ARUSHA: Meya, wamiliki wa shule, paroko na Waandishi, wakamatwa na Polisi Shuleni, wanyimwa dhamana

Mstahiki Mayor wa Jiji , Paroko , Mchungaji , Waandishi wa habari 7 , wamekamatwa leo na Jeshi la Polisi wakiwa Shuleni Lucky Vicent ambako Mayor alialikwa na Umoja wa Shule binafsi Tanzania , waliopenda kutoa rambi rambi moja kwa moja kwa wafiwa badala ya kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa .

Wazazi waliokuwa hapo wamepatwa na taharuki kubwa baada ya kuona viongozi hao wanachukuliwa bila sababu yoyote ya msingi , mpaka sasa wako Polisi wanaambiwa walikuwa na mikusanyiko isiyo halali .

Nafikiri tunachoka sana . Mungu mpaka lini mambo haya ?
=====

Wamiliki wa Shule Binafsi walioenda kutoa rambirambi katika Shule ya Msingi ya Lucky Vincent wakiwa na waandishi wa habari wamewekwa chini ya ulinzi na polisi shuleni.

Mwandishi wetu ambaye yuko eneo la tukio hivi sasa ameeleza kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya Arusha ambaye hajamtaja jina amewaambia kuwa wako chini ya ulinzi kwa kosa la kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria.

Mwandishi wetu ameeleza kuwa katika msafara huo pia yupo Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro, viongozi wa dini, wazazi waliofiwa na waandishi kama 10.

Chanzo: Mwananchi
Eleza vizuri lazima kuna sababu sio kuleta mambo nusunusu.
 
Waandishi wa habari jijini Arusha wamekamatwa na Polisi muda huu wakiwa shule ya Lucky Vincent, waandishi hao walikuwa na Meya pamoja na viongozi mbalimbali wa dini shuleni hapo.Waandishi hao wamepelekwa kituo cha polisi.

Habari zaidi zitafuata
Hadi sasa haijajulikana chanzo cha kukamatwa kwao kwani walikuwa kwenye majukumu yao ya kazi pamoja na Meya wa jiji na viongozi wa dini.

Majukumu yao ya kazi!! ngoja wakaeleze huko walikuwa wanafanya kazi gani pale shuleni.
 
Nilitaka kwenda kutoa. Lakini kwa hali hii siende?
 
Wacha wakamatwe wanataka kufanya siasa msibani
 
Kama ndo waandishi hawa hawa wachochezi inatakiwa wapigwe na viboko kabisa...alafu walale central wiki mbili wakila pumba na maji...hakuna kulemba hapa kazi tuuuuuuuuuuuuuuuuu
Hapa kuiba rambirambi tu sio eeh
kwaio mnaomba jwa udi na uvumba ajali nyingine itokee ili muendele kufaidi rambirambi
 
Labda wanataka kodi kwenye hiyo 18 milioni.!

Hii nchi bwana.
 
Hapa kuiba rambirambi tu sio eeh
kwaio mnaomba jwa udi na uvumba ajali nyingine itokee ili muendele kufaidi rambirambi
Hayo ni maombi yako.....ili upate kiki ya mtaani....
 
Kama vipi na yeye asusiwe na vyombo vya habari. Ananyanyasaje waandishi wa habari bana!
 
Mstahiki Mayor wa Jiji , Paroko , Mchungaji , Waandishi wa habari 7 , wamekamatwa leo na Jeshi la Polisi wakiwa Shuleni Lucky Vicent ambako Mayor alialikwa na Umoja wa Shule binafsi Tanzania , waliopenda kutoa rambi rambi moja kwa moja kwa wafiwa badala ya kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa .

Wazazi waliokuwa hapo wamepatwa na taharuki kubwa baada ya kuona viongozi hao wanachukuliwa bila sababu yoyote ya msingi , mpaka sasa wako Polisi wanaambiwa walikuwa na mikusanyiko isiyo halali .

Nafikiri tunachoka sana . Mungu mpaka lini mambo haya ?
=====

Wamiliki wa Shule Binafsi walioenda kutoa rambirambi katika Shule ya Msingi ya Lucky Vincent wakiwa na waandishi wa habari wamewekwa chini ya ulinzi na polisi shuleni.

Mwandishi wetu ambaye yuko eneo la tukio hivi sasa ameeleza kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya Arusha ambaye hajamtaja jina amewaambia kuwa wako chini ya ulinzi kwa kosa la kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria.

Mwandishi wetu ameeleza kuwa katika msafara huo pia yupo Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro, viongozi wa dini, wazazi waliofiwa na waandishi kama 10.

Chanzo: Mwananchi
Siasa za ccm ni za kishamba sana ! Hivi wanadhani watatumia polisi hadi lini ? Ni bora Kinana alivyoamua kujiuzuru tu kuepuka aibu .
 
Naona kuna ukweli kwamba Mrisho Gambo kapiga pesa za rambirambi. Sasa ameamua kujilinda dhidi ya wanaotaka kumuumbua kwa kuanza kuwakamata na kuwasweka lupango. Hii ni AIBU kwa dola.
Hivi ulidhani tuhuma hizo ni za kughushi ? Mkuu lengo la ccm kwenye nchi hii ni kuhakikisha watanzania mnabaki mifupa mitupu , hawajawahi kuwa na huruma .
 
Back
Top Bottom