Arusha: Makada 5 wa CHADEMA wakamatwa wakidaiwa kuingilia mifumo ya mawasiliano ya kibenki ili kuiba fedha kwa ajili ya Uchaguzi

Mmmmh yani kuingilia mifumo ya benki ni rahisi kiasi hicho? Yaani uingie kwenye mfumo wa benki na ki laptop chako 'intel duo core'...uchote fedha uhamishie kwenye account yako na ukazitoe hapa hapa TZ....Niliwahi kutumiwa 5mil. baada ya muda mfupi nikatumiwa tena 5mil...nilipigiwa simu na NMB
 
Wanachama wanafuata tabia za mwenyeki wao mpendwa. Chama kimejaa wapigaji.
 
Kamanda Hamduni upo duni kweli, unakubali kuharibu image ya jeshi la polisi kubambika watu kesi ya jinai!? Kuingilia mifumo ya kibenki ni kosa la uhujumu uchumi.
 
Eti kosa ni kutaka kuingilia mifumo ya kibenki na kuiba fedha za uchaguzi!😁😁😁😁,hili jeshi kwakweli linafanya propaganda za kipumbavu kabisa!Hivi mnatuona watanzania ni wajinga?
Kwanini waseme wanataka kuiba fedha kwa ajili ya uchaguzi?Watuhumiwa wamekiri hivyo?Pumbav kabisa hili jeshi
 
Makada watano CHADEMA mbaroni kwa tuhuma za makosa mtandaoni

MAKADA watano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Arusha, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuingilia mifumo ya mawasiliano ya kibenki.

Vilevile, wanatuhumiwa kuendesha mafunzo batili yanayolenga kutenda uhalifu wa kijinai katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 28 mwaka huu.

Jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Salum Hamduni, alithibitisha jeshi hilo linawashikilia watu hao baada ya kuwakamata Oktoba 5 mwaka huu majira ya saa 11:45 jioni.

“Polisi ilipokea taarifa kuwapo kwa watu hao kwenye ofisi binafsi za aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini (Godbless Lema) zilizoko Mtaa wa Esso, ambako kumekuwa na kawaida ya watu kukusanyika kuendesha mafunzo ya kulenga kutenda uhalifu wa kijinai unaohusishwa na kuingilia mifumo ya mawasiliano ya kibenki.

“Sasa, baada ya taarifa hizo kupokewa, wapelelezi walifika eneo hilo kufanya uchunguzi. Askari wapepelezi walikwenda kwa nia ya kufanya upekuzi kwenye ofisi hizo na kukamata watu wote.

“Kumekuwa na taarifa ambazo zilikuwa zinazagaa kwenye mitandao ya kijamii watu wasiofahamika wamevamia, hapana! Ni Jeshi la Polisi na askari wake walikuwa wamevaa 'uniform' (sare)," alisema.

Kwa mujibu wa Kamanda Hamduni, waliokamatwa ni mdogo wake na Lema aitwaye Nelson Lema (31), mkazi wa Arusha ambaye ni mfanyabiashara.

Wengine ni Lazaro Viola (46), ambaye Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Arusha, mfanyabiashara Wilbad Tarimo, Joshua Lukumay, mfanyabiashara na Mohamed Omar (45) ambaye ni wakala wa mabasi.

Alisema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kuhusiana na taarifa hizo na inakusudia kuchukua hatua nyingine za kisheria kwa kadri ambavyo ushahidi utapatikana.

Katika taarifa yake, Kamanda Hamduni, alisema taratibu za dhamana kwa watuhumiwa hao ziko wazi na zinaendelea kushughulikiwa, hivyo taratibu zikikamilika watapewa haki hiyo.

Alisema Jeshi la Polisi halijihusishi na siasa na kwamba wajibu wa jeshi hilo umeelezwa kwenye katiba.

KAULI YA LEMA

Akizungumzia tukio hilo katika mkutano wake na waandishi wa habari jana jijini hapa, mgombea ubunge wa Arusha Mjini ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Lema, alilaani kitendo akidai kuwa ni kinyume cha sheria.

Alisema askari polisi zaidi ya 30 walifika katika ofisi hizo huku wakiwa wamebeba silaha za moto na kufanya upekuzi kwenye ofisi hizo kwa zaidi ya saa tatu.

Kwa mujibu wa Lema, askari polisi hao walidai kuwa ofisini huko kulikuwa na wahamiaji haramu kutoka mataifa ya Kenya na Israel.

Lema alidai kuwa vitu vilivyochukuliwa na polisi ni pamoja na nyaraka za siri za chama, simu nane na kompyuta mpakato mbili.

Lema alisema: “Juzi majira ya saa 6:30 jioni, nilipokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Arusha Mjini, kwamba maofisa wa Jeshi la Polisi walifika katika ngome hiyo na kuwakamata viongozi watano wa chama na kuchukua baadhi ya vifaa na nyaraka.

Alisema kuwa kutokana na polisi kuwakosa wahalifu waliodai kuwa wapo kwenye ofisi hizo, walibadilisha maelezo na kusema kuwa watu hao walikuwa kwenye mpango wa kuingilia mifumo ya kibenki kwa ajili ya kujipatia fedha za kuendesha uchaguzi.

Chanzo: IPP Media
....kinacho shangaza kwenye vyombo vyetu vya usalama nikumkamata MTU wakiwa hawajatengeneza ushahidi au hawana ushahidi na ukifika polisi utapigwa mpaka ukubali hats kama hau husiki utataja hats watu ambao hawakuhusika ili ukiepuke kipigo skuhizi kuna usemi unasema polisi hatu kataagi tuna kataa mahakamani"
 
Habari zimezagaa mjini ndiyo Nini hapo panahitaji ufafanuzi.Tuseme benki sijui ipi walilalamika kuwa mfumo wao umeingiliwa kwa fedha zinahamia kwenye akaunti ya chadema dah Mimi sielewi bhana.
 
Marehemu Sitta aliziita siasa za maji taka. Kule Singida mgombea wa ubunge wa CHADEMA alivamiwa usiku nyumbani kwake na kupigwa eti kwa vile kulikuwa na silaha nnyumbani kwake. Alipopekuliwa, wakamkuta na kisu na panga nyumbani kwake. Wakamkata na kumpeleka kituoni kwa kukutwa na kisu na panga nyumbani kwake! bi siasa za maji taka kweli kweli.
 
Mkuu kabisa napenda sana niwe katika kundi la wanao jielewa, naomba unisaidie sifa zao ili na mimi nijielewe. Nisaidie tafadhali . . . . .
1.Mifumo ya kibenki haijaingiliwa ila wanatuhumiwa kuwa na nia ya kutaka kuingilia mifumo ya kibenk!
2.Hata kosa la wizi halijatendeka wala kuingilia hiyo mifumo ila tayari RPC anajua fedha zilizotaka kuibiwa ni kwa ajili ya uchaguzi!
3.Kwanini Lema ambaye ndio mkuu wa kambi hiyo ya uchaguzi hajakamatwa maana kama mipango ni ya kutenda uhalifu basi Lema ndiye mpishi!

Wadanganyeni wapumbav wasiojielewa,huu ni upuuzi kama upuuzi mwingine!
Polisi Tanzania ni vinara wa kubambikizia kesi!Ni aibu kwa jeshi kukiingiza kwenye siasa za majitaka,shwain!
 
Mmmmh yani kuingilia mifumo ya benki ni rahisi kiasi hicho? Yaani uingie kwenye mfumo wa benki na ki laptop chako 'intel duo core'...uchote fedha uhamishie kwenye account yako na ukazitoe hapa hapa TZ....Niliwahi kutumiwa 5mil. baada ya muda mfupi nikatumiwa tena 5mil...nilipigiwa simu na NMB
Yaani wanatuhumiwa kwa kutaka kuingilia mifumo ya kibenki na sio kuingilia mifumo ya kibenki!Hapa ndipo unaona ukilaza wa jeshi letu la polisi!Wanatumika hata kujidhalilisha wao wenyewe!
Angalia sasa hao watuhumiwa,hakuna expert wa IT hapo!
 
Makada watano CHADEMA mbaroni kwa tuhuma za makosa mtandaoni

MAKADA watano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Arusha, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuingilia mifumo ya mawasiliano ya kibenki.

Vilevile, wanatuhumiwa kuendesha mafunzo batili yanayolenga kutenda uhalifu wa kijinai katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 28 mwaka huu.

Jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Salum Hamduni, alithibitisha jeshi hilo linawashikilia watu hao baada ya kuwakamata Oktoba 5 mwaka huu majira ya saa 11:45 jioni.

“Polisi ilipokea taarifa kuwapo kwa watu hao kwenye ofisi binafsi za aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini (Godbless Lema) zilizoko Mtaa wa Esso, ambako kumekuwa na kawaida ya watu kukusanyika kuendesha mafunzo ya kulenga kutenda uhalifu wa kijinai unaohusishwa na kuingilia mifumo ya mawasiliano ya kibenki.

“Sasa, baada ya taarifa hizo kupokewa, wapelelezi walifika eneo hilo kufanya uchunguzi. Askari wapepelezi walikwenda kwa nia ya kufanya upekuzi kwenye ofisi hizo na kukamata watu wote.

“Kumekuwa na taarifa ambazo zilikuwa zinazagaa kwenye mitandao ya kijamii watu wasiofahamika wamevamia, hapana! Ni Jeshi la Polisi na askari wake walikuwa wamevaa 'uniform' (sare)," alisema.

Kwa mujibu wa Kamanda Hamduni, waliokamatwa ni mdogo wake na Lema aitwaye Nelson Lema (31), mkazi wa Arusha ambaye ni mfanyabiashara.

Wengine ni Lazaro Viola (46), ambaye Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Arusha, mfanyabiashara Wilbad Tarimo, Joshua Lukumay, mfanyabiashara na Mohamed Omar (45) ambaye ni wakala wa mabasi.

Alisema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kuhusiana na taarifa hizo na inakusudia kuchukua hatua nyingine za kisheria kwa kadri ambavyo ushahidi utapatikana.

Katika taarifa yake, Kamanda Hamduni, alisema taratibu za dhamana kwa watuhumiwa hao ziko wazi na zinaendelea kushughulikiwa, hivyo taratibu zikikamilika watapewa haki hiyo.

Alisema Jeshi la Polisi halijihusishi na siasa na kwamba wajibu wa jeshi hilo umeelezwa kwenye katiba.

KAULI YA LEMA
Akizungumzia tukio hilo katika mkutano wake na waandishi wa habari jana jijini hapa, mgombea ubunge wa Arusha Mjini ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Lema, alilaani kitendo akidai kuwa ni kinyume cha sheria.

Alisema askari polisi zaidi ya 30 walifika katika ofisi hizo huku wakiwa wamebeba silaha za moto na kufanya upekuzi kwenye ofisi hizo kwa zaidi ya saa tatu.

Kwa mujibu wa Lema, askari polisi hao walidai kuwa ofisini huko kulikuwa na wahamiaji haramu kutoka mataifa ya Kenya na Israel.

Lema alidai kuwa vitu vilivyochukuliwa na polisi ni pamoja na nyaraka za siri za chama, simu nane na kompyuta mpakato mbili.

Lema alisema: “Juzi majira ya saa 6:30 jioni, nilipokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Arusha Mjini, kwamba maofisa wa Jeshi la Polisi walifika katika ngome hiyo na kuwakamata viongozi watano wa chama na kuchukua baadhi ya vifaa na nyaraka.

Alisema kuwa kutokana na polisi kuwakosa wahalifu waliodai kuwa wapo kwenye ofisi hizo, walibadilisha maelezo na kusema kuwa watu hao walikuwa kwenye mpango wa kuingilia mifumo ya kibenki kwa ajili ya kujipatia fedha za kuendesha uchaguzi.

Chanzo: IPP Media
Watatengeneza sana kesi za kuwapa Chadema. Ila mwisho ya haya yote ni October 28.
 
Yaani wanatuhumiwa kwa kutaka kuingilia mifumo ya kibenki na sio kuingilia mifumo ya kibenki!Hapa ndipo unaona ukilaza wa jeshi letu la polisi!Wanatumika hata kujidhalilisha wao wenyewe!
Angalia sasa hao watuhumiwa,hakuna expert wa IT hapo!
Nimebaki nashangaa tu...ujaribu kuhack bank? Bank..bank...nani angekuwa maskini sasa
 
CCM na jeshi la polisi wamelaaniwa.
 
Back
Top Bottom