TheCrocodile
JF-Expert Member
- May 31, 2021
- 1,864
- 5,254
Ni swali gumu pia lenye majibu tata.Duuh miaka 11 anapata vp mawazo ya kujinyonga?
Ni hatari sana. Mambo ni mengi.Mhhh, Saivi hata waliopo tumboni wataanza kujinyonga. Kila kundi linastress zake
Kwa wenzie shuleni, au aliona kwenye TV au mitandaoni huko Youtube. Dunia ya sasa hivi ya tofauti sana.Duuh miaka 11 anapata vp mawazo ya kujinyonga?
Kweli kabisa, inawezekana dogo alijua labda atarudi.... Hata hiyo barua yake anaomba pia mama yake apate hela ya ada (kwa ajili yake)Ni swali gumu pia lenye majibu tata.
Ninafikiri utandawazi unachangia.
Dogo anawekana aliona tukio kama hilo kwenye mitandao ya kijamii la mtu kujinyonga na kuacha maandishi.
Kwa umri wake akaamua kuigiza bila kujua kwamba kwenye maigizo, kipengele cha "kujitundika" kuna utaalamu wake.
R.i.p toto..!
Inawezekana kabisa!Kinanisikitisha mimi alifanya hivyo akidhani kuna come back kumbe ndiyo nitolee,hapo aliposema Baba na mama wapate ada ya shule kalidhani kataenda karudi kakute wamepata ili kaendelee na masomo.
Mungu akurehemu binti
Mungu atusaidie kizazi cha sasa hivi mambo yamebadilika sana.Aiseee 🙌
RIP Lightness.Mtoto mmoja wa kike mwenye umri wa miaka 11, darasa la sita anayefahamika kwa jina la Lightness Mkiindi, mkazi wa Mtaa wa Namayana, Kata ya Ilboru, wilayani Arumeru mkoani Arusha, amefariki dunia akidaiwa kujinyonga
Kwa mujibu wa maelezo ya mama mzazi na bibi wa marehemu, siku ya tukio Januari 29, mtoto huyo hakuenda shule kutokana na kuwepo kwa msiba wa jirani uliokuwa karibu na makazi yao, ambapo familia ilikuwa ikishiriki shughuli za maombolezo. Kabla ya tukio hilo, inaelezwa mtoto alikuwa nyumbani akicheza na wenzake.
Familia imesema walipokea taarifa ya dharura wakati wakiwa msibani, iliyomtaka mama wa mtoto kurejea nyumbani haraka. Alipofika, alikuta mtoto huyo tayari amefariki katika mazingira yanayoashiria alijinyonga kwa kutumia kanga ya kuogea.
"E baba Mungu ninaomba kwa niaba ya familia yangu na jamii nzima pamoja na majirani, Mungu naomba umpe bibi yangu hela pamoja na mama yangu pamoja na baba yangu, bibi yangu apate hela ya marejesho na baba na mama wapate hela ya ada ya shule. Mungu atusaidie, Milele Amina amefanya maajabu jina lake liimidiwe" ameandika mtoto ambaye anadaiwa kujinyonga bafuni.
Chanzo cha tukio hilo bado hakijabainika mara moja, huku tukio hilo likiacha majonzi makubwa kwa familia, ndugu na wakazi wa eneo hilo.
View attachment 3537053
Kwa sababu kamtaja Mungu kwenye ujumbe alioacha?RIP Lightness.
Imani ya Mungu inechangia kifo hiki.
Inasikitisha sana.Daah! Ameandika kama mtu mzima.
Pole kwa familia.
Inawezekana. Kipindi cha balehe huwa kina mihemko na misukosuko mingi sana.Nafikiri balehe imechangia mihemko katika hili.
Kabisa kwa umri aliokuwa nao huyo dogo hii dhana inakuwa na mashiko zaidi.Inawezekana. Kipindicha balehe huwa kina mihemko na misukosuko mingi sana.