ARUSHA: Askari Polisi 7 waliombambikia pembe za ndovu Prof. Justin Maeda na kuchukua milioni 100 wafukuzwa kazi, Profesa afunguka

ARUSHA: Askari Polisi 7 waliombambikia pembe za ndovu Prof. Justin Maeda na kuchukua milioni 100 wafukuzwa kazi, Profesa afunguka

Ushahidi ndio shida mzee hawa jamaa kama wali master mind hio plan lazima hawakuacha ushahidi
 
Nimefuatilia kwa karibu sana tukio la unyanyasaji na ujambazi aliofanyiwa na polis wa kituo cha polis Usa River kule Arusha, Prof Maeda la million 100, nikagundua, kuwa pamoja na polisi 7 kufukuzwa kazi hado hadi leo OCD na OC CID,na mkuu wa kituo cha polisi Usa River, wapi kazini na wanaendelea kuchapa kazi kama kawaida na IGP amepiga kimya kama kawaida yake. Ninashauri nilio wataja waunganishwe na hao askari 7 na kufikishwa mahakamani haraka na mapema iwezekanavyo.
huo ni unafiki au unachuki biafsi na hao uliowataja sasa waliotenda kosa wamefukuzwa kazi hao wengine wa nini wewe? kesi ikiunguruma ndiyo kama nao wanahusika watatajwa yaani waache kazikwa kosa gani wakati wamefanya kazi kuwatoa hao wahalifu? acha chuki za kike hizo kama mnagombea bwana
 
polisi wa chini au ngazi za kati wanaweza kutenda kosa bila wakubwa wao kujua,ndio maana wanatanguliza malipo au rushwa kabla ya kukufikisha ngazi za juu wasigundue
 
Profesa asimulia alivyochukuliwa millioni 100 na askari akidaiwa kuwa na pembe za ndovu

Godfrey Thomas TZA · 24 minutes ago

[https://millardayo]
Profesa Justin Maeda ambaye amefanya kazi sehemu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa msaidizi wa hayati mwalimu Julius Nyerere amesimulia tukio lililotokea nyumbani kwake baada ya watu waliofika nyumbani kwake nakujitambulishwa kuwa ni askari wakidai kwamba awape fedha shilingi million 100 ili waweze kumsaidia baada ya kwenda kwenye eneo lake analofugia nyuki nakukuta pembe ambayo hajajua imetoka wapi.

Maeda anasema alichukuliwa nakupelekwa kituo cha polisi Usa River Mkoani Arusha akiwa na askari hao huku wakimuamuru kutoa shilingi million 200 la sivyo atashtakiwa kwa kosa la uhujumu uchumi ndipo baadaye walimtaka kutoa millioni 100 nakwenda naye benki nakutoa million zaidi ya 70 alizolipwa baada yakustaafu nakuwapa askari ambapo baadaye aliamua kwenda TAKUKURU.

Taasisi yakuzuia nakupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Arusha kupitia kwa mkuu wa taasisi hiyo James Ruge amekiri kuwashilikia askari saba kwa uchunguzi kuhusiana na tuhuma hizo za rushwa.

TAKUKURU ARUSHA YAWASHIKILIA ASKARI SABA KWA TUHUMA ZA RUSHWA “UCHUNGUZI UNAENDELEA”

Nimefuatilia kwa karibu sana tukio la unyanyasaji na ujambazi aliofanyiwa na polis wa kituo cha polis Usa River kule Arusha, Prof Maeda la million 100, nikagundua, kuwa pamoja na polisi 7 kufukuzwa kazi hado hadi leo OCD na OC CID,na mkuu wa kituo cha polisi Usa River, wapi kazini na wanaendelea kuchapa kazi kama kawaida na IGP amepiga kimya kama kawaida yake. Ninashauri nilio wataja waunganishwe na hao askari 7 na kufikishwa mahakamani haraka na mapema iwezekanavyo.
 
huo ni unafiki au unachuki biafsi na hao uliowataja sasa waliotenda kosa wamefukuzwa kazi hao wengine wa nini wewe? kesi ikiunguruma ndiyo kama nao wanahusika watatajwa yaani waache kazikwa kosa gani wakati wamefanya kazi kuwatoa hao wahalifu? acha chuki za kike hizo kama mnagombea bwana
Kugawana milioni 100 kwenye kituo cha polisi bila OCD , OC CID na mkuu wa kituo kuhusishwa ni miujiza kwa kituo cha polisi Usa River Arusha. Pia kuendelea na kazi ni kutanya kazi ya uchunguzi kuwa ngumu na kufichwa kwa ukweli.
 
Ni mara chache sana polisi wadogo wajihusishe na tukio kubwa kiasi hiki bila wakubwa kushiriki
 
Kugawana milioni 100 kwenye kituo cha polisi bila OCD , OC CID na mkuu wa kituo kuhusishwa ni miujiza kwa kituo cha polisi Usa River Arusha. Pia kuendelea na kazi ni kutanya kazi ya uchunguzi kuwa ngumu na kufichwa kwa ukweli.
siyo kweli huo ni unafiki wako tu hebu ficha aibu ya chuki zako kwa hao watu mtu anaweza kupiga dili mkama hiyo hata pekeyake itakuwa watu saba? kesi tayariishaingia kwenye upelelezi kwanini usiache wafanye upelelezi kama wamowata julikana wewe unalazimisha waache kazi au walikupigia mkewako ndiyo maana unachuki nao?
 
In short, kituo cha polisi Usa River Arusha, kinamuaibisha IGP. Nitashangaa sana kama viongozi wa hao hawatawajibishwa.
 
Nchi ya kishamba sana hii, hao wote ni wakufukuza kabiss tena wawekwe ndani kabisa. Maana watakuwa wanajua kila kitu kilichotokea.

Naomba nikabiziwe nchi mwezi mmoja tu nimsaidie mama kutoa huu uchafu .
 
...Nimvekwazika kidogo hapo Mkuu. Kama huyu Profesa naye alikuwa ni Msafi na hana Mazonge zonge yoyote, kwa nini alitaka kuwapa hao makalamba hela yote hiyo wakati moyomi ansjua yupo safi na hana kosa lolote?
Inafikirisha. [emoji848][emoji848]
Ukiona hivyo labda Mzee anakula na baadhi ya wakubwa wa vyombo vya ulinzi na Usalama! Sasa vyuma vimeuumana!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Huyo Prof. naye TAKUKURU wamfungulie mashitaka kwa kushawishi kutoa rushwa(Corruption transaction) kama alikuwa hausika kwanini aogope kufikishwa mahakamani ili mahakama itoe maamuzi kama alibambikiwa kesi au la, hayo meno ya kwenda kumbambikizia yeye hao askari waliyatoa wapi kama si walipata taarifa kutoka wa raia wema kuwa kuna pembe za ndovu shambani kwa huyo mzee.

Jeshi la POLISI na TAKUKURU wachunguze account za huyo mzee na wapime biashara zake kama kwa haraka tu ametoa milioni mia inatia shaka.Kosa la hao askari ni kukubali kupokea rushwa baada ya kushawishiwa na mtuhumiwa.
 
Katika wizara zote wizara ya mambo ya ndani na genge lake la polisi wanahitaji kufanyiwa marekebisho makubwa aisee
Polisi wengi ni mijizi mikubwa,walafi,njaa njaa,na wapenda rushwa wakubwa Nina ushahidi juu ya Hilo kabisaaaa hii mijitu inawalinda wahalifu na kuwapa case innocent people!
Kwa kweli inauma sana! Alafu siku hizi ukienda kituo cha police kutoa malalamiko yako,eti wanakwita mteja wao!! Maana matatizo yako kwao ndiyo fursa ya kupunguza ukali wa Maisha kwao!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
HV kwel utoe million Mia kwa Jambo ujalifanya kabsa nadhani huyu prof kuna jambo
Na Kama kweli alikua hajawai katika Maisha yake Kuambiwa kakutwa na meno ya Tembo,kwa umri wake ule kwanza angendondoka kwa mshutuko na wala asingekua na nguvu ya kuzunguka ma bank yote kutoa pesa kwa ku force!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Kuna mamia ya watu hususan wafanyabiashara waliporwa fedha zao kwa yanayosemekana kuwa maagizo kutoka juu. Inasikitisha sana kisa hiki:
 
Hawa jamaa hawana hata akili mtu ameshawahi kua mshauri wa raisi wewe unategemea ni mtu wa kawaida tu huyo!

Prof Maeda anaishi maisha simple sana ila ni mtu mmoja mkali san kwenye mali zake nakumbuka alimuona mjinga kijana alieokota mkoba wake wa pesa na kumrudishia,akamshangaa na kumuambia atakufa masikini.

Mzee ambae pamoja na mali nyingi alizonazo ila hata akinunua hindi la kuchoma lazima aombe punguzo. Si mtu wa mchezo na pesa anayo nyingi tu sema hao askari haki yao wameipata hao watu wa kuishi nao vyema kwenye jamii sababu ni sawa na wawekezaji wa ndani
 
Back
Top Bottom