ARUSHA: Meya, wamiliki wa shule, paroko na Waandishi, wakamatwa na Polisi Shuleni, wanyimwa dhamana

ARUSHA: Meya, wamiliki wa shule, paroko na Waandishi, wakamatwa na Polisi Shuleni, wanyimwa dhamana

Kutoa rambirambi ni matakwa ya mtu binafsi na hauwezi kumpangia mtu namna ya kutoa rambirambi. Za kwanza mlizila na hizi kidogo mnataka kula tena?
 
Kamanda wa police arusha anasema waandishi wa habari hawakukamatwa bali walipewa lifti waandishi wanasema tulikua na magari yetu na yamebaki shuleni
 
*KUKAMATWA VIONGOZI CHADEMA ARUSHA*


*Na Felix Mushi,Arusha*

Niko hapa eneo la tukio Shule ya Msingi Lucky Vicent iliyopo Olasit Jijini Arusha, Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha, na Viongozi wengine wa Chadema wamekamatwa wakiwa kwenye mkutano na wazazi wa watoto waliofariki kwenye ajali hiyo.

Katika kikao hicho Meya wa Jiji alianza kwa kutoa pole kwa wafiwa na kuwaeleza kuwa ametumwa na Mbunge ili kuwapa pole za kipekee kwa msiba huu na zaidi ameelekezwa kuja kuwajengea ujasiri wazazi ili waendelee kudai fedha zilizoliwa na wajanja.

Akawaeleza kuwa wao kama Chama makini wako pamoja na wafiwa kwa hali zote na kwamba lazima haki itashinda. Pia aliwafafanulia kuwa ni jambo la aibu kuona wadau mbalimbali wametoa fedha lakini watu wachache wanakula michango hiyo lakini wanaachwa.

Kabla hajaendelea na maelezo hayo, alisimama mzazi aliyejulikana kwa jina moja la mama Ivo ambaye alimuuliza Meya juu ya fedha milioni 10 ambazo Mbunge na uongozi wa CHADEMA waaliahidi walipokuja kuwapa pole siku ya msiba kwamba ni vyema wangezitoa ziwasaidie kuliko kuendelea kuwaeleza juu ya wizi wa rambirambi ambazo hata hawana uchungu nazo. Aidha alumina Meya Alasdair kurejeshewa fedha za ada ambazo walilipa shuleni siku moja kabla ya ajali kwani ni haki yao.

Swali hilo liliamsha shangwe na vigelegele kutoka kwa baadhi ya wazazi huku wengine wakiguna kichinichini. Hata hivyo Meya aliwaeleza kuwa fedha ambazo wao kama CHADEMA waliziahidi wasiwe na hofu watazipata lakini hiyo siyo agenda iliyowaleta leo! Akawaomba wamvumilie kwani yeye na viongozi wenzake watatafuta siku muafaaka ambayo Mbunge atakuwepo ili awakabidhi mwenyewe. Alitumia nafasi hiyo pia kuwasihi wafiwa wapuuze maneno ya mtaani kwamba CHADEMA hawajachangia chochote zaidi ya kufanya siasa Kwenye mitandao. Akawahakikishia kuwa fedha hizo watazipata kabla ya tarehe 21 Mei.

Hata hivyo maelezo haya yalionekana kutojitosheleza kwa baadhi ya wazazi ambao waliendelea kuguna na wengine wakizomea huku wengine wakionyesha kufurahishwa na majibu hayo na wakizomea kwa nguvu. Fujo za kutosikilizana zilipoendelea iliymlazimu mzazi mmoja kuwapigia simu polisi kuja kudhibiti sintofahamu iliyojitokeza. Naamini watakuwa wanaendelea kutoa maelezo huko!

Hasira za Baadhi ya wazazi hao pamoja na walimu ni kuchoshwa na kile walichokiona ni usanii wa baadhi ya viongozi kuendelea kutumia msiba huo kama ngao ya siasa huku wakiwa hawatoi michango waliyoahidi zaidi ya kupiga danadana.
____
Nitaendelea kuwajuza kinachoendelea juu ya Muvi hii nzuri!
tmp_5880-Screenshot_2017-05-18-14-43-321150168722.png

Mmekula rambirambi mmeona haitoshi mmewakamta na watoa rambirambi.

Hakika huu ndio "UONGOZI UNAOACHA ALAMA."
 
IMEFIKA WAKATI TUHESHIMU MAMLAKA ZILIZOPO.HAIWEZEKANI UTARATIBU ULIWEKWA TOKEA MWANZO KUWA HELA ZOTE ZA RAMBIRAMBI ZIPELEKWE KWA MKUU WA MKOA ARUSHA,HALAFU LEO MSTAHIKI MEYA ANAKWENDA KUGAWA HELA MOJA KWA MOJA BILA KUFUATA UTARATIBU.HII NI DHARAU YA HALI YA JUU NA SEREKALI HII HAITAKIWI KULIFUMBIA MACHO SWALA HILI HATUA KALI ZICHUKULIWE DHIDI YA MEYA HUYU NA WENGINE WATAKAO MJARIBU MH GAMBO.HAIWEZEKANI KUFANYA DHARAU YA NAMNA HII HATA BUNGE LILIFUATA UTARATIBU HUU NA LIKATUMA HELA KWA MKUU WA MKOA IWEJE MEYA AFANYE KINYUME.NAOMBA TUACHE SIASA KATIKA MAMBO YA MSINGI KAMA HAYA MHE.GAMBO AACHWE AMALIZIE KAZI ALIYOIFANYA KWA KUJITOLEA NA KWA UAMINIFU MKUBWA.
Huwezi kumpangia mtu jinsi ya kutumia hela yake. Period.
 
Serikali hii ina penda kufatilia vitu vya ajabu sana.kama watoto vile.unaweza ukajiuliza hawa wazima kweli?
Jeshi la polisi ndo kabisaaaa.
Twendeni/nendeni huku wanaenda tu.inasikitisha sana

Wanapenda kufanya hivyo,halafu wakilalamikiwa wanajiona wanadharaulika
 
Nachokijua upinzani wajiandae kisaikolojia uchaguzi ujao kuna wabunge watatangazwa kwa lazima hata kama watakua waneshidwa kwa namana police tunavyokwenda nayo
 
Pale unapojaribu kuzima moto kwenye nyumba ya nyasi kwa kutumia mafuta ya petrol. .. sikuzote mwisho wa ubaya huwa ni aibu tu.
 
Mwendawazimu anapopewa dhamana ya kuongoza watu. Huyu RC kipo anachotafuta. Uongozi ni karama.
 
Vipi unahisi mambo ya Kibiti yanaweza kusambaa hadi AR?
Hatuombei iwe hivyo lakini pia yakitokea usishangae coz hivi pia ni viashiria vya kuelekea huko. Nadhani tutumie nguvu zetu zote kukemea vitu kama hivi.

Mungu ibariki Tanzania, uwape hekima zaidi watawala wa awamu hii.
 
Mmekula rambirambi mmeona haitoshi mmewakamata na watoa rambirambi.

Hakika huu ndio "UONGOZI UNAOACHA ALAMA."
 
Back
Top Bottom