Arusha: Mahakama yamkuta Lengai Ole Sabaya na kesi ya kujibu

Arusha: Mahakama yamkuta Lengai Ole Sabaya na kesi ya kujibu

Unyang'anyi na wizi wa kutumia tofauti ninini? Huyu anapaswa kupigwa selasini flani jinga sana!
 
Mabeberu wanajua kazi aliyofanya Magufuli Tanzania miaka takriban sita kama Rais wa Jamhuri na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi na kabla ya hapo miaka kama 20 kama waziri.

Katika kipindi chake cha urais muda huo kuanzia 'go' taa kuwaka kijani kupitia vibaraka wao wakiongozwa na lissu walianza kumpiga vita kwa pupa uongo na lugha za kishenzi kabisa. Yote ilikua mshtuko na hamaki kwa kujua magufuli ni kiongozi imara na mtetezi mkubwa wa maslahi ya umma. Ni mtu muadilifu hahongeki hivyo kua mtu hatari kwa ubwanyenye na unyonyaji wa nguvu kazi ya wavuja jasho.

Wapinga maendeleo wakiongozwa na chadema wamekua wanamuombea kila janga magufuli hadi wamekua wanamwombea kifo. Tuliona kina lema wakimtabiria kifo kama hataacha kuwapambania wanyonge.

Magufuli alipotwaliwa na mola wake adui zake wakiongozwa na wanachadema walionyesha furaha hadharani na kuamini mungu amejibu maombi yao. Kwa imani kwamba mungu amewaletea samia bila shaka wakampelekea fitna nyingi na mama kumtupa sabaya mtumishi mwaminifu wa umma gerezani.

Hii kesi ya sabaya kwa waliyoipanga lengo lao ni kumchafua magufuli. Leo fisadi na wakwepa kodi aliyotumwa sabaya kuwafuatilia ndio wanamuita sabaya jambazi. Hili halitakubaliwa na wananchi kama walivyokataa pale jaribio la kumchafua baba wa taifa lilifanyika na wapinga maendeleo.

Mahakama ipo/ zipo haki ya sabaya itapatikana na magufuli atabakia daima kwenye mioyo ya Watanzania.
 
Dizaini ya watu kama nyinyi huwa ni hasara sana aisee. Hebu mjibu mwana CCM mwenzako hapo juu, kumchafua mtu ambae ameshakufa inasaidia nini?

Na useme wazi wazi kuwa Rais Samia anamchafua Magufuli maana ujinga wote wa huyo unaemtetea ulianzishwa na Samia.
 
Mabeberu wanajua kazi aliyofanya magufuli tanzania miaka takriban sita kama rais wa jamhuri na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi na kabla ya hapo miaka kama 20 kama waziri...
Kwani waliomhusisha magufuli na kesi ya sabaya ni waliofungua kesi au ni aliyefuunguliwa kesi ambaye ni sabaya(kijana wa magufuli)?
 
Okay...

Tuseme lengo ni kumchafua Magu kwa maana Magu hawezi kutuma mtu kufanya uhuni kama uliokuwa unafanywa na Sabaya!!

Kwanini Magu achafuliwe kupitia Sabaya na sio mtu mwingine yeyote yule?

Kuna mazingira yapi yaliyowafanya wanaotaka kumchafua Magu wamtumie Sabaya kufanya uchafuzi huo?

Lakini kwa upande mwingine, kila mwenye macho, utambuzi usio na shaka, na akili timamu; alikuwa anashuhudia au kusikia uhuni uliokuwa unafanywa na Sabaya!!

Sasa tuseme Magu hakuwa akimtuma! Je, unataka kusema Magu hakuwa miongoni mwa wale wenye macho, utambuzi usio na shaka, na akili timamu za kuweza kushuhudia au angalau kusikia uhuni uliokuwa unafanywa na Sabaya?
 
Mtazamo wangu binafsi, Kesi ya Lengai Ole Sabaaya imechukua U-Turn kumchafua Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwageuka wafuasi wa Hayati Magufuli katika Serikali yake.

Kwanini nasema hivo?

Kwa Lengai Ole Sabaaya kuwataja mahakamani;

1) Hayati Magufuli (Huyu ana Kinga kikatiba kwasababu alikua Rais).

2) Dk Mpango (Hana kinga Kisheria kwasababu alikua Waziri Wa Fedha Wakati Jinai Inatendwa).

3) Prof Luoga (Hana Kinga Kisheria - Gavana BOT)

Amewataja kama waambatanaji katika makosa ya jinai alioyafanya (Accomplice & Accessory To The Crime - Kisheria wana hatia na adhabu ni sawa na mtendaji wa jinai).

Hayati Magufuli alikua Rais na anakinga ya Kikatiba kushtakiwa, hao wawili hawana kinga kikatiba katika hayo makosa ya jinai jijini Arusha (Dk Mpango na Prof Luoga) na kisheria ni Accomplice & Accessory to the Crime.

Hoja za kumchafua na kumpima uadilifu Rais Samia Suluhu;

● Je, Wata wajibishwa kisheria na katiba ili Mahakama iachwe ifanye kazi yake ya kutoa hukumu dhidi yao kama wana hatia au hawana, au watawekwa juu ya sheria na katiba???

● Je, Ole Sabaaya ametumika na wanaompinga Rais SSH ndani ya CCM kumtikisa Rais kwa kuwatia kwenye Jinai watu muhimu katika Serikali yake???

● Je, ndio miongoni mwa njia wanayotumia wana CCM waliokua wafuasi wa Hayati Magufuli aliowaacha kwenye Serikali yake, na wakaamua kumpinga Rais SSH kwenye Chanjo za Covid wazi wazi kama njia ya kuonesha dunia yeye ni muumini wa "Double Standard kwenye kuwajibisha watu kisheria".

Rais Samia Suluhu alipo hojiwa na BBC, alisema - Freeman Mbowe aachwe awajibishwe kisheria na mahakama ndio itakayoamua juu ya hatia yake dhidi ya jinai anayo tuhumiwa nayo.

JE, kwa Prof Luoga na Dk Mpango nao watawajibishwa kisheria kama waambatanaji wa hayo makosa ya Ole Sabaaya na mahakama itaachwa kuamua juu ya hatia zao, au watawekwa juu ya katiba ya nchi kwasababu ni watu muhimu katika serikali yake!

 
Wakitaka kumchafua Magufuli wafanye kazi ya maana sio kwà Maneno tu.
 
Acheni uboya mwendazake anachafuliwa anajichafua mwenyewe yaani atume watu kuua kudhalilisha kubambikia kesi na kufilisi leo hii mnasema anachafuliwa shame on you
 
Uongo wako na uache magufuli alichafuliwa toka siku anateuliwa hata mkewe alisema, m nataka awe rais mnamfahamu vizuri lakini, mpaka baba yake mkapa kafa na Juto kubwa. Sembuse sa baYA
 
Hawataweza, wananchi tutampigania Magufuli mpaka mwisho kama alivyotupigania.
 
Mabeberu wanajua kazi aliyofanya magufuli tanzania miaka takriban sita kama rais wa jamhuri na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na kabla ya hapo miaka kama 20 kama Waziri.

Katika kipindi chake cha urais muda huo kuanzia 'go' taa kuwaka kijani kupitia vibaraka wao wakiongozwa na lissu walianza kumpiga vita kwa pupa uongo na lugha za kishenzi kabisa. Yote ilikuwa mshtuko na hamaki kwa kujua magufuli ni kiongozi imara na mtetezi mkubwa wa maslahi ya umma. Ni mtu muadilifu hahongeki hivyo kua mtu hatari kwa ubwanyenye na unyonyaji wa nguvu kazi ya wavuja jasho.

Wapinga maendeleo wakiongozwa na CHADEMA wamekua wanamuombea kila janga magufuli hadi wamekua wanamwombea kifo. Tuliona kina lema wakimtabiria kifo kama hataacha kuwapambania wanyonge.

Magufuli alipotwaliwa na mola wake adui zake wakiongozwa na wanachadema walionyesha furaha hadharani na kuamini mungu amejibu maombi yao. Kwa imani kwamba mungu amewaletea samia bila shaka wakampelekea fitna nyingi na mama kumtupa sabaya mtumishi mwaminifu wa umma gerezani.

Hii kesi ya sabaya kwa waliyoipanga lengo lao ni kumchafua Magufuli. Leo fisadi na wakwepa kodi aliyotumwa sabaya kuwafuatilia ndio wanamuita Sabaya jambazi. Hili halitakubaliwa na wananchi kama walivyokataa pale jaribio la kumchafua baba wa taifa lilifanyika na wapinga maendeleo.

Mahakama ipo/zipo haki ya sabaya itapatikana na magufuli atabakia daima kwenye mioyo ya watanzania.

Wanataka kufuta legacy ya Magufuli katika mioyo ya watu kwa kumtumia sabaya.
 
Back
Top Bottom