ARUSHA: Meya, wamiliki wa shule, paroko na Waandishi, wakamatwa na Polisi Shuleni, wanyimwa dhamana

ARUSHA: Meya, wamiliki wa shule, paroko na Waandishi, wakamatwa na Polisi Shuleni, wanyimwa dhamana

"You Gonna Leap What You Saw" by Late Luck dube.

Nionapo haya huku kiongozi mkuu wa nchi akiwa kimya kana kwamba anafurahi juu ya yote yanayotokea nakumbuka wimbo wa Hayati Luck Dube. YOU GONNA LEAP WHAT YOU SAW, na hakika watavuna wanachopanda. Ipo siku rambirambi zao tutazikusanya na kuenda kununulia chakula cha NGURUWE.
yeye ni mtumaji mkuu
 
Vyama vya upinzani nendeni vijijini anzieni huko

Hapa baba sio vyama ni haki dhidi ya udhalimu wa dola, Mie sina chama na huyu bwana tulimpigania kwa kuamini atakuwa msikivu na binadamu.
 
Kutoa rambirambi kwa wafiwa kibali cha nini?
Mkutano unafanyika ndani ya premises za shule kibali cha nini?
 
Lema amekamatwa jana?
Lema
Kachoka kukamatwa aliorganise akamwachia msaidizi wake yeye akasepa. Sababu alijua kitakachotokea kambwagia msaidizi wake wa ofisi ya mbunge .Huyo meya hajitambui lema kamwingiza Mkenge kamwachia soo. Huyo yuko huru wasiojielewa aliowatumia wako Ndani. Siku ingine watumie bongo zao wazishirikishe pia.Sasa hivi lema naona kabuni staili mpya yeye anasukumizia wengine mwenyewe anasepa ili nao waonje mahabusu kama yeye. Anawatungia halafu anawabwagia
 
Kachoka kukamatwa aliorganise akamwachia msaidizi wake yeye akasepa. Sababu alijua kitakachotokea kambwagia msaidizi wake wa ofisi ya mbunge .Huyo meya hajitambui lema kamwingiza kamwachia soo. Huyo yuko huru wasiojielewa aliowatumia wako Ndani. Siku ingine watumie bongo zao wazishirikishe pia

Usishabikie upuuzi maana yake ni RAIS ndiye anayeaibika hapo rafiki.Tanzania yetu sote,Taifa letu sote kwanini chuki na visasi??Itawapeleka wapi?
 
Ipo siku kuna watu watatamani dunia ipasuke wajifiche!Wanaacha alama hasi ktk jamii.Historia yao wanaiandika vibaya.Wabadilike dunia ijayo iwe na chakujifunza kutoka kwao.
 
Jamaa alikuwa anafuatilia ukweli wa mgawanyo wa rambiramb na kupeleka rambarambi nyingine moja kwa moja kwa wafiwa bila kupitia "middle man/mtu wa kati(RC/serikali).Maana kuna kipengere kilisema chakula na vinywaji vya wageni wa meza kuu ilikuwa milioni 4.3(?),wakati hakuna mtu wa meza kuu aliyekula hata kidali cha bata mzinga,watu walimaliza kuaga wakaingia kwenye magari kukwepa mvua.Sasa hiyo milioni 4 ya chakula na vinywaji ilikuwajekuwaje?

Wafiwa walipewa milioni moja,na baadae wakahaidiwa kupewa milioni 2 na ushee zilizobaki,sasa maswali ikawa,inakuwaje rambirambi zinakuja nusunusu wakati zilitolewa kwa pamoja?

Walisema Serikali itagharamia safari na mazishi ya watoto,walimu na madereva.Lakini kwenye mchanganuo wanaonyesha kuwa pesa za rwmbirambi zilitumika kulipa madereva na magari ya usafiri,wakati kina Chambili,Kampuni ya Leopards na wadau wengine walichangi kama msaada,sasa hizo zilipoteaje?

Kudhihirisha chuki ya Kisiasa,siku ya msiba Gambo alitangaza CHADEMA kama Chama kimetoa shilingi milioni 5,Lakini kwenye mchanganuo wa jedwali lake,hajaweka CHADEMA kama chama kilichochangia,zaidi kawaweka UWT-Taifa,CCM mkoa wa Arusha nk...Sasa haya mambo ndio yanajenga machuki yasiyo na maana.

Wanamtumia Nyalandu kupenyeza "userikali" kwa kuwapeleka watoto marekani,Lakini ukiangalia website ya hawa jamaa,utaona kuwa wao walitaka siku ileile watoto wapelekwe US kutibiwa,lakini urasimu wa serikali na Gambo kwa "kiburi" kuwa serikali itawatibu kiliwachelewesha,mpaka wakatumia nafasi ya Makamu wa Rais alipoenda Hospital Mount Meru,wakawasakizia wale wamama wenye watoto kumsihi Mama Samia watoto waende nje kutibiwa kwa msaada wa Wazungu.

Halafu wanajidai kusema "Uongozi unaoacha Alama"...Hizo ni alama gani?au za chuki na visasi?Buree kabisaa
Well said mkuu, mambo na wenzake wanatafuta cheap political millage,wangewakamata na wafiwa ijulikane ,Kwanzaa nini wengine wamewaacha,kitendo cha kuwakamata meya na viongozi wa dini inaonyesha culclations zao zimefeli.
 
meya si kama DS anachaguliwa na mkulu. uache uongo meya ni diwani na diwani amechaguliwa na wananchi kufikia udiwani badala ya hapo ndio anagombea umeya ila anatokana.na wananchi hakuna mfumo wa kutoka nje kama bungeni.

Afu na we eti unajiita msomi!! nimekuuliza swali dogo tu meya anachaguliwa na wananchi!!!? unajib majib mengiii ht ambayo hujaulizwa .....
 
Wewe nikikutafsiri nashindwa kuvuta taswira ambayo inaweza kukufaa, akili umeamua kuitupilia mbali kabisa na unaanza kutumia utashi wa mnyama ambaye hajui huyu ni mama yake au mwanae yeye.
Muda ndio jibu!!!

Kwahyo na we unajiona umeandika hapo!!! muda wa nn!! muda ndo huu watu wanatenda we endelea kuusubiri ....punguani we!
 
Idd Amin pamoja na mabaya yake yote lakin bado kuna baadhi ya Watu walimpenda,kwa hiyo na Gambo pamoja na kula rambi rambi za wafiwa bado kuna Watu wanaona yupo sahihi,kwa hiyo kila Shetani na Mbuyu wake,ila mim nauona ni upuuz kutetea upuuz na ni ujinga kujitoa akili kwenye ukwel

Mfano wako mbna hauna uhalisia...acha chuki binafsi...wacha watu wapige kazi...wewe mbna uligombania mali za marehemu pale mtaani kwenu...kisa lema hajahusishwa kwenye rambirambi povu linakutoka...
 
Wakati wapinzani mkifikiria juu ya ubunifu hebu tuchambue tukio la Arusha.

Rc anaagiza watu wanaopeleka rambirambi wakamatwe.
Labda tuulizane.
Siku ya jana familia ngapi mkoani Arusha walipelekewa rambirambi, au walikuwa na maziko watu wakakusanyika na wengine kutoa rambirambi zao?
Je, katika makusanyiko yote hayo, Rc ameliona hilo moja tu kwamba ni HATARISHI?
Je, katika makusanyiko yote hayo, je yote yaliomba kibali isipokuwa hawa waliokamatwa?
Je, hiyo hatari ya kusanyiko ilikuwa kwa nani hasa,
Hatari kwa mkuu wa mkoa?
Hatari kwa raia?
Hatari kwa shule?
Hatari kwa wafiwa?
Hatari kwa waandishi? (Wao waliachiwa)
Je, ni hatari ipi inayozungumziwa?

Polisi walipewa amri ya kukamata.
Maana yake ni kwamba wao kama wao HAWAKUONA kosa la kuwakamata hadi amri ilipotoka.
Sote tunajua kuwa, mara zote ambazo mikusanyiko na maandamano kuzuiwa, polisi ndio wenye kutoa amri, na sio KUPOKEA amri (sizungumzii amri za kisirisiri kama zipo), kwa kuwa HAIJAWAHI KUTOKEA mkusanyiko kuzuiliwa na kiongozi. Mara nyingi polisi husema "intelijensia" inaonesha kutakuwa na uvunjifu wa amani...

Kwa maana hiyo, amri hiyo inatufanya tutafsiri kuwa labda kwa tukio hilo polisi hawakuijua kazi yao, hadi walipokumbushwa na Rc....

Lakini....
Tatizo ni kutoa rambirambi?
Tatizo ni uwepo wa waandishi?
Tatizo ni kuwapelekea wahusika?
Tatizo ni kutokumuamini RC kama mpokeaji rambirambi upande wa serikali?

Haiwezekani tusimame watu kumi nyumbani kwa fulani, kisha wanne wakamatwe wanavunja amani, watatu wapewe lifti, kwamba wao walikuwa wanakwenda "kushuhudia" uvunjifu wa amani, na mwenye mji aliyetukaribisha abakizwe, wakati yeye ndiye aliyepanga tukusanyike tuivunje hiyo amani.... It's quite absurd!

Lengo lilikuwa ni kukabidi hiyo rambirambi... Lengo likavunjwa na amri, lakini tumejua kuwa ilikuwa kiasi gani... Mil 18, hivyo nguvu yote ile haijaweza kuficha ukarimu wa umoja wa shule binafsi....

Halafu....
Kimantiki kabisa, RC ni mtu mkubwa sana kujishughulisha na mambo ya rambirambi. Haki vile! Yaani majukumu yake ya MKOA mzima wenye kila aina ya kero, aache kushughulikia suala la maji, barabara, madawa, elimu nk, ahangaike na nani kaenda kuhani msibani?? Hivi viwanda tunavyoimba vinajengwa na fedha ya rambirambi?

Nadhani wapo viongozi katika maeneo mengi HAWAJUI maana ya nafasi walizonazo. Yaani ni sawa na baba mwenye nyumba aache kwenda kazini, anaketi anavizia nani anachuma waridi bustanini...au nani atawasha moto wa mkaa kwa makaratasi ya rambo wakati ameagiza uwashwe kwa mafuta ya taa! Sasa hausi geli afanye nini?

Kwa upande upande wa wale waliopewa "dezo" kwenye gari ya polisi, wanatakiwa wajue ile haikuwa dezo, lengo la RC kuagiza waachiwe ni namna ya kukwepa kile kilichomkuta mwenzake. Naamini ndiye aliyesema waachiwe, kwa sababu, haiwezekani polisi watumwe kukamata wahalifu halafu watoe lifti kwa wasio wahalifu. Ama utaratibu wa kutoa lift umeanza lini? Kwamba wale waandishi walifikaje pale mara ya kwanza?, je walikuwa wanasubiri defender ya lift wakishamaliza shughuli zao? Waandishi mmekubali na kuridhika kwamba mlipewa kadezo hadi polisi? Kama waliwapa lift kwa nini wawashushie polisi, au mnaishi hapo kituoni?
Ah! Mambo mengine yanaudhi sana!

Serikali ya ccm msipoondosha viongozi wajinga wenye kupenda sifa za kijinga uhalali wa kuaminiwa umekufa
 
Back
Top Bottom