ARUSHA: Meya, wamiliki wa shule, paroko na Waandishi, wakamatwa na Polisi Shuleni, wanyimwa dhamana

ARUSHA: Meya, wamiliki wa shule, paroko na Waandishi, wakamatwa na Polisi Shuleni, wanyimwa dhamana

Only in Tanzania unakamatwa ukiwa kwenye majukumu unapelekwa polisi na baadaye unaambiwa tulikupa lift tu.


Labda wameshazichukua hizo rambirambi na kuzipeleka kwa Bwana mkubwa kwani ndio mshika bakuli na mgawaji.

Oh my foot.


Jeshi la Polisi limesema, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ndiye aliyetoa amri ya kukamatwa kwa walioenda kutoa salamu za rambirambi katika Shule ya Msingi ya Lucky Vincent leo.

====
UPDATES:

Waandishi zaidi ya 8 waliokamatwa Arusha leo ktk utoaji rambirambi kwa Lucky Vicent wameachiwa, Polisi wawaambia waliwapa lift tu.
 
Only in Tanzania unakamatwa ukiwa kwenye majukumu unapelekwa polisi na baadaye unaambiwa tulikupa lift tu.


Labda wameshazichukua hizo rambirambi na kuzipeleka kwa Bwana mkubwa kwani ndio mshika bakuli na mgawaji.

Oh my foot.

Utachukua pesa za watu bila kupewa??Naona labda alitaka kuwepo kwenye hilo group,kutokuwepo kwake kumemuumiza sana.Siunajua jana walimkimbia kwenye msiba baada ya kutaka kupeleka siasa makaburini?
 
eti waliwapa lifti kwani walienda kwa miguu. mwaka huu number inasomeka tena kwa herufi kubwa
 
Waandishi wa habari waliokamatwa Arusha leo katika utoaji wa rambirambi shule ya Lucky Vincent wameachiwa, polisi waliwaambia waliwapa lift tu.
Kwa hiyo wamewapa lift kwenda kukusanya habari, au lift ya kuwapeleka kituoni, amabapo hakukuwa na habari wala ratiba ya kuwa hapo?
 
Kuna nini Arusha? Yaani hakuna kabisa jinsi ya kupandisha chati wapinzani hata watu wafariki? Kwa nini msipande Mlima Meru au kulala na masimba Serengeti ili tuwaone mashujaa, kwa nini mnasubiri misiba? Lilianzia kule Usukumani kwa marehemu Mawazo tukaona Mnyika na Mwalimu na Lowassa na Mbowe na Sumaye wakipigania maiti mortuary Bugando! Mkakataliwa na Wanyamwezi sasa imebaki Arusha. Kuna nini Arusha? Haya ndiyo mabadilikoooooo!!
 
Mambo kama haya ndiyo huchochea matukio ya.kigaidi kama ya huko Rufiji viongozi wa CCM wanapoifanyia jamii mabaya watu huamua kulipiza kwa vibaraka wao polisi na viongozi wa ngazi za chini. Viongozi mjiangalie mchawi sio muuaji wachaji ndio ninyi. Mtapukutika kibao mwaka huu msipobadilika reaction yake huenda kwa raia. Sifurahii haya.lkn why itokee kwa viongozi wa CCM na polisi. Jibu ni upumbavu kama wa kina Mrisho Gambo. Mimi raia mtiifu kabisa msiniteke aisee
 
Mstahiki Mayor wa Jiji , Paroko , Mchungaji , Waandishi wa habari 7 , wamekamatwa leo na Jeshi la Polisi wakiwa Shuleni Lucky Vicent ambako Mayor alialikwa na Umoja wa Shule binafsi Tanzania , waliopenda kutoa rambi rambi moja kwa moja kwa wafiwa badala ya kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa .

Wazazi waliokuwa hapo wamepatwa na taharuki kubwa baada ya kuona viongozi hao wanachukuliwa bila sababu yoyote ya msingi , mpaka sasa wako Polisi wanaambiwa walikuwa na mikusanyiko isiyo halali .

Nafikiri tunachoka sana . Mungu mpaka lini mambo haya ?

======

UPDATES: 1

Waandishi waliokamatwa na jeshi la polisi Arusha kwa madai tulihudhuria kikao ambacho hakikua na kibali katika shule ya Luck vincent ambapo shirikisho la wamiliki wa shule binafsi walikuwa wanaendwa kutoa rambirambi. Sisi tulipata taarifa tukaenda kufanya kazi.

1 .Godfrey Thomas -ayo tv

2.King Alphonce Saul Kusaga

3.Filbert Emmanuel -mwananchi

4.Husein Tuta ITV

5.Joseph Ngilisho -Sunrise radio

6.Geofrey Stephen -Radio 5

7.Janeth Mushi -Mtanzania

8.Zephania Ubwani -The Citizen

9.Elihuruma Yohani -mwakilishi wa Tanzania Daima

10.Idd Uwesu - Azam Tv

UPDATES; 2

Waandishi wa habari waliokamatwa Arusha leo katika utoaji wa rambirambi shule ya Lucky Vincent wameachiwa, polisi waliwaambia waliwapa lift tu.

UPDATES: 3

Kaimu RPC wa Arusha Yusuph Ilembo amesema watu wote waliokamatwa leo shuleni Lucky Vincent ni utekelezajiwa wa agizo la RC wa Arusha Mrisho Gambo

UPDATES;
Wamiliki wa Shule Binafsi walioenda kutoa rambirambi katika Shule ya Msingi ya Lucky Vincent wakiwa na waandishi wa habari wamewekwa chini ya ulinzi na polisi shuleni.

Mwandishi wetu ambaye yuko eneo la tukio hivi sasa ameeleza kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya Arusha ambaye hajamtaja jina amewaambia kuwa wako chini ya ulinzi kwa kosa la kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria.

Mwandishi wetu ameeleza kuwa katika msafara huo pia yupo Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro, viongozi wa dini, wazazi waliofiwa na waandishi kama 10.


Chanzo: Mwananchi

Come on Lema

As a shrewd politician do something stop posting these things

Show that you can win that battle against good for nothing leaders....


Your posts in social media can not change anything since you are leading people with different characters, level of education don't forget you are leading poor people they don't even understand themselves
 
*KUKAMATWA VIONGOZI CHADEMA ARUSHA*


*Na Felix Mushi,Arusha*

Niko hapa eneo la tukio Shule ya Msingi Lucky Vicent iliyopo Olasit Jijini Arusha, Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha, na Viongozi wengine wa Chadema wamekamatwa wakiwa kwenye mkutano na wazazi wa watoto waliofariki kwenye ajali hiyo.

Katika kikao hicho Meya wa Jiji alianza kwa kutoa pole kwa wafiwa na kuwaeleza kuwa ametumwa na Mbunge ili kuwapa pole za kipekee kwa msiba huu na zaidi ameelekezwa kuja kuwajengea ujasiri wazazi ili waendelee kudai fedha zilizoliwa na wajanja.

Akawaeleza kuwa wao kama Chama makini wako pamoja na wafiwa kwa hali zote na kwamba lazima haki itashinda. Pia aliwafafanulia kuwa ni jambo la aibu kuona wadau mbalimbali wametoa fedha lakini watu wachache wanakula michango hiyo lakini wanaachwa.

Kabla hajaendelea na maelezo hayo, alisimama mzazi aliyejulikana kwa jina moja la mama Ivo ambaye alimuuliza Meya juu ya fedha milioni 10 ambazo Mbunge na uongozi wa CHADEMA waaliahidi walipokuja kuwapa pole siku ya msiba kwamba ni vyema wangezitoa ziwasaidie kuliko kuendelea kuwaeleza juu ya wizi wa rambirambi ambazo hata hawana uchungu nazo. Aidha alumina Meya Alasdair kurejeshewa fedha za ada ambazo walilipa shuleni siku moja kabla ya ajali kwani ni haki yao.

Swali hilo liliamsha shangwe na vigelegele kutoka kwa baadhi ya wazazi huku wengine wakiguna kichinichini. Hata hivyo Meya aliwaeleza kuwa fedha ambazo wao kama CHADEMA waliziahidi wasiwe na hofu watazipata lakini hiyo siyo agenda iliyowaleta leo! Akawaomba wamvumilie kwani yeye na viongozi wenzake watatafuta siku muafaaka ambayo Mbunge atakuwepo ili awakabidhi mwenyewe. Alitumia nafasi hiyo pia kuwasihi wafiwa wapuuze maneno ya mtaani kwamba CHADEMA hawajachangia chochote zaidi ya kufanya siasa Kwenye mitandao. Akawahakikishia kuwa fedha hizo watazipata kabla ya tarehe 21 Mei.

Hata hivyo maelezo haya yalionekana kutojitosheleza kwa baadhi ya wazazi ambao waliendelea kuguna na wengine wakizomea huku wengine wakionyesha kufurahishwa na majibu hayo na wakizomea kwa nguvu. Fujo za kutosikilizana zilipoendelea iliymlazimu mzazi mmoja kuwapigia simu polisi kuja kudhibiti sintofahamu iliyojitokeza. Naamini watakuwa wanaendelea kutoa maelezo huko!

Hasira za Baadhi ya wazazi hao pamoja na walimu ni kuchoshwa na kile walichokiona ni usanii wa baadhi ya viongozi kuendelea kutumia msiba huo kama ngao ya siasa huku wakiwa hawatoi michango waliyoahidi zaidi ya kupiga danadana.
____
Nitaendelea kuwajuza kinachoendelea juu ya Muvi hii nzuri!
 
Si ni mkuu wa usalama wa mkoa au? Labda mumulize sababu, naamini atakuwa na sababu zinazoeleweka juu ya hili tatizo.
RC ni mwenyekiti wa kamati ya Usalama ya Mkoa. Siyo Mkuu , Mkuu ni RPC kwa kuwa ndiye mwenye Jeshi hapo mkoani. Ndiyo kisa Uongozi unahitaji watu waliopevuka kiakili siyo vijana wa miaka 21.Hawa wanakuwa bado wanawauliza wazazi wao majibu kuhusu maisha!
 
  • Thanks
Reactions: OTG
Hivi hii serikali kwa nini hawajifunzi? La Kagera walipigiwa sana kelele. Nilidhani sasa wataacha kuchezea rambirambi za wafiwa, lakini wapi? Mnajiabisha jamani. Kwa nini wanataka rambirambi ipitie kwa mkuu wa mkoa? Hakika hii serikali ina mapepo, sio kwa hivi vituko!!!
 
Hakika watendaji wa mtukufu wamekosa busara ktk hili.
 
Hekima na busara ni ziro kabisa kwa hawa watu... wakati maji yana chemka usiweke mkono subiri yatapoa tu! Mavurugu hayana faida!
 
Back
Top Bottom