Arusha: Atobolewa Jicho na kung'olewa meno mawili kisa wivu wa mapenzi

Arusha: Atobolewa Jicho na kung'olewa meno mawili kisa wivu wa mapenzi

Matukio ya kushamiri kwa wivu wa mapenzi mkoani Arusha yaanza kutikisa tena mara baada ya Mwanamke Mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Jackline Mnkonyi{38} mkazi wa Sombetini Jijini Arusha mei 23 mwaka huu majira ya saa 5 usiku alipata kipigo kikali kutoka kwa mume wake ikiwa ni pamoja na kung’olewa meno mawili na kutobolewa jicho kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

IMG-20230526-WA0016.jpg


Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwa wazazi wake eneo la Sinoni kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha,Jackline alisema kuwa baada ya kupata kipigo hicho alichukuliwa bila kujitambuwa na kupelekwa nyumbani kwa wazazi wake Sinoni na kutupwa getini bila ya kujitambua.

Alisema Mume wake mara baada ya kufika eneo la nyumbani aliwapigia simu wazazi wake na wazazi wake walipofungua geti walimkuta katika hali mbaya na baadae waliamua kumchukua na asubuhiu alipelekwa hospital ya kaloleni kwa matibabu zaidi.

Akizungumza Mkasa huo alisema kuwa,mchana wa mei 23 mwaka huu alitembelewa na mjomba wake ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi{CCM} Simiyu aliyetambuliwa kwa jina la Vicent Matai .

IMG-20230526-WA0017-768x1024.jpg


Jackline alisema na kumtaja mume wake kwa jina la ,Isaack Mnyagi Mwalimu na mkazi wa wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro huja baada ya muda wa zaidi ya miezi mitatu na zaidi kuona watoto wawili aliozaa nao na siku hiyo alikuja usiku ghafla.
Alisema alipofika nyumbani Sombetini maajira ya saa 4.45 usiku aligonga mlango na kufunguliwa na watoto lakini hakutaka salamu na kuingia chumbani na alipomfuata alitoka chumbani.

Jackline alipoona hivyo alimuuliza kulikoni alichoambulia ni maneno mazito na matusi na kuulizwa mchana alikuwa na nani na alimjibu kuwa alikuwa na mjomba wake hatua ambayo alikana na kusema kuwa ni mtu wake na huwa wanafanya umalaya hatua ambayo alipinga lakini alijikutaja akipigwa na ‘’mjeledi’’ mgongoni.

FB_IMG_1685098776337.jpg


Picha ya Mume wa Jacline aliye mshambulia Mke wake kwa silaa za jadi .

Alisema alijitahidi sana kujieleza lakini ilishindikana na Mume wake Mnyagi alichukua Plaizi kifaa cha gereji na kumwamuru afungue mdomo na kung’olewa jino moja baada ya lingine huku akipata kipigo kikali na kujikuta na maumivu makali hadi jana.

Jackline alisema hatua hiyo aliona kama haitoshi aliamua kuchukua kitu chenye Icha kali na kumtoboa jicho moja ambalo hadi sasa hawezi kuona na kumwambia maneno mazito na mtusi huku akiendelea kupigwa hali iliyomfanya kupoteza fahamu.

Alisema hakujua jinsi alivyofikishwa nyumbani kwa wazazi wake Sinoni Daraja mbili na kutupwa getini kwani nilishtuka nikiwa hospital .

‘’Nimetobolewa jicho na nimeng’olewa meno mawili kwa chombo kinachoitwa Plaiz nina maamuvi makali sana naiomba serikali ichukue hatua dhidi ya mume wake kwani amenifanyia unyama wa hali ya juu’’alisema Jackline

Naye Mzazi wa Jackline,Mzee Elimilis John Mkonyi alisema kuwa baada ya kumpeleka katika hospital ya Rufaa ya Mount Meru na kupata matibabu alikwenda kituo kikuu cha polisi Arusha na kufungua jalada shambuli la kuzulu mwili kesi namba ARS/RB/5416/2023.


IMG-20230526-WA0002.jpg


Muonekano wa Jackline akiwa mzima kabla ya kupata kipigo kutoka kwa mume wake

Yani ni hili lipumbavu ndo limepiga mke, yupo kwenye hii video anaimba na Fanuel Zedekia, wimbo ukianza tu utaona anavyotabasam

 
Huyo mbwa bado hajawekwa nyuma ya nondo,Wanawake wenzangu ukiona Mpenzi wako anakupiga kofi jua iko siku atakuja kukuvunja meno endeleeni kuvumilia [emoji51]
Lazima yupo nyuma ya nondo na kipondo kikali sana kutoka kwa polisi wetu shupavu, na bado atatupwa jela ataishi maisha ya mateso kwa miaka mingi huko akapigane na wanaume wenzie aone virungu vinavyoingia, shenzi zake
 
Mngeanza kubadilika nyie, ukiona mtu hakufai achana nae kumpiga mwanamke ni udhaifu na matusi makubwa kwa mtu anayejiita mwanaume, yaan ukimpiga mwanamke urijali wako umevuka.
Ukihudumia mgodi na ukakupotezea muda na gharama unajua matokeo yake?
 
Back
Top Bottom