Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Sheria za kishetani.Tangu lini mtu aliyeripua jengo ambalo hakuna madhara yaliyotokea akahukumiwa kifo.SHURA YA MAIMAMU TANZANIA
MASHEIKH SITA 6 WAHUKUMIWA KUNYONGWA ARUSHA LEO
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo tarehe 12/12/2023, imewasomea hukumu Masheikh tisa miongoni mwa wale wanaoshikiliwa na Serikali kwa zaidi ya miaka kumi katika Gereza Kuu la Kisonge Mkoani Arusha.
Masheikh hao wanatuhumiwa na Serikali kwa Ugaidi wa kulipua Kanisa Katoliki la Ole sita mkoani Arusha mwaka 2013.
Akisoma hukumu hiyo Jaji Nkwabi aliwaachia huru Masheikh watatu ingawa mmoja miongoni mwao amerejeshwa jela kwa sababu ya kukabiliwa na tuhuma nyingine.
Walioachiwa huru ni: Abduli Humud Wagoba, Abdurahmani na Amani Mussa Pakasi (ambaye amerejeshwa gerezani).
Aidha Jaji Nkwabi alionesha kuridhishwa na ushahidi wa Polisi kwamba Masheikh sita katika shauri hilo akiwemo imamu mkuu wa Msikiti mashuhuri Masjid Quba Arusha, Sheikh Jaafar Hashim Lema waliripua Kanisa Katoliki na kusababisha madhara makubwa.
Kwa sababu hiyo Jaji Nkwabi aliamua kuwahukumu adhabu kali ya kunyongwa mpaka kufa.
Masheikh hao waliokaa gerezani kwa zaidi ya miaka kumi na hatimaye kuhukumiwa kifo ni:
1. Imam Jaafar Hashima Lema.
2. Yusuf Ali Huta
3. Ramadhani Hamadi Waziri.
4. Abdul Hassa Masta.
5. Kassim Idrisa. Na-
6. Abashari Hassan Omari.
Masheikh hao pamoja na wenzao kumi walio hukumiwa kunyongwa hivi karibuni mkoani Tanga, watanyongwa baada ya Rais Samia Suluhu Hassani kutia saini.
Pia, soma;
Mlipuko mkubwa watokea kwenye Kanisa Katoliki Arusha, watu kadhaa wajeruhiwa
Huyo jaji atakuwa ni padre wa hilo kanisa au mfuasi wake.
Jengine hakuna shambulio linalofanywa la kulipua likafanywa na kikundi kama hicho.Kubwa hawahusiki na kama kuna mtu alifanya uhuni huo atakuwa alitumwa na alfanya peke yake halafu hao masheikh wakashikwa na wapinzani wa imani yao.
Raisi Samia hawezi kutia saini hukumu hiyo ya kishetani.Akikosea atakuwa ameingia mtego wa kijinga sana.