ARUSHA: Meya, wamiliki wa shule, paroko na Waandishi, wakamatwa na Polisi Shuleni, wanyimwa dhamana

ARUSHA: Meya, wamiliki wa shule, paroko na Waandishi, wakamatwa na Polisi Shuleni, wanyimwa dhamana

Meya wa jiji la Arusha muda huu amekamatwa na polisi akiwa katika shule ya Lucky Vincent! Sababu haswa hazijulikani.

Meya wa Arusha,viongozi wa dini na waandishi wa habari wamekamatwa na polisi muda huu eneo la shule ya Lucky Vincent,walikoenda kutoa rambirambi!

=====

Wamiliki wa Shule Binafsi walioenda kutoa rambirambi katika Shule ya Msingi ya Lucky Vincent wakiwa na waandishi wa habari wamewekwa chini ya ulinzi na polisi shuleni.

Mwandishi wetu ambaye yuko eneo la tukio hivi sasa ameeleza kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya Arusha ambaye hajamtaja jina amewaambia kuwa wako chini ya ulinzi kwa kosa la kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria.

Mwandishi wetu ameeleza kuwa katika msafara huo pia yupo Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro, viongozi wa dini, wazazi waliofiwa na waandishi kama 10.


Chanzo: Mwananchi
Kweli nimeamini sikio la kufa halisikii dawa yaani ccm inajifia hivihivi!
 
Mstahiki Mayor wa Jiji , Paroko , Mchungaji , Waandishi wa habari 7 , wamekamatwa leo na Jeshi la Polisi wakiwa Shuleni Lucky Vicent ambako Mayor alialikwa na Umoja wa Shule binafsi Tanzania , waliopenda kutoa rambi rambi moja kwa moja kwa wafiwa badala ya kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa . Wazazi waliokuwa hapo wamepatwa na taharuki kubwa baada ya kuona viongozi hao wanachukuliwa bila sababu yoyote ya msingi , mpaka sasa wako Polisi wanaambiwa walikuwa na mikusanyiko isiyo halali .

Nafikiri tunachoka sana . Mungu mpaka lini mambo haya ?
 
Hii ni nchi ya ajabu sana ila kuna miroboti kazi kupiga makofi na kusifu.

Mwisho wa siku hata wanafamilia kukutana/kukaa bazani itakuwa ni mkusanyiko usio halali.

Bora JK hakuwa vuguvugu mzee wa watu ingawa nae alikuwa na mapungufu yake lakini haya ya rambirambi hatukuwahi kuyasikia enzi zake.
 
Kipindi ambacho watoto wetu wanahitaji wataalam wa tiba za saikolojia ili kuwapa nasaha baada ya kupoteza marafiki zao, wanasiasa wapumbavu wanatafuta umaarufu!
Wale watoto akili zao hazijakaa vizuri, ugeni wa watu ambao sio wale waliozoeleka hapo shuleni vinaamsha majonzi upya! Wanasiasa acheni uharamia na tamaa!
Nimetafuta tusi zito limekosa,........Mungu nipe moyo wa uvumilivu!
 
nafikiri alikuwa anafatilia ukweli wa rambirambi,hakuna rc wa arusha alikuwa mbabe kama mulongo magesa,leo hii anaenda kwa shubash patel kuomba ajira....gambo you are exception and your downfall will be quick and heavy
mkuu ya kweli hayo ya mulongo?
 
Kwa nini tunashindwa kutumia akili kidogo tu?

Kwani wafiwa wakipewa mkononi na walioko mbali shule ikainjinia mpango wa kuwapelekea tutapungukiwa na nini?
 
Back
Top Bottom