Arusha: Lengai Ole Sabaya afikishwa Mahakamani kwa Uhujumu Uchumi, Utakatishaji Fedha

Jamaa kawa chokoraa ndani ya kipindi kifupi
Jaman haya maisha tuishi vizuri na watu
Kwa mara ya kwanza naanza kuingiwa na huruma dhidi ya huyu jamaa

Nakumbuka akina Mbowe wanawekwa ndani ya makosa ya kubambikwa kuna watu walishangilia

Ili liwe funzo jamani
 
Kazi yote aliyofanya Sabaya ya kumng'oa Mbowe pale Hai leo hii analipwa kwa kushikiwa "bastola" kama jambazi?
Aisee!!!!!
Sabaya ni jambazi na mbakaji mkubwa,,we dada lazima umtetee sababu ni bwanaako pia.
 
Atakapofungwa pia mtujulishe! Nasikia watu wa 'system' na wafia Green hawafungwaji
 
Sabaya atamkumbuka sana Mh Lema kwa maonyo yake kwake. Alambiwa sana ila alishupaza shingo.
mke wa mtu anaweza kukushauri mwanaume kweli? lema kaolewa huyo ni mke wa wanaume huko hana ushauri kwa wanaume
 
Naona hii itakuwa habari njema sana kwa wafuasi wa Mbowe.
Sasa watachekelea utafikiri jimbo la Hai watalipata tena.
By the way, Sabaya alipaswa kupewa tuzo ya heshima na CCM na siyo kushtakiwa. Huu ni usaliti kwa mpiganaji kama huyu.
Mpiganaji wa kitu gani,ndio kusema alitumwa na CCM kufanya aliyoyafanya?
 
Ulisema maneno haya wakati ule wa kina Seth Harbinder na Rugemalila?
 
Hawa TAKUKURU wanaweza kuwasilisha ushahidi dhaifu halafu mwisho wa siku anaachiwa.

That’s what is going to happen!! Ni kweli ana tuhuma kama zote lakini sasa kwamfano tuhuma za kuwataka wake za watu kinguvu kuwabaka nk ishu itakayowachinja ni Ushahidi, je waliripoti polisi? Na taratibu zingine kama hizo
 
Ndugai sheria ilishatengenezwa hatakaa ashitakiwe labda muende kwenye mahakama za asili
 
Unatakiwa kuelewa maana ya jinai kinga anayo raisi tu. Wengine wote lolote linaweza kutokea.
 
hivi wewe hujawahi ona picha cctv za sabaya mitandaoni? na tuhuma mbali mbalia? tumia akili yako hata kwa asilia tano
 
Kwa hizo picha, kwa kweli alikuwa ana haki ya kumwaga machozi alipofarikiJPM ambaye alikuwa anamdekeza!
Bado BASHITE!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…