Mtazamo wangu binafsi, Kesi ya Lengai Ole Sabaaya imechukua U-Turn kumchafua Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwageuka wafuasi wa Hayati Magufuli katika Serikali yake.
Kwanini nasema hivo?
Kwa Lengai Ole Sabaaya kuwataja mahakamani;
1) Hayati Magufuli (Huyu ana Kinga kikatiba kwasababu alikua Rais).
2) Dk Mpango (Hana kinga Kisheria kwasababu alikua Waziri Wa Fedha Wakati Jinai Inatendwa).
3) Prof Luoga (Hana Kinga Kisheria - Gavana BOT)
Amewataja kama waambatanaji katika makosa ya jinai alioyafanya (Accomplice & Accessory To The Crime - Kisheria wana hatia na adhabu ni sawa na mtendaji wa jinai).
Hayati Magufuli alikua Rais na anakinga ya Kikatiba kushtakiwa, hao wawili hawana kinga kikatiba katika hayo makosa ya jinai jijini Arusha (Dk Mpango na Prof Luoga) na kisheria ni Accomplice & Accessory to the Crime.
Hoja za kumchafua na kumpima uadilifu Rais Samia Suluhu;
● Je, Wata wajibishwa kisheria na katiba ili Mahakama iachwe ifanye kazi yake ya kutoa hukumu dhidi yao kama wana hatia au hawana, au watawekwa juu ya sheria na katiba???
● Je, Ole Sabaaya ametumika na wanaompinga Rais SSH ndani ya CCM kumtikisa Rais kwa kuwatia kwenye Jinai watu muhimu katika Serikali yake???
● Je, ndio miongoni mwa njia wanayotumia wana CCM waliokua wafuasi wa Hayati Magufuli aliowaacha kwenye Serikali yake, na wakaamua kumpinga Rais SSH kwenye Chanjo za Covid wazi wazi kama njia ya kuonesha dunia yeye ni muumini wa
"Double Standard kwenye kuwajibisha watu kisheria".
Rais Samia Suluhu alipo hojiwa na BBC, alisema - Freeman Mbowe aachwe awajibishwe kisheria na mahakama ndio itakayoamua juu ya hatia yake dhidi ya jinai anayo tuhumiwa nayo.
JE, kwa Prof Luoga na Dk Mpango nao watawajibishwa kisheria kama waambatanaji wa hayo makosa ya Ole Sabaaya na mahakama itaachwa kuamua juu ya hatia zao, au watawekwa juu ya katiba ya nchi kwasababu ni watu muhimu katika serikali yake!
Habari Wana JF, Mnamo tarehe 13 Agosti 2021, Mtuhumiwa Ole Sabaaya katika kesi ya jinai ya kupora fedha kwa kutumia silaha mkoani Arusha inayomkabili, yeye na wenzake, milango ya utetezi iliwekwa wazi kwa watuhumiwa ili kuanza kutoa ushahidi wa kujitetea. Hii ilikua mara baada ya Mahakama kutoa...