ARUSHA: Meya, wamiliki wa shule, paroko na Waandishi, wakamatwa na Polisi Shuleni, wanyimwa dhamana

ARUSHA: Meya, wamiliki wa shule, paroko na Waandishi, wakamatwa na Polisi Shuleni, wanyimwa dhamana

Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema akizungumza baada ya Meya wa Arusha kukamatwa na Polisi maeneo ya shule ya Lucky Vincent.
MSIKILIZE

Atoe jibu gari ya St Vincent haikuwa na bima majeruhi na wafiwa atawasaidiaje kulipwa fidia na mumiliki wa hiyo shule. Waandishi wa habari mkomalieni lema aeleze anawasaidiaje kupata fidia zao. Mtoleeni uvivu.
 
Sijutii kutoipigia kura CCM toka nifikishe umri sahihi wa kupiga kura... hakuna marefu yasiyo na ncha. Shame
 
Kipindi ambacho watoto wetu wanahitaji wataalam wa tiba za saikolojia ili kuwapa nasaha baada ya kupoteza marafiki zao, wanasiasa wapumbavu wanatafuta umaarufu!
Wale watoto akili zao hazijakaa vizuri, ugeni wa watu ambao sio wale waliozoeleka hapo shuleni vinaamsha majonzi upya! Wanasiasa acheni uharamia na tamaa!
Nimetafuta tusi zito limekosa,........Mungu nipe moyo wa uvumilivu!
Dah kwa akili hz kila mtu atafute maendeleo yake binafsi. Itakuwa vigumu sana kuendelea kwa pamoja kama nchi.
1. Hv ukipewa rambirambi na mtu usiyemjua unaathirika kisaikolojia?
2. Hv raia kutembelea shule tena ambayo inataarifa ya ugeni kunahitaji kibali cha RC ama polisi?
3. Ni mara ngapi watu wanatembelea shule na kutoa misaada ama hospitali kutoa pole misaada? Je huwa wanapewa vibali na ma-RC ama polisi?
4. Hv siku hz ukifiwa unahitaji wataalamu wa saikolojia badala ya pole?
5. Kumbe wale watoto wa lucky vicent na shule zingine waliokuwa pale sheikh amri abeid walihitaji wataalamu wa saikolojia badala ya kupewa pole na waheshimiwa na raia wengine waliokuwa pale kuaga?
Dah najiuliza mengi kwa hii comment yako nakosa majibu. Hv kwann siasa inatufanya wajinga kiasi hiki? Kwann tunafikiria kwa kutumia siasa badala ya akili?
 
Kwa hiyo wamebaki Mayor na Madiwani??AU issue ilikuwa kumweka Mayor ndani??
Meya na madiwani bado wanaendelea na mahojiano sababu bado hazijatolewa labda wao walipewa lift kama sisi
 
Compensation ni lazima, shule iuzwe awalipe wazazi wa majeruhi na waliofiwa, gari haikuwa na bima, aasalale jamani!
 
Meya na madiwani bado wanaendelea na mahojiano sababu bado hazijatolewa labda wao walipewa lift kama sisi

Sasa hao wengine wameulizwa nini??Au Mla RAmbirambi alizitaka rambirambi akafanye nazo karamu??
 
Hivi ni nini maana halisi ya rambi rambi. Utampangiaje mtu hela zake ambazo anatoa kwa ihari.

Rip watoto..... sio nia yetu kuendelea kulumbana kwa ajili ya swala lenu.
 

Mstahiki Mayor wa Jiji , Paroko , Mchungaji , Waandishi wa habari 7 , wamekamatwa leo na Jeshi la Polisi wakiwa Shuleni Lucky Vicent ambako Mayor alialikwa na Umoja wa Shule binafsi Tanzania , waliopenda kutoa rambi rambi moja kwa moja kwa wafiwa badala ya kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa .

Wazazi waliokuwa hapo wamepatwa na taharuki kubwa baada ya kuona viongozi hao wanachukuliwa bila sababu yoyote ya msingi , mpaka sasa wako Polisi wanaambiwa walikuwa na mikusanyiko isiyo halali .

Nafikiri tunachoka sana . Mungu mpaka lini mambo haya ?

======

UPDATES: 1

Waandishi waliokamatwa na jeshi la polisi Arusha kwa madai tulihudhuria kikao ambacho hakikua na kibali katika shule ya Luck vincent ambapo shirikisho la wamiliki wa shule binafsi walikuwa wanaendwa kutoa rambirambi. Sisi tulipata taarifa tukaenda kufanya kazi.

1 .Godfrey Thomas -ayo tv

2.King Alphonce Saul Kusaga

3.Filbert Emmanuel -mwananchi

4.Husein Tuta ITV

5.Joseph Ngilisho -Sunrise radio

6.Geofrey Stephen -Radio 5

7.Janeth Mushi -Mtanzania

8.Zephania Ubwani -The Citizen

9.Elihuruma Yohani -mwakilishi wa Tanzania Daima

10.Idd Uwesu - Azam Tv

UPDATES; 2

Waandishi wa habari waliokamatwa Arusha leo katika utoaji wa rambirambi shule ya Lucky Vincent wameachiwa, polisi waliwaambia waliwapa lift tu.

UPDATES: 3

Kaimu RPC wa Arusha Yusuph Ilembo amesema watu wote waliokamatwa leo shuleni Lucky Vincent ni utekelezajiwa wa agizo la RC wa Arusha Mrisho Gambo

UPDATES;
Wamiliki wa Shule Binafsi walioenda kutoa rambirambi katika Shule ya Msingi ya Lucky Vincent wakiwa na waandishi wa habari wamewekwa chini ya ulinzi na polisi shuleni.

Mwandishi wetu ambaye yuko eneo la tukio hivi sasa ameeleza kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya Arusha ambaye hajamtaja jina amewaambia kuwa wako chini ya ulinzi kwa kosa la kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria.

Mwandishi wetu ameeleza kuwa katika msafara huo pia yupo Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro, viongozi wa dini, wazazi waliofiwa na waandishi kama 10.


Chanzo: Mwananchi

Hivi kuna mtu ambaye hajachoka!! mods leteni ban haraka tena maanake mimi nimejizuia mno kuwatukana hawa umbwa
 
Wee ndo hamnazo kabisa hao viongozi walienda kula au kusaidia kumbe nyie maccm ndo tabia yenu mkiona misiba hata nyumbani hamuachi hela ya mboga, yaani hata aibu huoni eti viongozi wangekula nini,,

Pesa ipo over 50m hiyo haijabaki!? Mnalalamikia kiasi kidogo mnachotamani mpewe ha ha aaaaa

Semeni mengine inatia aibu nchi yetu.
 
Back
Top Bottom