Arusha: Lengai Ole Sabaya afikishwa Mahakamani kwa Uhujumu Uchumi, Utakatishaji Fedha

Arusha: Lengai Ole Sabaya afikishwa Mahakamani kwa Uhujumu Uchumi, Utakatishaji Fedha

Picha hiyo ikutafakarishe mtu yeyote utakayeiona.

Tambua ya kuwa nafasi uliyonayo ni ya muda tu. Hata kama utaishikilia mpaka mwisho wa uhai wako, ipo mahali utalipwa kutokana na matendo yako.

Busara zikuongoze utende haki na muombe Mungu akusimamie.

Majivuni na ukatili hayana lolote bora la kulipalilia.

Jana ulikuwa ukiwaamuru polisi na kukupigia salute, leo wanakupigisha magoti na pingu mkononi.
DAB imfikie kwenye file aione
 
Hivi huyo jamaa info zake zilikuwa hazifiki kwa wakubwa, aliwezaje ku-survive na mauchafu yote hayo.....
 
nenda hai utapata wengi wenye makovu ya kutendewa na huyu ubwa aliteka vijana wadogo kabisa akaenda kufanyia unyama Arusha huyu Mungu hamuachi sio suala la serekali
Vijana gani hao? Lini? na ilikuwaje?

Hebu taja majina yao!
 
Naona hii itakuwa habari njema sana kwa wafuasi wa Mbowe.
Sasa watachekelea utafikiri jimbo la Hai watalipata tena.
By the way, Sabaya alipaswa kupewa tuzo ya heshima na CCM na siyo kushtakiwa. Huu ni usaliti kwa mpiganaji kama huyu.
CCM yetu haiwaenzi wabakaji, pengine ile CCM ya Bashiru na Mwendazake!
 
Ina maana Magufuli angekuwa bado anaishi, sabaya angekuwa bado mkuu wa wilaya!
Ama kweli, kua uyaone😕
Tunaposema mwendazake alikuwa dikteta uchwara mtuelewe jamani

Kijana wake mpendwa Huyo hapo kadakwa
 
Picha hiyo ikutafakarishe mtu yeyote utakayeiona.

Tambua ya kuwa nafasi uliyonayo ni ya muda tu. Hata kama utaishikilia mpaka mwisho wa uhai wako, ipo mahali utalipwa kutokana na matendo yako.

Busara zikuongoze utende haki na muombe Mungu akusimamie.

Majivuni na ukatili hayana lolote bora la kulipalilia.

Jana ulikuwa ukiwaamuru polisi na kukupigia salute, leo wanakupigisha magoti na pingu mkononi.
Mkuu Mungu akubariki kwa hilo Neno jema.
Tunahubiriwa kila siku, hatusikii!!
 
Siyo kwamba una akili duni, ni kwamba uliwekeza sana kwa mwendazake kiasi kwamba hata mteule wake alipoimba nyimbo za uzalendo hukuweza kujiuliza na hata sasa ni ngumu kwako kufungua ubongo na kufikiri kwa mapana juu ya tuhuma za Sabaya, kwa sababu huyu ni mteule wa shujaa wako. Huwezi kuyaona makosa ya Sabaya na hata ukiambiwa huwezi kuamini. Mwendazake alikamata akili za watu.
 
Back
Top Bottom