Arusha: Masheikh 6 wahukumiwa kunyongwa hadi kifo

Safi sana.......huwezi kuua binadamu mwenzako kwa akili za kijinga hata kidogo....Sijui binadam wengine wanatoaga wapi ubavu wa kudhulumu uhai wa binadam wenzao!!

Ukiuwa kwa upanga na wewe utauliwa kwa upanga.......

Waafrika tunachukiana kwa sababu ya madini ya wazungu na waarab huo ni upuuz kama upuuz mwengine
 
ARUSHA: Masheikh 9 miongoni mwa wanaoshikiliwa kwa zaidi ya Miaka 10 katika Gereza Kuu la Kisongo wamesomewa Mashtaka katika Mahakama ya Kuu ya Kanda

Masheikh 6 kati yao wamekutwa na hatia ya kulipua Kanisa Katoliki la Parokia ya Mtakatifu Joseph #Olasiti Mwaka 2013 na kusababisha madhara makubwa hivyo kuhukumiwa kunyongwa

Waliohukumiwa ni Imam Jaafar Hashima Lema, Yusuf Ali Huta, Ramadhani Hamadi Waziri, Abdul Hassa Masta, Kassim Idrisa na Abashari Hassan Omari na waliochiwa huru ni Abduli Humud Wagoba, Abdurahmani na Amani Mussa Pakasi (ambaye amerejeshwa gerezani kwa kosa lingine)

Soma Arusha: Masheikh 6 wahukumiwa kunyongwa hadi kifo

#JamiiForums #JFMatukio
 
Hivi kweli kesi inakaa zaidi ya miaka kumi mbona hatari hii? Yani wanakuachia wanasema hauna hatia na hapo ushakaa zaidi ya miaka 10? Kwakweli sjui upelelezi wetu ukoje ....
 
Your browser is not able to display this video.
 
Katika kulipua kanisa hiyo watu wangapi walipoteza maisha, kama hamna alio kufa wsmeonea, na soon watakua huru uonevu hauwezi kufanikiwa
Walikufa waumini watatu. Hawa wanastahili kunyongwa hasa maana siyo mashekh hao wala hawa wakilishi Uislam zaidi ya kuwa walitanguliza tamaa zao tu za dunia kwa ujira wa vipande vya fedha.

Namsihi Rais Samia asaini mapema wanyongwe hawa hadi wafe ili haki ya marehemu iwe served.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…