Arusha: Dereva wa Serikali aenda na maiti bar

Arusha: Dereva wa Serikali aenda na maiti bar

Sisi tutajua kama kweli ni bar hapo !!??

Hata kama ni baa, huko ndani ya jeneza muhusika yumo tayari ndani????

Sisi tutakuamini vp, je labda unavisa na dereva wa gari ONESHWA hapo juu???

: MKAZANE MAISHA MAGUMU 😆
Sisi source yetu ni mleta Mada mpaka Mtuhumiwa atakapojitokeza na kueleza upande wake wa Story.
 
Unaweza kuta walisimama hapo kumpitia mtu waende naye ama kuchukua msosi au vinywaji ila mpita njia mpiga picha kwakuwa hajui kinachoendelea akaamua kutunga story, hata angekuwa amepaki guest house na jeneza tupu ungesikia mengine. Hakuna mtu mwenye akili timamu wa kufanya kitu kama hiko ukizingatia ni mtumishi wa umma na ukizingatia pia dunia ni kijiji.
 
Kifo ni ukumbusho kua binadamu ni mtu wa kupita tu,kama unavyoona maiti basi tambua kua hata wewe ni maiti mtarajiwa,so,maiti huheshiwa kama wanavyoheshimiwa walio hai,pia kuheshimu maiti ni kuheshimu au kuutukuja uwezo wa Mungu kwa kuchukua uhai wa kiumbe chake,huo hua ni wakati wa kujitafakari kwa wewe ambae bado upo hai na unapumua,

Unapataje ujasiri wa kulewa au kuangalia EPL katika hali hiyo? huyo dereva ni mtu asiyekua na imani,ni mtu wa hatari sana katika jamii ya watu waliostaarabika.
 
Na Malisa GJ

Habari kaka.

Kuna tukio limetokea hapa Arusha usiku huu limenisikitisha sana. Kuna Familia imepata msiba, wanatakiwa kusafirisha kwenda wilayani kuzika lakini hawana uwezo. Hivyo wameomba msaada wa gari ya serikali kusafirisha maiti. Gari hiyo imebeba maiti na ndugu wachache wa marehemu.

Cha kushangaza dereva amekuja na maiti hapa Sakina bar, amepaki gari, akawashusha ndugu wa marehemu kisha akaingia ndani kutizama EPL. Nimeumia sana kuona wamama wako nje wanalia, jamaa yuko ndani anakunywa na kuangalia game. Hakika umaskini ni mbaya sana. Naomba upaze sauti ili serikali iweze kuchukua hatua kwa kitendo hiki cha kinyama na kisicho cha utu.

Binadamu wote wana haki ya kulindiwa utu wao. Umaskini usiwe sababu ya kudhalilisha wengine. Huyu dereva angekua amefiwa na baba yake mzazi, angediriki kwenda kumuanika bar halafu aangalie mpira? Namba za gari ni STM 3708. Tunaomba serikali ichukue hatua kali kwa dereva na wote waliohusika. Huu ni udhalilishaji mkubwa wa utu.View attachment 2788969View attachment 2788971
Tutakuamini vipi?

Tunaomba picha ya dereva na ndugu wa marehemu wakiwa wanaangua kilio.

Hivi mnatuonaje watanzania?

Usikute ulinyimwa lifti na jamaa unaanza visa na yeye.

Umerogwa na nan?
 
Mambo ya Madereva tuwaachie wenyewe.

Unajuaje je alikuwa hajisikii vizuri na kutaka kupumzika kidogo.

Kama angeendelea kuendesha na akapata ajali Nani angelaumiwa.

Safari ndefu dereva anahitaji kupumzika wakati fulani ili afike salama.
 
Mambo ya Madereva tuwaachie wenyewe.

Unajuaje je alikuwa hajisikii vizuri na kutaka kupumzika kidogo.

Kama angeendelea kuendesha na akapata ajali Nani angelaumiwa.

Safari ndefu dereva anahitaji kupumzika wakati fulami ili afike salama.
.. hovyo kbs! kwahiyo akapumzike bar na maiti huku wafiwa wakiwa nje wanalia unaona imekaa sawa? shuwaini kabisa ww!
 
Na Malisa GJ

Habari kaka.

Kuna tukio limetokea hapa Arusha usiku huu limenisikitisha sana. Kuna Familia imepata msiba, wanatakiwa kusafirisha kwenda wilayani kuzika lakini hawana uwezo. Hivyo wameomba msaada wa gari ya serikali kusafirisha maiti. Gari hiyo imebeba maiti na ndugu wachache wa marehemu.

Cha kushangaza dereva amekuja na maiti hapa Sakina bar, amepaki gari, akawashusha ndugu wa marehemu kisha akaingia ndani kutizama EPL. Nimeumia sana kuona wamama wako nje wanalia, jamaa yuko ndani anakunywa na kuangalia game. Hakika umaskini ni mbaya sana. Naomba upaze sauti ili serikali iweze kuchukua hatua kwa kitendo hiki cha kinyama na kisicho cha utu.

Binadamu wote wana haki ya kulindiwa utu wao. Umaskini usiwe sababu ya kudhalilisha wengine. Huyu dereva angekua amefiwa na baba yake mzazi, angediriki kwenda kumuanika bar halafu aangalie mpira? Namba za gari ni STM 3708. Tunaomba serikali ichukue hatua kali kwa dereva na wote waliohusika. Huu ni udhalilishaji mkubwa wa utu.View attachment 2788969View attachment 2788971
Huyu jamaa hana utu hata kidogo, hana aibu, sio binadamu kabisa khaa.
 
Huyu jamaa hana utu hata kidogo, hana aibu, sio binadamu kabisa khaa.
Maeneo ya njia panda Himo, kukuta gari za maiti zimepark watu wanakula/kumwagilia moyo baada ya safari ndefu kutoka Dar kuja Kaskazini ni kawaida.

Inawezekana wahusika walipita hapo sakina Bar kupata chochote kitu ili waendelee na safari

Mleta mada: hiyo maiti ilitokea wapi na inapelekwa wapi?

Hii inaweza saidia kujua kweli dereva alipaki hapo kwa lengo baya au nzuri
 
Back
Top Bottom