BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Linaweza kuwa ni moja kati ya matukio ya nadra kutokea nchini, baada ya Jeshi la Polisi nchini kumtia mbaroni Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ya Loliondo kwa tuhuma za kumlawiti kijana mwenye umri wa miaka 29 baada ya kumlewesha pombe.
Mbali na hakimu huyo kushikiliwa na Jeshi la Polisi, lakini jeshi hilo linamshikilia pia mwathirika wa tukio hilo kutokana na msimamo wa sheria unaosema mwanamume anayemruhusu mwanamme mwenzake kumwingilia naye ametenda kosa la jinai.
Mwananchi Digital ilifanya juhudi za kumtafuta Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo kwa njia ya simu lakini haikufanikiwa baada ya simu yake kuita bila kupokelewa.
Akizungumza na Mwananchi Digital, leo Jumamosi Februari 3,2024, Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Kanali Wilson Sakulo, amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo ambapo amesema Polisi wanaendelea na uchunguzi.
Taarifa kutoka wilayani humo zinadai kuwa hakimu huyo wa Mahakama ya Mwanzo Loliondo, anashikiliwa katika kituo cha Polisi cha Loliondo.