusha na Makao makuu wanapaswa kutupia macho zaidi kituo hicho maana dhuruma na uhuni umekithiri kupita kiasi hivyo hatua zinapaswa kuchukuliwa sasa.
Profesa Maenda ambaye ana Mke na Watoto watatu ambao wote wako nje ya nchi alisema polisi hao ambao walikuja nyumbani kwake na gari mbili za polisi marchi 19 mwaka huu majira ya kati ya saa 7 mchana na saa 8 wakiwa wamejaa kwenye gari na wakiwa na silaha na gari ndogo aina ya Rv4 ambayo hakufanikiwa kushika namba walijitambulisha kuwa ni polisi ya Us ana makao makuu na alimtambua mmoja{jina tunahifadhi} wameagizwa kwenda kwake kupekua kwa kuwa wanataarifa za kiitelejesia kuwa anafanya biashara ya nyara za serikali ikiwemo meno ya tembo na Ngozi za chui.
Alisema kwa kuwa hajawai na hajui kitu kinaitwa Nyara za serikali na hajawahi kufanya biashara hiyo aliwaruhusu kufanya upekuzi lakini cha kushangza hawakufanya ndani ya nyumba bali walikuwa wakipita nje ya kwenda moja kwa moja shambani kwenye mizinga ya nyuki.
Profesa ambaye ameshafanya kazi UN hususani UNICEF nchi mbali za kiafrika na kumalizia nchi ya Zimbabwe mwaka 2002 alion aaskari mmoja akichukua mzinga na kutoa ndani ya mzinga kitu alichodai ni meno ya tembo na kusema hicho ndio kitu walichokuwa wakikitafuta.
Alisema kuwa yeye alisema shambani kwake hukaa zaidi ya miezi miwili au mitatu kuingia hivyo aliwauliza askari hao hii imeletwa na nani kwani hajawahi kufanya biashara hiyo ila alijibiwa na askari hao kuwa hiyo imekula kwake kwani hii ni kesi ya uhujumu uchumi na angefungwa Maisha hivyo anatakiwa kuweka mambo sawa.
Mzee huyo ambaye isema alistaafu miaka ishirini iliyopita alilipwa kiinua mgongo chake{PENSHENI} cha kiasi cha shilingi milioni 74 na kuweka benki ya CRDB na NMB alichukuliwa hadi kituo cha polisi Us ana kuanza kuchukuliwa maelezo na kuombwa rushwa ya shilingi milioni 200 wakati akitoa maelezo.
Profesa alisema yeye aliwaambia kuwa jana yake yaani marchi 18 mwaka huu alikwenda benki na kuchukua kiasi kidogo cha pesa hivyo kiasi hicho hana na kuwataka wapokee milioni 100 na ndipo alipokwenda benki akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi na kuchukua shilingi milioni 74 na baadae alikwenda dukani kwa mdogo wake hapo Usariver na kuchukua kiasi cha shilingi milioni 30 na zote aliwapa polisi katika kituo cha Usa kwani rushwa ilifanyika hapo.
Alisema na kuiomba serikali iweze kumrudishia kiasi cha pesa yake kwani ni kiunua mgongo cha utumishi wake wa kazi wa miaka mingi kazi.
Mwisho
Hao viongozi wenyewe waliingiaje madarakani?Lawama tu bila sababu, hemu tushauri chujio la maadili ili tuwashauri viongozi wetu walitumie!
Unadhani tabia za kubambikizia watu makosa ya uhujumu uchumi askari waliiga kutoka kwa nani?Hawa askari Angekuwepo mzee Magufuli. ..Hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii. (in Magu sukuma's voice)
Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Wewe hujui kitu, hivi uliisha wahi kumiliki pesa? Hayo ya kubambikizwa kesi yatatokea kila siku .CV. peke yake haitoshi kuwa sababu ya yeye kushindwa kujihusisha na makosa ya kiuhalifu wa kutaka kupata pesa nyingi kwa muda mfupi na ukizingatia yupo jirani na hifadhi si mgeni na pembe za ndovu kuna wasomi wana CV nzuri lakini wanapiga dili mpaka unashangaa,ninachotaka kusema uchunguzi wa kutosha ufanyike na huyo Prof.asipoitwa na TAKUKURU kuhojiwa kwanini alijihusisha na kushawishi na utoaji rushwa kama sheria inavyosema mtoaji na mpokeaji wote wana kosa la kujibu hapo tutakuwa na safari ndefu ya kupambana na kuzuia vitendo vya rushwa ambapo mpaka msomi ambaye Prof.aliyetumikia taifa kwa muda mrefu mpaka amestaafu leo hii anaongozana na watu kwenda benki kutoa pesa na kutoa hongo ili asifikishwe mahakamani inasikitisha sana.