Arusha: Atobolewa Jicho na kung'olewa meno mawili kisa wivu wa mapenzi

Arusha: Atobolewa Jicho na kung'olewa meno mawili kisa wivu wa mapenzi

Ndio hivyo akishikwa na njaa ndio pa kukamatwa Ila kuna jamaa alisimulia humu kua kuna sehemu uko mipakani ndio hua jamaa waharifu hua wakakimbilia mara nyingi
Huko mipakani msosi atapewa na nani,aheri ushibie jela,njaa inatesa hatari.Labda aende kwa ndugu wa mbali wamhifadhi.Ila nawaza kazini kule Rombo itakuaje? Je hatafukuzwa kazi?
 
Kwa muonekano huu pichani sikubaliani na kauli kwamba siku ya tukio huyu mjeruhiwa alionekana akiwa na mjomba wake mwenyekiti wa ccm wilaya ya Simiyu.
IMG_20230527_203743.jpg
 
moja wapo kusini, nilishawahi muona jamaa alifanya soo miaka ya nyuma Kinondoni
nikamkuta Nyangao ndani ndani huko Mahiwa, jamaa midevu kibao
Yes maeneo hayo hayo km unaelekea Msumbuji au mpakani mpakani huko polisi hua hawakanyagi,
 
Kuishi na mtu mliekutana ukubwani inahitaji moyo wa chuma,kama sio uvumilivu na kusameheana utaishi dingo mpaka ufe
Ndio inabidi uwe na moyo wa uvumilivu sana kinyume na hapo utazua taharuki kwa Jamii kwa tukio utakalolifanya watu hawatoamini km ni wewe ndie uliefanya hivyo,
 
Huko mipakani msosi atapewa na nani,aheri ushibie jela,njaa inatesa hatari.Labda aende kwa ndugu wa mbali wamhifadhi.Ila nawaza kazini kule Rombo itakuaje? Je hatafukuzwa kazi?
Kuna wavuvi mkuu pembezoni humo mwa Bahari ya Hindi, kazi ndio kwakheri huyo anaanza ukurasa mpya km mharifu na mtu aliefanya shambulio la mwili na kutishia kuua yaan hapo ana mashtaka km 10 hivi kwa haraka haraka itategemea na maelezo ya mwanamke yamesemaje Ila ana mashtaka 10 ya haraka haraka na katika hayo 10 Basi 5 hachomoki maana alishajivuruga alipowaambia wazazi wa mwanamke nendeni muchukue mzoga wenu hapo getini
 
Naona wengi wanasema hawajui chanzo mara ooh story ya upande mmoja. Hivi vuta picha ni binti yako wa kumzaa ndio anafanyiwa hivyo na mumewe!? Utaelezwa lugha gani ili uelewe somo. Acheni kujifanya mna haki na maisha ya watu, sababu na uhakika hata huyo baba huko alikokuwa miezi mitatu hakuwa mtakatifu sasa ya nini kumhukumu mwenzio.

Tunatofautiana, Mi ni baba na nimejaliwa watoto jinsia zote ila wanangu hata wakiuliwa ni wao since sitegemei watoto kwenye maisha yangu, na nishaga wambia kilakitu kuhusu mambo ya mahusiano tena kama uyu wakike anavyolelewa ovyo na mama ake sijui kama atawezana na mahusiano ila siku akinimbia amepata mchumba mimi sikatai natoa baraka, so akienda akapigwa visu na kutolewa meno iyo ni juu yake maana kachagua mwenyewe, mimi nitamuuliza tu unaendelea au umemaliza, akisema anaendelea na mwambia safari njema na dua namwombea.
 
Itafika kipindi watu wataogopa kuozesha watoto wao

Sasa wang’ang’anie waje wapigiwe mimba nyuma ya nyumba yako kama paka, watoto wakikua sio wako tena ni wadunia we waambie ukweli wako na ushauri so atayefata afate asiefata mwache apate exposure na experience ya maisha na awe mfano kwa wenzake.
 
Huyo mbwa bado hajawekwa nyuma ya nondo,Wanawake wenzangu ukiona Mpenzi wako anakupiga kofi jua iko siku atakuja kukuvunja meno endeleeni kuvumilia [emoji51]
Mimi baba angu akiozesha anamuita mkwe na wazazi wake anamuambia hivi"Binti hapigwi Mimi watoto wangu nawaelekeza wanaelewa siwapigi pia"akikushinda mrudishe Kwa wema Bora talaka kuliko jeneza au ulemavu wa kudumu"anamaliza hapo Mzee wangu nampenda Sana
Na hakuna mapenzi kwenye kupigana Ndoa ni huruma na mapenzi...
 
Wanaume tunakwama wapi jamani!? Mbona maisha matamu hata mkitengana!?kwann umuumize mzazi mwenzio!? Mkishindwana achana nae!? Wazuri wapo jamani!! Daaah
 
Mwanamke Mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Jackline Mnkonyi mwenye umri wa miaka 38 mkazi wa Sombetini Jijini Arusha mei 23 mwaka huu majira ya saa 5 usiku alipata kipigo kikali kutoka kwa mume wake ikiwa ni pamoja na kung’olewa meno mawili na kutobolewa jicho kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

IMG-20230526-WA0016.jpg

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwa wazazi wake eneo la Sinoni kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha,Jackline alisema kuwa baada ya kupata kipigo hicho alichukuliwa bila kujitambuwa na kupelekwa nyumbani kwa wazazi wake Sinoni na kutupwa getini bila ya kujitambua.View attachment 2635779

Alisema Mume wake mara baada ya kufika eneo la nyumbani aliwapigia simu wazazi wake na wazazi wake walipofungua geti walimkuta katika hali mbaya na baadae waliamua kumchukua na asubuhiu alipelekwa hospital ya kaloleni kwa matibabu zaidi.

Akizungumza Mkasa huo alisema kuwa,mchana wa mei 23 mwaka huu alitembelewa na mjomba wake ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi{CCM} Simiyu aliyetambuliwa kwa jina la Vicent Matai .

IMG-20230526-WA0017-768x1024.jpg

Jackline alisema na kumtaja mume wake kwa jina la ,Isaack Mnyagi Mwalimu na mkazi wa wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro huja baada ya muda wa zaidi ya miezi mitatu na zaidi kuona watoto wawili aliozaa nao na siku hiyo alikuja usiku ghafla.
Alisema alipofika nyumbani Sombetini maajira ya saa 4.45 usiku aligonga mlango na kufunguliwa na watoto lakini hakutaka salamu na kuingia chumbani na alipomfuata alitoka chumbani.

Jackline alipoona hivyo alimuuliza kulikoni alichoambulia ni maneno mazito na matusi na kuulizwa mchana alikuwa na nani na alimjibu kuwa alikuwa na mjomba wake hatua ambayo alikana na kusema kuwa ni mtu wake na huwa wanafanya umalaya hatua ambayo alipinga lakini alijikutaja akipigwa na ‘’mjeledi’’ mgongoni.

FB_IMG_1685098776337.jpg

Picha ya Mume wa Jacline aliye mshambulia Mke wake kwa silaa za jadi .

Alisema alijitahidi sana kujieleza lakini ilishindikana na Mume wake Mnyagi alichukua Plaizi kifaa cha gereji na kumwamuru afungue mdomo na kung’olewa jino moja baada ya lingine huku akipata kipigo kikali na kujikuta na maumivu makali hadi jana.

Jackline alisema hatua hiyo aliona kama haitoshi aliamua kuchukua kitu chenye Icha kali na kumtoboa jicho moja ambalo hadi sasa hawezi kuona na kumwambia maneno mazito na mtusi huku akiendelea kupigwa hali iliyomfanya kupoteza fahamu.

Alisema hakujua jinsi alivyofikishwa nyumbani kwa wazazi wake Sinoni Daraja mbili na kutupwa getini kwani nilishtuka nikiwa hospital .

‘’Nimetobolewa jicho na nimeng’olewa meno mawili kwa chombo kinachoitwa Plaiz nina maamuvi makali sana naiomba serikali ichukue hatua dhidi ya mume wake kwani amenifanyia unyama wa hali ya juu’’alisema Jackline

Naye Mzazi wa Jackline,Mzee Elimilis John Mkonyi alisema kuwa baada ya kumpeleka katika hospital ya Rufaa ya Mount Meru na kupata matibabu alikwenda kituo kikuu cha polisi Arusha na kufungua jalada shambuli la kuzulu mwili kesi namba ARS/RB/5416/2023.

IMG-20230526-WA0002.jpg

Muonekano wa Jackline kabla ya kupata kipigo kutoka kwa mume wake
Huyi bwana ni mshenzi!
 
Inafikirisha sana Ila kuna maelezo hayajajitosheleza kuna kitu bado kimejificha jamaa anaweza akawa na maelezo mengine yatakayo waacha watu midomo wazi ngoja akamatwe aje kusema ukweli
Alivyosema ni kwamba: alipigwa ngumi nyingi kwanza hadi nusu kuzimia, ndio mengine yakaendelea
 
Kabisa kabisa kumpiga mwanaumee yeyote mpigaji mi nasemaga ni chiziii ana afya ya akili
Ni uchizi kweli wala sio uzima na sio tu Mwanamke hata kumpiga mtoto hua nasema naonekana mbaya juzi kati huko huko Arusha Baba kampiga mtoto wake wa darasa la kwanza kipigo kama cha mwizi wa kariakoo hadi kamuharibu sehemu za siri, yaan mtoto mdogo kaumuka uso hadi anatisha, Mwanaume mzima na misuli imemkomaa ya mikono anapiga mtoto kama unaua nyoka au anapiga Mwanamke kama anakanda unga wa Maandazi akili zitoke wapi hapo kama sio ukichaa kasoro kuvua nguo.
 
Mwanamke Mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Jackline Mnkonyi mwenye umri wa miaka 38 mkazi wa Sombetini Jijini Arusha mei 23 mwaka huu majira ya saa 5 usiku alipata kipigo kikali kutoka kwa mume wake ikiwa ni pamoja na kung’olewa meno mawili na kutobolewa jicho kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

IMG-20230526-WA0016.jpg

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwa wazazi wake eneo la Sinoni kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha,Jackline alisema kuwa baada ya kupata kipigo hicho alichukuliwa bila kujitambuwa na kupelekwa nyumbani kwa wazazi wake Sinoni na kutupwa getini bila ya kujitambua.View attachment 2635779

Alisema Mume wake mara baada ya kufika eneo la nyumbani aliwapigia simu wazazi wake na wazazi wake walipofungua geti walimkuta katika hali mbaya na baadae waliamua kumchukua na asubuhiu alipelekwa hospital ya kaloleni kwa matibabu zaidi.

Akizungumza Mkasa huo alisema kuwa,mchana wa mei 23 mwaka huu alitembelewa na mjomba wake ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi{CCM} Simiyu aliyetambuliwa kwa jina la Vicent Matai .

IMG-20230526-WA0017-768x1024.jpg

Jackline alisema na kumtaja mume wake kwa jina la ,Isaack Mnyagi Mwalimu na mkazi wa wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro huja baada ya muda wa zaidi ya miezi mitatu na zaidi kuona watoto wawili aliozaa nao na siku hiyo alikuja usiku ghafla.
Alisema alipofika nyumbani Sombetini maajira ya saa 4.45 usiku aligonga mlango na kufunguliwa na watoto lakini hakutaka salamu na kuingia chumbani na alipomfuata alitoka chumbani.

Jackline alipoona hivyo alimuuliza kulikoni alichoambulia ni maneno mazito na matusi na kuulizwa mchana alikuwa na nani na alimjibu kuwa alikuwa na mjomba wake hatua ambayo alikana na kusema kuwa ni mtu wake na huwa wanafanya umalaya hatua ambayo alipinga lakini alijikutaja akipigwa na ‘’mjeledi’’ mgongoni.

FB_IMG_1685098776337.jpg

Picha ya Mume wa Jacline aliye mshambulia Mke wake kwa silaa za jadi .

Alisema alijitahidi sana kujieleza lakini ilishindikana na Mume wake Mnyagi alichukua Plaizi kifaa cha gereji na kumwamuru afungue mdomo na kung’olewa jino moja baada ya lingine huku akipata kipigo kikali na kujikuta na maumivu makali hadi jana.

Jackline alisema hatua hiyo aliona kama haitoshi aliamua kuchukua kitu chenye Icha kali na kumtoboa jicho moja ambalo hadi sasa hawezi kuona na kumwambia maneno mazito na mtusi huku akiendelea kupigwa hali iliyomfanya kupoteza fahamu.

Alisema hakujua jinsi alivyofikishwa nyumbani kwa wazazi wake Sinoni Daraja mbili na kutupwa getini kwani nilishtuka nikiwa hospital .

‘’Nimetobolewa jicho na nimeng’olewa meno mawili kwa chombo kinachoitwa Plaiz nina maamuvi makali sana naiomba serikali ichukue hatua dhidi ya mume wake kwani amenifanyia unyama wa hali ya juu’’alisema Jackline

Naye Mzazi wa Jackline,Mzee Elimilis John Mkonyi alisema kuwa baada ya kumpeleka katika hospital ya Rufaa ya Mount Meru na kupata matibabu alikwenda kituo kikuu cha polisi Arusha na kufungua jalada shambuli la kuzulu mwili kesi namba ARS/RB/5416/2023.

IMG-20230526-WA0002.jpg

Muonekano wa Jackline kabla ya kupata kipigo kutoka kwa mume wake
HV mtu unatembee had na mjomba wako huu umalaya ni wa wapi bila shaka hawa Ni wanyaturu
 
Back
Top Bottom